LIFANYE JICHO LA MUNGU LIWE KIPIMO


 LIFANYE JICHO LA MUNGU LIWE KIPIMO

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu

Leo naomba kuwajulisha neno au ujumbe mfupi ambao naamini unaweza kukuvusha kwenye maisha yako, ni hivi👇

SI KILA CHEMA NI SAHIHI MBELE ZA MUNGU.

Haleluyaaaa

Kuna mambo mengi ambayo huwa yanafanywa na watu kwenye maisha na mwisho wake ni hasara, kwasababu wengi hawajui kuwa jambo linaweza kuwa zuri kwa macho yako lakini kumbe halimpendezi Mungu.

Uliona hilo Biblia imekiri hivi👇

1 Wakorintho 10:23

[23]Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.

👉Hii ikusaidie kutambua kuwa kuna mambo mengine ni mema kabisa kwenye maisha yetu lakini utakuta hayampendezi Mungu.

👉Mungu anachokiangalia mbele za mtu si kutenda jambo fulani jema lakini wema wa jambo hilo ni lazima uanzie machoni pa Mungu mwenyewe. 

.Hebu soma hapa👇

Mathayo 4:3-11

[3]Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.

[4]Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

[5]Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,

[6]akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, 

Atakuagizia malaika zake; 

Na mikononi mwao watakuchukua; 

Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

[7]Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

[8]Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,

[9]akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

[10]Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

[11]Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.


Sasa katika vifungu hivyo juu, tunaona mambo matatu ambayo shetani alimtaka Yesu ayafanye ambayo ni haya hapa👇

👉Kugeuza mawe kuwa mkate kwa ajili ya chakula

👉Kuonyesha/ kuuonyesha ulinzi wa Mungu unaomlinda

👉Kuchukua mali na utajiri wa dunia bila kutumia nguvu nyingi.

Haya ndiyo mambo ambayo Shetani alimtaka Yesu ayafanye.

Na ukiangalia vizuri hayo mambo kwa karibu na kwa mwili utagundua kuwa hayakuwa mabaya.

Kugeuza mawe kungemfanya Yesu kupata chakula

Kujitupa kumhakikishia Shetani ulinzi wake

Kumsujudia kungempa milki ya dunia yote.

Lakini Yesu alikataa kuyatenda kwasababu pengine yalionekana yana faida lakini hayakumpendeza Mungu.

Uzuri wa jambo unavyoliona wewe haina maana kuwa Mungu naye anaweza kuliona hivyo. Sasa ili tushinde katika hili ni lazima tuwe na uwezo wa kusema kama alivyosema Yesu mahali fulani alipokuwa akiomba 

Alisema hivi👇

Mathayo 26:42

[42]Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.

MAPENZI YAKO YATIMIZWE.

Je uzuri wa jambo unalolifanya upo katika mapenzi ya Mungu au unadhani kukupendeza wewe inatosha???

👉Tujifunze kuyatazama mambo kwa jicho la Mungu ndipo tuyafanye haijalishi yanaonekana mazuri kiasi gani, kwasababu wewe unaweza yaona ni mazuri lakini kumbe machoni PA Bwana ni kosa,

👉Kufanikiwa katika jambo na maamuzi unayoyafanya, hakikisha kwanza maamuzi yako unayapima kwa jicho la Mungu.,,kwamba je hili ninalolifanya au ninalotaka kulifanya ,..mbele za Mungu linaonekanaje? ??

Kwasababu 👇

Mithali 14:12

[12]Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, 

Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Lakini ukilifanya jicho la Mungu kuwa kipimo cha kila unachokifanya basi hutatenda kinyume na mapenzi ya Mungu hata siku moja.

👉Hata kama jambo linafaida kiasi gani lakini Kama halimpendezi Mungu, au kwa jicho la Mungu ni dhambi basi usilifanye bila kujali utaonekana mjinga kwa watu kiasi gani 😔😔

Ni heri kuwa mjinga kwa dhambi ila uwe mwelevu kwa hekima ya Mungu .

Mungu akubariki sana 


Taifa Teule Ministry 

Mwl / Ev Mathayo Sudai 

0744474230 /0628187291 


Maoni

  1. Chesco ndelema5 Oktoba 2023, 09:57

    Ubarikiwe Sana mtumishi
    Nimejufunza kitu hapa.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI