BINTI USIONGOZWE NA MACHO YA WATU

 BWANA Yesu ASIFIWE mabinti wazuri kabisa...

Leo Ni siku nyininge ambapo natamani tujifunze Jambo moja zuri San kwaajili ya mamufaa yako...

Ni kuhusu  MACHO YA WATU YANAVYOHARIBU MAISHA YA BINTI...

Ni kweli kabisa kwamba kwenye jamii huwa Kuna watu ambao huongozwa na macho ya watu fulani

👉watu wengi Leo hii wanafanya uamuzi fulani kwasababu ya watu fulani ambaonwapo kwenye jamii yao...

👉ukiangalia maneno ya Yesu alipokuwa akizungumza Ni ishara kamili kwamba alizungumza like alichotumwa na Wala si Kama vile wanavyotaka watu.....


Yohana 6:38

Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.


Sasa hii ilimfanya Yesu kufanya Jambo sahihi kwa wakati ule bila kujali kwamba watu watalikubali au watakataa

👉sasa niketoa mfano huo wa Yesu ili kukuonyesha ni kwa namna gani mabinti wenge na vijana wengi huingia katika ndoa na watu wasiosahihi kwasababu tu ya kuwatazama watu wanaowazunguka.....

👉Ni kweli kwamba Kuna sifa fulani Binti anaipata kutoka kwa rafiki zake au ndugu zake kwakuolewa na Dactari bingwa, Mwanajeshi, mwanasheria, Mwenye pesa nyingi au mtu maarufu Yeyote Yule...

👉Jambo hilo huwafanya mabinti wengi kuangalia na kujiandaa kwa nguvu kubwa ili tu kuja kufanya Jambo ambalo wengi watamsifia nankutamani kuwa Kama yeye, pasipo kujua madhara ya Jambo hilo....

Ni lazima ujue Kwamba kwa kufanya Jambo ili likupatie utukufu fulani, Basi unaweza kujikuta unaolewa na mtu asiye sahihi...

👉kwanza Ni lazima uje kuwa maisha ni yako mwenyewe hivyo kama ni kilio utakipata wewe na Kama Ni kicheko pia utakipata wewe mwenyewe..Sasa Kama ni hivyo Basi hata uamuzi..yafaa Sana Kama wewe ndiye utahusika kwa asilimia 90% katika kufanya uchaguzi sahihi

NI HIVI👇

👉Unaweza kumuhitaji Dactari lakini kumbe Hana upendo na mwisho wake uanze kuchanganywa na wanawake wengine kwenye ndoa yako

👉Unaweza mpenda mwenye Mali na fedha lakini kumbe akakudharau na kukuona mtumwa kwake

👉Anaweza kuwa kila kitu, kama Nyumba,gari , pesa  lakini kumbe Hana Mungu

🌝Hivyo unavyokuwa unamtazama mwanaume sahihi usijaribu kuyahusisha macho ya watu wengine namna na jinsi watakavyokutazama..Bali fanya maamuzi sahihi...

Tena Ni lazima ujue haya👇

👉mtu anaweza kuwa sahihi kwako Ila rafiki zako wasimkubali

👉mtu anaweza kuwa sahihi kwako lakini wewe mwenyewe usijue na kumtazama kwasababu tu Kuna macho ya watu fulani ambayo unatamani yakuone ukiwa na mtu fulani wa Kiwango Cha juu...

👉 mwanaume anaweza kuwa sahihi lakini hata jamii isimfikirie kwako.....


LAKINI LEO

👉Natamani usifanye Jambo la kimaisha kwasababu ya msukumo na ushawishi wa watu Tena hasa Jambo nyeti Kama uchaguzi wa Mume

👉 Tambua kwamba Ni vizuri Sana kama utaanza na mtu asiye na jina na baadae mkapata jina ..kuliko kumkuta Mwenye jina/kitu halafu na wewe ukajipachika hapo ...kwasababu itakuwa rahisi Sana kukutupa nje pale atakapojisikia mwenyewe kwasababu huna mchango wa jina lake kufika alipo labda. daktari, mwanasheria, Mwanajeshi, tajiri n.k

katika hili sisemi umkatae tajiri Bali lengo langu ni kwamba USIMKATAE MTU KWASABABU UNÀMTAKA MTU FULANI KWA MACHO YA WATU FULANI ...Wala pia sisemi umkatae asiye na jina kubwa Bali usifanye uchaguzi ili ujionyeshe ubora wako ...

Mtaji wa kipekee ambao kila mwanaume utakayemkubali Ni lazima awe nao Ni MUNGU

 👉Kabla hujaenda kwenye sifa yoyote Basi jiulize JE ANA MUNGU..?, 

usiangalie visivyovyaa Bali vifaavyo


Zaburi 119:37

[37]Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, 

Unihuishe katika njia yako.


          Mungu akubariki Sana


laddies in Christ

MwlEv Mathayo Sudai

0744474230/0628187291

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI