KUWA MAKINI NA MAMBO HAYA MANNE KWENYE UCHUMBA


 KUWA MAKINI NA MAMBO HAYA MANNE KWENYE UCHUMBA

Bwana Yesu asifiwe mabinti wazuri ndani ya Kristo

Karibu katika kujifunza mambo manne kati ya mengi mazuri unayotakiwa kuyafanya kila siku kama unajiandaa kuwa na Familia nzuri...

Kwanza awali ya yote ni lazima ujue kuwa familia inaundwa na BABA, MAMA pengine na watoto...

👉Hao wote wanamchango mkubwa sana katika kuisimamisha nyumba hiyo...

👉Lakini ndani ya Biblia ni mtu mmoja tu ndiye mwenye uwezo wa kuivunja nyumba na huyo si mwingine bali ni MWANAMKE na kibaya zaidi anao uwezo wa kuivunja kwa mikono yake mwenyewe...

Mithali 14:1

[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; 
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Sasa tutoke huko...Leo tuangalie mambo manne ambayo unatakiwa tuyatazame kila siku kama wewe ni binti unayejiandaa au unayehitaji kuingia ndani ya ndoa..


HAYA HAPA 👇

1: MUOMBEE MUME WAKO

Unapokuwa umepata mchumba au hata kama hujapata Basi ni lazima ujue kuwa wewe ni mtu ambaye utakamilisha mfumo ndani ya nyumba na utapokea utaratibu kwa mumeo kila siku maana ndiyo amri ya Mungu kwamba Mwanamke awe chini ya mwanamume..

👉Sasa shetani akiwa analijua hilo, anaweza kuamua kukuwekea mipango ya kukuangamiza kabisa kupitia ndoa yako...utakuta una mtu mzuri tu lakini akisha kuoa mambo yanabadilika mpaka unaaanza kusema mbona Mwanzo hakuwa hivyo...lakini Leo hii ni lazima uanze kupinga hila za shetani katika kumtumia mume kama sababu ya upotevu wako kupitia pengine udhaifu alionao...

NA Mungu atakupigania hata shauri lake kusimama...

Mithali 19:21
Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.
[21]Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; 

Hivyo Usikubali kukatishwa tamaa au hata kuteseka na kufa kwaajili ya hila za shetani ..Hakikisha unamuombea kumuandaa kwaajili ya Familia yako ...na hapo ndipo unakuwa unaijenga nyumba kwa misingi imara...


2: USIWE WA BEI RAHISI

Unapojiandaa kwaajili ya ndoa yako, Usikubali hata siku moja ukajiweka katika namna ambayo kila mwanamume akaweza kukufikia.

👉Ni lazima ujue kuwa unapojiweka na Kujirahisisha sana kwa kila mwanamume..Basi unakuwa unajishusha thamani bila kujua ...na Wengi watakuchezea

👉Na ni lazima ujue mume wako anahitaji kuiona thamani yako, hivyo ilinde sana thamani yako na mtu yeyote asije akaishusha.

👉Hapa utashinda pale tu utakapokaa mbali na wanaume wasiofaa waendao pasipo utaratibu mzuri ambao mara nyingi huwaharibu watu na kuwapotezea Muda.

2 Wathesalonike 3:6

[6]Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu...


3 KUWA MAKINI NA RAFIKI

KUNA mambo mengi na matatizo mengi ambayo huletwa na rafiki asiyefaa ...

Sasa unapojiandaa kuwa ndani ya ndoa maana yake wewe si mtoto tena bali ni mtu mzima Kwahiyo angalia Aina ya watu unaowaweka kuwa karibu yako kama rafiki..

👉Kuna wanawake wengine hutakiwi kuambatana nao kama marafiki kwasababu wanaweza kukufanya ukafanya maamuzi mpaka ukayajutia na ndiyo maana wengi ukiongea nao utaona wanataja rafiki zao kama ndiyo sababu...

Asilimia 90% ya Wengi waliowahi kuharibikiwa chanzo chake ni rafiki au wale wanaofuatana nao

1 Wakorintho 15:33
[33]Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

Unapomkaribisha rafiki asiyefaa atakuharibu na kujutia maisha Yako..

👉Ukilitazama hilo utakuwa ni mtu wa thamani sana...


4: USIWE NA MAAMUZI YA HARAKA

Mhubiri 7:9
[9]Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, 
Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

MAAMUZI ambayo watu huyafanya ndiyo huwa yanawafikisha pale walipo...

👉Kila uamuzi ulioufanya ndiyo uliokufikisha hapo ulipo...

👉Katika kipindi cha uchumba usiwe na maamuzi ya haraka kwa kila kitu utakachokiona kwasababu Kuna wakati shetani atakujia kwa lengo la kukurudisha nyuma ..

Utashangaa ghafla Kuna kitu mwenzako amekifanya ambacho pengine si kizuri ..Lakini katika hilo pasipo kujua ni kwamba shetani anakuwa anakulenga wewe akisubiri useme NI BORA TUACHANE....

Japo hilo laweza kutokea kama ikibidi lakini ni lazima Uwe na hekima na utulivu ili tu kutokufanya maamuzi yasiyo sahihi....

Mithali 23:20
Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
[20]Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; 

Kwasababu hata shetani mwenyewe hapendi Uwe na ndoa au mume mzuri hivyo ni lazima atakuletea vikwazo ..lakini wewe kushinda ni kuwa mtulivu, epuka maamuzi ya haraka..

Uwe na desturi ya kumshirikisha Roho mtakatifu ili upate shauri linalotoka kwa Mungu ...maana yeye ndiye mfariji, mshauri na nguvu yetu pia...

👉Ni lazima ujue Kuna wakati hutakiwi kuuchukua ushauri wa mtu yeyote bali ushauri wa Roho mtakatifu tu...maana yeye ndiye ajuaye zaidi...

Isaya 9:6
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, 
Tumepewa mtoto mwanamume; 
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; 
Naye ataitwa jina lake, 
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, 
Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Tumepewa mtoto mwanamume; 
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; 
Naye ataitwa jina lake, 
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, 
Baba wa milele, Mfalme wa amani.


Mungu akubariki sana 

Laddies in Christ 
Mwl /Ev Mathayo Sudai 
0744474230 /0628187291 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI