MADHARA YA KUNUNG'UNIKA


 MADHARA YA KUNUNG'UNIKA

TUANZE HIVI👇

👉Kunung’unika ni hali ya kuwa mtu wa kusema sema pembeni kwa watu wasiohusika pale unapoona jambo usilo furahishwa au kubaliana nalo.

👉 Kunung’unika kunaweza kutokana na jambo dogo kama kumaliziwa chakula fulani au jambo kubwa kama uongozi wa mchungaji wako. Kunung’unika mara zote huambatana na kulalamika.

Hebu soma hapa👇

Yuda 1:16

[16]Watu hawa ni wenye kunung’unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.

Unaona hapo kumbe..wenye kunung'unika wapo hivi👇

👉Huwa wakala imani sana 

👉Mara nyingi huenda mawazo yao au njia ndizo zafatwe, na ikishindikana tu basi hawafurahishwi

👉Huwa mara nyingi sana Kiburi na hawapendi kurekebishwa

👉Hupenda mema tu lakini yakija mabaya wanachukia na kutokuwa na imani tena

đź‘Źđź‘ŹNa ndiyo maana Kunung’unika kuliwafanya wana wa Israeli kushindwa kufika katika nchi ya ahadi.

Katika kitabu cha hesabu tunaona jinsi ambavyo walilalamika baada ya wale wapelelezi kuleta habari za nchi ya ahadi. Hesabu 13:31-33, 14:1-4. Katika habari hii tunajifunza mambo yafuatayo:

👉Unaponung’unika unapuuza uwezo wa Mungu

Wana wa Israeli walisahau na kupuuza uwezo wa Mungu aliyewatoa Misri utumwani na kuwavusha katika bahari ya Shamu na kuwapigania katika safari yao na kuona kuwa lililo mbele yao haliwezi na kuishia kunung’unika na kulalamika.

👉 Kungu’unika huchochewa na taarifa isiyo sahihi

Uchochezi, uongo, majungu n.k huchochea kunung’unika kutokana na kuwa huleta habari ambazo sio sahihi zenye lengo la kuharibu na kuangamiza. Kuna watu wanapenda kusikia habari mbaya za watu wengine au jambo Fulani ili wapate kitu cha kulalamika na kulaumu.

👉 Mtu anayelalamika ni rahisi kufikia maamuzi ambayo si sahihi

Wana wa Israeli walimlaumu Mungu kwa hali waliyoisikia kuhusu nchi ya kanaani na hata kufikia hatua ya kupanga kurudi Misri.

👉 Katika hali ya kulalamika, ni rahisi kufanya mambo mabaya bila kufikiria.

Wana wa Israeli katika kulalamika na kunung’unika kwao walitaka kuwapiga mawe wale walioleta taarifa nzuri kuhusu kanaan. 14:10. Kunung’unika kunakufanya ushindwe kufikiri kwa makini na kuona uhalisia wa jambo husika.

👉 Kunung’unika huzidi katika mazingira ya hofu

Hofu ya wana wa Israeli iliwapelekea kunung’unika, japo Joshua na caleb waliwatoa hofu kwamba wasiogope wao bado walijawa na haofu hali iliyowapelekea kuzidi kunung;unika hasa kwa kutokujua nini kitatokea baada ya kusahau kabisa ukuu wa Mungu.

👉 Kunung’unika kukiachwa kuendelea hupelekea uasi

Wana wa Israeli walikuwa tayari kuchagua viongozi wengine na kuasi mbele za Mungu na kurudi Misri. Hii ilitokana na kunungu’unika kwao hadi wakaona kuwa wao ndio wanaojua zaidi ya Mungu.

👉Mwisho wa kunung’unika ni kuwa mtu asiyeridhishwa na chochote

Unapoendelea kunung’unika unazidi kuona kila kitu ni kibaya na hakifai. Wana wa Israeli walipewa kila kitu na Mungu na bado hawakuridhika kwa sababu ya tabia ya kunung’unika.

Sababu ya kunung’unika kwao hawakuona upendo wa Mungu, wala ukuu wake wala uzuri wa nchi ya ahadi wao waliona mabaya tu.

Kunung’unika ni jambo linalotutoa kwenye uwepo wa Mungu. Mtu anayenung’unika hana imani kwa Mungu na nguvu yake. Ni hali ya kutokuamii kuwa Mungu anaweza akatumia mambo magumu uanayotokea katika maisha yetu kwa ajili ya kutupatia mema aliyoyakusudia.

NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA MANUNG’UNIKO ?

1.Kuomba

Kwa maombi tunayapeleka matatizo yetu kwa Mungu, na kumsubiri aweze kutuongoza katika njia SAHIHI. lakini pia katika kuomba tunapokea amani ya ajabu iliyoambatana na imani

2. Malalamiko yako yapeleke kwa wahusika

Unapozungumza tatizo Fulani na mtu asiyehusika unakuwa unachangia manung’uniko na kulizidisha tatizo hilo. Jambo la msingi hapo ni kwamba ongea na wahusika kwa utaratibu na busara, uwe tayari kusikia maoni yake na ufafanuzi na pia uwe tayari kubadili msimamo wako pale utakapopata taarifa sahihi.

3. Waeleze wengine wanaonung’unika nini cha kufanya

Usipende kuwa sehemu ya manung’uniko ya watu wengine wala kuwachochea kuendelea kulalamika. Waonyeshe nani wamwendee ili kupata majibu ya maswali yao, ili watoke katika kifungo hicho.


Mungu akubariki sana 


Taifa Teule Ministry 

Mwl / Ev Mathayo Sudai 

0744474230 /0628187291 



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI