RAFIKI YAKO NI NANI ???


 RAFIKI YAKO NI NANI ???

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu

Leo naomba tuichunguze hekima juu ya rafiki zetu ambao tunao.

Baada ya hapo naomba chukua hatua.

Hebu soma hapa👇


Mithali 18:24

[24]Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; 

Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Hapo Biblia inasema mtu akiwa na rafiki wengi, maana yake amerengeneza nafasi kubwa ya yeye kuumia, kupotea au kuangamia

Na hii ni kwasababu, uadui na ubaya alionao mtu kwake huwa ipo ndani ya mtu na hivyo kwasababu umejitengenezea rafiki wengi itakuwa ni vigumu kujua kila mtu kati ya hao wanakuwazia nini, au wanakufanyia nini.

Na hii ni kwasababu, wengi katika maisha ya kawaida, huumizwa na wale ambao waliwaona kuwa ni marafiki zao.

👉Ni lazima uwe makini na wale wanaoknekana kuwa marafiki kwako.

👉Rafiki zako ndiyo wanaweza kufanyika njia na sababu ya wewe kuangamia.

Na ndiyo maana ukisoma Biblia utagundua kwamba mafarisayo, waandishi na makuhani ndiyo waliokuwa wanapanga kumuua Yesu, lakini aliyekamilisha na kutengeneza kifo chake alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana Yuda.

Soma hapa👇

Mathayo 26:45-46

[45]Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.

[46]Ondokeni, twende zetuni! Tazama, yule anayenisaliti amekaribia.

Unaona hapo Yesu anawaambia wanafunzi kwamba YULE ANAYENISALITI, Amekaribia.

Biblia inasema kwamba maadui wa Yesu walikuwa wakitafuta njia yakumkamata Yesu na kumwua lakini waliikosa

Lakini Yuda alipomsaliti ti, ndipo jambo likakamilika maana yake aliyefanikisha jambo hilo ni Yuda mtu wa karibu na Yesu.

😔Na ndiyo maana hata Yesu hakusema ole wake wanaomuua bali alisema ole wake atakayemsaliti.

👉Maana yake ni heri mtu anaekuua moja kwa moja kuliko rafiki yako anayekusaliti ili ufe.👇

 Mathayo 26:24,

[24]Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.


Sasa katika hili natamani tujifunze kuwa

👉Tunapohitaji marafiki basi tusiwe na marafiki wengi maana wingi wa marafiki unaongeza nafasi ya uharibifu

👉Tuwe makini na yule rafiki uliyenaye maana anaweza kuwa sababu ya wewe kuumia.


Tena ni lazima ujue kuwa wengi huwa hawaumizwi na maadui zao Bali marafiki ndiyo husababisha maadui Kukuangamiza.

👉Pengine ni kazini kwako basi kuwa makini na marafiki

👉Pengine ni kwenye biashara, kuwa makini na marafiki

Popote ulipo na unapofanyia kazi basi kuwa makini na marafiki.


Pia Biblia inasema " yupo rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu"


Hapa panatoa faida ya kuwa na rafiki mwema.

Hivyo ukifanikiwa kuwa na rafiki anayejua thamani yako, basi unakuwa umepata mtu ambaye anaweza kuambatana katika hali zote za maisha tena zaidi ya ndugu zako wengine.


👉Kuna ndugu wanaweza wasiwe na mawazo mema kwako lakini rafiki mwema anaweza

👉Kuna wakati ndugu zako wanaweza kukukataa kwa sababu fulani lakini rafiki mwema anaweza kukuunga mkono.


Hapa pakusaidie kumuheshimu rafiki mwema uliyenaye.

Ukiwa na rafiki ambaye anaambatana na wewe popote pale

👉Unapokuwa na njaa yupo tayari kukulisha

👉Unapokuwa na shida analia pamoja na wewe

👉Uchumi wako unaposhuka yeye anakuwa pamoja na wewe .


Mtu wa namna hii jua kabisa kuwa jlni rafiki mwema na Inapaswa kumuheshimu sana.


Rafiki mbaya ni yule ambaye

👉Ukiwa kwenye shida yeye anafurahi

👉Ukifirisika anashangilia

👉Ukiwa na udhaifu fulani anakutangaza kwa watu


Basi ukiwa na mtu kama huyo kuwa makini na fanya uchaguzi sahihi kabla ya kufanya kama alichikifanya Yuda.


Tambua kuwa, kuongezeka popote panategemea RAFOKI YAKO NI NANI😔


NI HERI UWE NA RAFIKI MMOJA ANAYEKUPENDA, KUHESHIMU NA KUKUJALI kuliko wengi ambao wanakuwazia uharibifu na wanafurahi unapokuwa una matatizo.

Na ni lazima ujue kuwa unapokuwa na marafiki wengi basi ni ngumu sana kuwajua wote.

👉Jambo la msingi unalotakiwa kulijua ni kwamba uharibifu huwa unasababishwa na kukamilishwa na rafiki siyo adui.


Ni hivi👇

👉Aliyemsaliti Yesu ni rafiki siyo adui

👉Waliomuuza yusufu utumwani ni rafiki( ndugu) sio adui

👉Aliyemuua hanili ni rafiki( kaka) siyo mtu wa mbali

👉Waliomuua Stefano ni wayahudi wenzake sio watu wa mbali

👉Samsoni alisalitiwa na mchumba wake (Delilah ) sio mtu wa mbali

🤔Ukiona mtu hana faida kwako, usijaribu kumfanya kuwa rafiki yako, bali awe mtu wa kawaida kwako hata kama kuna mambo ambayo mnayafanya kwa pamoja.

👉Kuishi nyumba moja ya kupanga na mtu haina maana anatakiwa kuwa rafiki

👉Kusoma na mtu darasa moja haina maana anatakiwa kuwa rafiki yako

👉Kufanya kazi moja na mtu haina maana anapaswa kuwa rafiki

👉Kusali na mtu kanisa moja haina maana anapaswa kuwa rafiki

🤔Usiwe mwepesi kumfanya mtu kuwa rafiki yako ukifikiri anafanana na wewe.


Kwasababu kama mtu umemfanya kuwa rafiki wa karibu na kumbe hana madhara chanya, vipi kuhusu madhara hasi ??


Kuwa makini🤔🤔🤔


Mungu akubariki sana


Taifa Teule Ministry

Mwl / Ev Mathayo Sudai

0744474230 /0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI