USIMRUHUSU SHETANI KUVUNJA NDOA YAKO

  USIMRUHUSU SHETANI KUVUNJA NDOA YAKO

Haleluya watu wa Mungu

Leo naomba tutazame jambo la msingi ambalo linatokea kwenye dunia ya leo na watu bila kujua kuwa ni ajenda kabisa ya shetani akiwa na lengo maalumu.

Kwanza ni lazima ujue kuwa swala la ndoa ni msingi ambao mwanaume na mwanamke wanatakiwa kujua kuwa ndiyo msingi wa kwanza wa kuamua jinsi ambavyo jamii, taifa na hata ulimwengu unatakiwa kuonekanaje

Soma hapa

Kumbukumbu la Torati 31:12-13

[12]Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii;

[13]na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha BWANA, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.

Hapo Unaona wazazi wanapewa agizo la kuwapa watoto wao elimu ya kuwafanya waishi katika hiyo siku zote za maisha yao.

Soma hapa tena

Mithali 22:6

[6]Mlee mtoto katika njia impasayo, 

Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Unaona kumbe watoto wakilelewa katika misingi imara basi wanakuwa nayo mpaka uzeeni

👉Lakini kumbuka hawawezi kufika uzeeni kabla ya utoto, na ujana.

👉Sasa kwasababu anamisingi imara maana yake kumbe katika ujana atakuwa akiishi katika namna hiyo.

👉Hata wewe ni lazima ujue hivyo ulivyo ni matokeo ya misingi uliyojengewa.

Mungu katika taifa la Israeli aliweka makundi kadhaa kwaajili ya kutoa elimu kwenye jamii kama vile manabii, makuhani, waandishi na familia.

Sasa hapa ninachosema ni kuhusu familia.

FAMILIA nyingi leo hii zinavunjika bila hata watu kujua kuwa kuna jambo ambalo shetani analifanyia na madhara yake si ya familia tu bali ni upana kwa kiulimwengu.

Siri ni hii👇

Shetani anavyokuwa na ajenda ya kuangamiza ulimwengu na kuharibu kizazi huwa anaanza na nafasi ya familia ili kuharibu msingi kwasababu anajua kuwa misingi ikiharibika basi kinachofuata ni uharibifu.

Zaburi 11:3

[3]Kama misingi ikiharibika, 

Mwenye haki atafanya nini?

Sasa ili kuharibu msingi huu lazima aanze na kuvunja ndoa za watu.

👉Roho za giza zinatumwa ulimwenguni kote kwa lengo la kufarakanisha na kuvunja ndoa za watu, jambo linalopelekea watoto wengi kuishi maisha ya taabu, kukosa misingi imara, wengine wanakuwa na makundi ya uovu na hata madawa ya kulevya.

👉Jambo kama hilo maana yake ameshaharibu misingi ya ulimwengu mzima bila watu kujua kuwa kuna hatari katika hilo.

Ili kujua kuwa shetani amevamia ndoa yako basi kuna mambo yataanza kutokea

👉Utaanza kukosa hamu na mke/ mume wako

👉Utashangaa unaanza kumchukia tu mume/ mke wako

👉Utashangaa unaanza kuhitaji kuwa na wanawake wengi

👉Utaanza kuona kila anachokifanya mwenzako unakiona hakikupendezi

👉Utaanza kutoka nje ya ndoa

👉Utaanza kujiingiza kwenye vitu na makundi yasiyo na maana

👉Upendo kwa mke/mume unaanza kupoa

👉Kama kuna mambo ambayo mlikuwa mnafanya pamoja basi utashangaa hutaki tena bila sababu

👉Mlikuwa mnafanya ibada kila siku usiku na familia ghafla utaona mambo hayo yanaanza kufaa. Maana yake shetani amawaibia tabia ya maombi kwanza ili awavamie kirahisi

Jambo la msingi ni kwamba ukiona mambo hayo yanakupata basi jua shetani amekutembelea na kunakitu ambacho ndiyo maana umebadilika.

👉Ni lazima ujue kubadilika kivyovyote ni kwasababu ya msukumo unaoupata na ushawishi kutoka kwa roho fulani ( ya giza au nuru) kulingana na umebadilikaje

👉Kwani si ndiyo wewe mwanaume ambaye ulikuwa unampenda sana mke wako je ule upendo Umeendaje wapi

👉Si ndiyo wewe mwanamke uliyekuwa huwezi kulala bila kumuombea mume wako vipi imekuwaje leo hufanyi hivyo

👉Si ndiyo ninyi wanandoa ambao mlikuwa mnaishi pamoja kwa amani lakini leo kila mtu ana chumba chake cha kulala je imekuwaje??

👉Ile hamu kwa mume wako au mke wako uliyokuwa nayo MWANZA umeipeleka wapi

Usitumie nguvu kubwa kujiuliza...jibu ni kwamba KUNA KITU KINAFANYA KAZI NDANI YAKO. na lengo lake ni Pana sana kwahiyo in lazima uzuie ile nguvu inayokutaka kuvunja ndoa.

Kwasababu jambo hilo hata Mungu halimpendezi

Malaki 2:16

[16]Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.


👉Usiruhusu ndoa yako kuvunjika

👉Usikubali kumchoka na kumchukia mwenza wako maana yamebeba Siri kubwa sana kwako na kwa kizazi chako

👉Usikubali kuona mtu ukiyekuwa unapenda hadi kufunga naye ndoa akiharibikiwa au kuumia kwa kupata mzigo wa malezi ya watoto wenu.

👉Usiruhusu mtu wa nje kuivuruga ndoa yako maana ndio msingi mkuu wa jamii inavyotakiwa kuwa.

👉Ndoa ilifungwa na Mungu, Usiruhusu ikavunjwa na mtu ambaye hakuijenga.

👉Mungu hapendi kwasababu yeye ndiye huwa anawaunganisha watu lakini cha ajabu mvunjaji ni mwingine

👉Endelea kuzidisha upendo kwa mwenza wako ili kumkosesha shetani nafasi

👉Usiruhusu shetani akakubadilisha mawazo na kumuona mwenzako hana maana tena.

Mungu aikinde nyumba yako kwa jina la Yesu


Ubarikiwe sana


Taifa Teule Ministry

Mwl / Ev Mathayo Sudai

0744474230 /0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI