JE WEWE NI UZAO WA IBRAHIMU ?

 JE WEWE NI UZAO WA IBRAHIMU ?

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu

Leo ni siku nyingine naomba tujifunze juu ya kuwa uzao wa ibrahimu kwa njia ya imani.

Unajua ni lazima ujue kuwa kabla ya Yesu wana wa ibrahimu walikuwa ni wale ambao wapo katika uzao wa isaka na baadae yakobo na esau.

👉Lakini sisi hatukuwa uzao wa ibrahimu na tulikuwa tukiishi bila kumjua Mungu tunayemwabudu.

👉Lakini tulikuja kufanyika kuwa taifa baada ya Yesu kufa msalabani ambapo alitufanya kuwa wake kwa kututoa katika miungu yetu na kutufanya tumwabudu Mungu ambaye huabudia katika Roho na kweli.

Soma hapa kuliona hilo

1 Petro 2:9-10

[9]Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

[10]ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Lakini ibrahimu ndiye aliyempendeza Mungu kwa ile imani ambayo alimwamnini Mungu na ndiyo maana hata kwa wale walio uzao wa ibrahimu hawawezi kumpendeza Mungu bila imani.

Waebrania 11:6

[6]Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Kwa lugha nyingine ni kwamba ili tumpendeze Mungu ni lazima tuwe uzao wa ibrahimu.

Maana yake tuwe na imani kama alivyokuwa baba yetu wa imani.

Wazao wa ibarihimu wapo katika makundi mawili

1: Wazao wa kimwili ( Yakobo na Esau )

2: Wazao wa kiroho kwa njia ya imani

Sasa wale wa kiroho ndiyo wale ambao si waisraeli wa kuzaliwa bali ni kwa imani.

Soma hapa 👇

Wagalatia 3:7

[7]Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.

Sasa kumbe tunapokuwa unaishi kwa imani mbele za Mungu basi tunakuwa uzao wa ibrahimu na kwasababu hii Yesu aliangikwa msalabani ili sisi tuipokee hii njia ya wokovu ndipo baraka zitujilie.

Wagalatia 3:7,13-14

[7]Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.

[13]Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

[14]ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

Kumbe baraka za Mungu alizomuahidi ibrahimu zitatuhusu sisi kama tutampendeza Mungu kwa kuwa na imani kwake.

Je hizi baraka za ibrahimu ni zipi????

Soma hapa upate jibu👇

Mwanzo 12:2-3

[2]nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

[3]nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

Maneno hayo yote ya Mungu yanamuhusu kila mtu anayemwamini Mungu na kutoka katika desturi ya ulimwengu na kulifuata neno la Mungu.

👉Unapoomba Mungu akubariki hakikisha wewe ni uzao wa ibrahimu 

👉Unapohitaji Mungu akutukuze na kukuweka juu hakikisha kwanza wewe ni uzao wa ibrahimu

👉Unapohitaji adui shetani asikupige basi hakikisha unakuwa uzao wa ibrahimu

Yaani mwamini Mungu katika Kristo Yesu

Unapohitaji mkono wa Mungu, kwenye baraka zake na huku hutaki kumwamini na kulifuata neno lake basi jua huwezi kuwa ndani yake na yeye hawezi kuwa ndani yako na hivyo adui atakutesa na kukutumikisha katika kazi zake.

👉Lakini ukimwamini Mungu kweli kweli basi Mungu Atakulinda katika njia zako zote na hiyo ndiyo ahadi yake kwako ukishika kutenda maagizo yake. (Kumb 28:1-..)

Yeye Atakulinda kupitia imani yako kwake.

1 Petro 1:5

[5]Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.

MWAMINI YESU LEO na KAMA UMEMWAMINI BASI KUWA MWAMINIFU KWAKE.

Mungu akubariki sana 


Taifa Teule Ministry 

Mwl /Ev Mathayo Sudai 

0744474230 /0628187291 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI