BINTI JIFUNZE KUOMBEA UZAO WAKO
Bwana Yesu asifiwe mabinti wa kristo
Leo naomba kuwajulisha siri ambayo ipo kwa wanawake wengi, ambao mara nyingi wao wenyeye huwa hawajui jambo hilo.
Unaposoma Biblia Unakutana na wanawake kadhaa ambao Mungu alitumia matumbo/ vizazi vyao kwa ajili ya kubadilisha au kutengeneza historia fulani.
Jambo la msingi ni kwa habari ya uzao wako.
Je Ulishawahi kujiuliza kama binti kuwa je! Uzao wako utakuwa ni uzao wa namna gani.?
👉Hili swali ni la msingi na unatakiwa kulifanyia kazi kwasababu shetani huwa anaandaa ajenda kwa mtu na kuharibu hatima ya mtu na kizazi chake.
👉Lakini pia Mungu huwa anaujali sana uzao wa mwanamke kwasababu hata watumishi wake anategemea awapate kutoka kwenye uzao wa mwanamke.
👉Ni lazima ujue na kutambua kuwa tumbo lako halitakiwi kuja kutoa kidhaifu/ au usije ukafanyika sababu ya kizazi kuharibika kwasababu ya kile utakachokitoa kwenye uzao wako.
👉Ni lazima ujue kuwa unatakiwa uanze kumuomba Mungu ili kwamba uwe na uzao wa kipekee.
👉 Ni lazima ujue kuwa hali yako ya kimaisha, utajiri au pengine shida na umaskini..hivi vyote havitoi tafsiri ya uzao ulionao..
Soma hapa👇
1 1 Samweli 1:12-15
[12]Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za BWANA, Eli akamwangalia kinywa chake.
[13]Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
[14]Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako.
[15]Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA.
Ukisoma hapo utaona habari za mwanamke mmoja ambaye aliitwa HANA, ambaye alikuwa na haja ya kupata mtoto kwa juhudi kubwa sana kwasababu tumbo lake lilikuwa limefungwa
👉Alikuwa na juhudi kumuomba Mungu ampe mtoto ambaye pengine atakuwa suruhu na furaha kwake kwa yale maisha na aibu aliyokuwa nayo....hivyo aliomboleza sana.
👉Lakini jambo la msingi ambalo hana alilitambua na kukiona kwa habari ya huyo mtoto anayemwomba ni kwamba...si tu kupata kizazi au mtoto wake, lakini je huyo mtoto atasimama upande upi???
Turudi nyuma kidogo tuone alichokisema
Soma hapa👇
1 Samweli 1:10-11
[10]Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana.[
11]Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.
Unaona hapo...alipoomba maombi ya kuweka nadhiri👇
👉Hakusema ukinibariki nitakushukuru kwa kukutolea sadaka tu
👉Hakusema ukinibariki Nitakuwa mwaminifu kwako tu
👉Hakusema ukinibariki Nitakuwa na furaha tu
Bali jicho lake lilienda mbali kabisa..kwenye kulinda kizazi au uzao wake ambao utapatikana kwa baraka za Mungu
Akasema hivi👉 "ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake,......."
Maana yake ni kwamba mtoto anapokuja si tu kwamba analeta furaha lakini pia anakuwa kwenye mikono salama.
Kwanini lazima mwanamke ujue kuomba hivi?
Kwasababu👇
👉Shetani atalenga Kuangamiza uzao wako👇
Ufunuo wa Yohana 12:1-4
[1]Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
[2]Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
[3]Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
[4]Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
👉Shetani atahitaji kumtumia mtoto au uzao wako kwaajili ya ajenda zake. Na ndiyo maana
👉Wachawi wote ni uzao wa watu fulani
👉Wale wote ni uzao wa wanawake fulani
👉Kila aina ya ubaya unafanywa na watoto wa wanawake fulani
Je mtoto wako unataka aje afanye nini??
Hivyo ni lazima ujue kuwa uzao wako lazima uanze kuulinda hata kabla haujafika ili utakapofika basi uwe mikononi salama, kama hana alivyofanya.
👉Usiombe kuzaa na kufurahia uzao kama hujaweza mipaka na misingi ya uzao wako katika ulimwengu wa roho kwasababu, usije ukadhani utapata furaha kumbe ukafedheheshwa.
Lakini kwaanzia leo anza maombi ya kile kizazi ambacho Bwana amekupangia
👉Anza kutengeneza misingi ya kizazi chako
👉Kama kuna maroho yanayosumbua ukoo wenu, basi anza kuyashinda ili yasipenye kwenye uzao wako kwa jina la Yesu
👉Kama kuna kitu kilikupata wewe kikakusumbua basi anza kukizuia kwa watoto wako.
👉TABIA MBAYA za kifamilia zinaweza kusafiri hadi kwa watoto wako hivyo haribu MFUMO wa shetani kabla ya uzao wako kufika.
Biblia inasema itengenezeni njia yanyosheni mapito yake.
Hata Yesu kabla hajaja, ilibidi atumwe Yohana kwaajili ya kutengeneza njia, kuondoa aina fulani ya ugumu mioyoni mwa watu, kuvunja baadhi ya udhaifu ili ajapo aliye mkuu ulimwengu ustahimili ujio wake. Haleluyaa đź‘‹đź‘‹đź‘‹
Fanya kazi, kwa imani, ondoa vizuizi, KATAA roho chafu, maagano yote na kila laana zisiingie kwenye uzao wako.
KWA JINA LA YESU.
Tumbo lako ni la msingi sana mwanamke maana hapo ndipo watumishi wa Bwana wanapatikana.
FUNGUA macho yako,,,amka usingizini.
Mungu ukubariki sana
Mwl/ Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni