WOKOVU TULIOPATA NI KWA NEEMA TU.
WOKOVU TULIOPATA NI KWA NEEMA TU. *Waefeso 2:4-7* [4]Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; [5]hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. [6]Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; [7]ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Sisi tu kazi ya mikono yake Mungu, tuliumbwa ili tuyatende matendo mema, tangu awali Mungu aliyatengeneza ili iwe mwongozo wa maisha ya mwanadamu daima. Lakini baada ya mwanadamu huyo kufanya dhambi akaenda kinyume na yale aliyowekewa ili aenende nayo, Shetani akatuchukua mateka kutoka kwenye miliki ya Mungu ( pale Edeni), akatufanya kuwa watumwa wa dambi😭 mwanadamu akamchukiza Mungu. Sifa ya Mungu ni Mwenye upendo kwaa mwanadamu. Ni Mwenye huruma nyingi. Ni Mungu asiyependa mwanadamu aliyemuumb