USIMRUHUSU SHETANI KUVUNJA NDOA YAKO
USIMRUHUSU SHETANI KUVUNJA NDOA YAKO Haleluya watu wa Mungu Leo naomba tutazame jambo la msingi ambalo linatokea kwenye dunia ya leo na watu bila kujua kuwa ni ajenda kabisa ya shetani akiwa na lengo maalumu. Kwanza ni lazima ujue kuwa swala la ndoa ni msingi ambao mwanaume na mwanamke wanatakiwa kujua kuwa ndiyo msingi wa kwanza wa kuamua jinsi ambavyo jamii, taifa na hata ulimwengu unatakiwa kuonekanaje Soma hapa Kumbukumbu la Torati 31:12-13 [12]Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii; [13]na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha BWANA, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki. Hapo Unaona wazazi wanapewa agizo la kuwapa watoto wao elimu ya kuwafanya waishi katika hiyo siku zote za maisha yao. Soma hapa tena Mithali 22:6 [6]Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata