JIHADHARI NA UJIO WA SHETANI KWAKO.

 JIHADHARI NA UJIO WA SHETANI KWAKO.

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu

Leo naomba tupate ujumbe mfupi ambao unabeba nia ya ndani aliyonayo shetani kwaajili ya watu wa Mungu.

Ni lazima ujue kuwa kuna ajenda nyingi sana ambayo anazileta kwa watu akiwa na lengo la👇

👉Kujiinua na kuabudiwa yeye badala ya Mungu

👉Kuwasukumia watu jehanamu moja kwa moja.

Lakini kwa malengo yake hayo huwa anakujaje kwa mtu.

Soma hapa 👇

Mwanzo 3:1-2

[1]Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, 

"Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? "

[2]Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;

👉Kabla hatujachunguza hapo Soma hapa kwanza👇

Mathayo 4:1-4

Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.

[2]Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.

[3]Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.

[4]Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Sasa hivi vifungu viwili vinabeba maneno ya mwanzo kwenye agano la kale na agano jipya

MANENO YA KWANZA YA SHETANI KWENYE AGANO LA KALE👇

"Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? "

MANENO YA KWANZA YA SHETANI KWENYE AGANO JIPYA👇

Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.

Shetani alimuuliza mwanadamu wa kwanza kwa namna ile akiwa na lengo la kumtoa kwenye uwepo wa Mungu. Akawahakikishia kuwa Mungu ni mwongo na hataki wawe na ufahari na ndiyo maana amewanyima wasile tunda.

👉Bila kujua hawa naye akamuunga mkono shetani huku akihitaji kula tunda akijua kuwa atakuwa kama Mungu.

Lakini ukiyasoma maneno ya shetani kwenye agano jipya utagundua kwamba shetani alimwambia Yesu kwa namna ile kwasababu.

👉Alijua kwamba Yesu amekuja kurejesha kile alichokipoteza mtu wa kwanza

👉Alijua kabisa kwamba Yesu alikuwa mbinguni na kila kitu anakijua hivyo hawezi kukubali kama akitumia uongo alioutumia kwa hawa na Adamu.

👉Alijua kabisa Kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Na ndiyo maana akamwambia ,,,IKIWA WEWE NI MWANA WA MUNGU.....kuonyesha kuwa alikuwa anajua kuwa Yesu ni nani.

Lakini katika sehemu zote mbili unagundua kuwa shetani alikuwa na lengo la kuwaangusha WAHUSIKA .

👉Na wewe mtu wa Mungu ni lazima ujue shetani anapokuja kwako hana lengo lingine mbali na hilo. Yaani kukuangusha wewe na yeye mwenyewe kujitukuza .

Hili linakuja kuwekwa wazi na Yesu mwenyewe kwenye mistari hii.

Yohana 10:10

[10]Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

👉Kwenye kipengele cha kwanza Yesu anatoa Siri ya shetani anapokuja kwenye maisha yako kwa njia yoyote ni kwamba kwa ujumla KUKUANGUSHA.

Shetani anaweza kuja kwako kwa njia nyingi kama vili

👉Tamaa ya fedha

👉Mahusiano mabaya

👉Umaarufu na sifa fulani

N.k

Lakini katika yote ni lazima ujue kuwa analenga KUKUANGUSHA.

Kwasababu kwa agano la kale nia yake ya kwanza ilikuwa ni hivyo na kwa agana jipya nia yake ni hiyo hiyo.

Je wewe ni nani mpaka aje kwako kwa nia nyingine.???

Lakini kwa sehemu ya pili Yesu anatupa Siri tuliyonayo watu tuliookoka yaani tulio ndani ya Kristo Yesu.

Anasema hivi👉 "mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele."

Yesu anaweza kutuma uzima tele kwasababu alipofatwa na shetani ili aanguke,,,HAKUANGUKA.

Na wewe mtu wa Mungu pengine wewe ni msaada wa familia yako, au kizazi chako basi ni lazima ujue kuwa akikuangusha,,,basi huwezi kuwa msaada kwa hao.

Leo jua nia ya shetani kisha MPINGE kwa JINA LA YESU.


MUNGU AKUBARIKI


Taifa Teule Ministry

Mwl /Ev Mathayo Sudai

0744474230 /0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI