KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA


           KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA*

*Mithali 1:7*

[7]Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Kumcha Mungu ni kuyatenda Mapenzi ya Mungu.

Kumcha Mungu Ni kuepukana na dhambi.

Ulisome Neno la Mungu na kuliishi.

Uwe na moyo wa kupenda ibada na si kulazimishwa. moyo wako uridhie kumpenda Mungu kwa dhati.

Ukimpenda Mungu utamfanyia ibada, kumfanyia Mungu ibada ni pamoja na kumtolea Mungu sadaka.

Uwe na maisha ya maombi itakusaidia sana katika kuutunza uwepo wa Mungu ndani yako.

Tena ukimpata Yesu umepata vyote, na ndiyo maana Daudi anasema Kumcha Bwana ndiyo chanzo Cha maarifa.

maarifa mazuri tunayapata kwa Mungu tu


unaweza kuwa uliokoka lakini huishi maisha ya Kumcha Mungu yaani kufanya ibada ya kweli na Mungu.

kutenga muda wa kuzungumza na Mungu kwa kufunga na kuomba.

Pia kwa kuikimbia dhambi ambayo ni asili ya mabaya na Laana zote tunamcha Mungu na ndiye atupaye maarifa ya kuikimbia dhambi.

Kwa kumpenda Mungu tunamfanya Mungu kukaa karibu na sisi, hujaona tangu ulipookoka umeongezeka namna ya ufahamu na uelewa katika Mambo fulani😁 huko ndiko kuongezeka maarifa / kupata maarifa.✍️

Mwanzo ulikuwa hupendi kusoma Neno Wala kutafakari hukuwahi kuweza  lakini ulivyoanza kumpenda Mungu sasa  amekupa maarifa ya rohoni na kuwahubiria wengine unaweza sasa

Ona unauwezo wa kutafsiri ndoto Kama Yusufu💃😁

kwa Yesu kuzuri mnoo🥰

Tafuta kumjua Mungu Sana ili uwe na maarifa mengi ya ki-Mungu.🙌

Hayo maarifa yatakusaidia hata namna ya kuenenda/ kuishi  katika nyakati hizi za mwisho. hautasombwasombwa na mafundisho ya watumishi wa Uongo kwa sababu maarifa ya Ki- Mungu unayo ndani yako  yanakusaidia kupambanua Mambo.

*Tuombe*

Mungu wetu na Baba Yetu wa Mbinguni umetamalaki juu ya miungu yote Dunia yote hakuna Kama wewe  Bwana, Asante Roho Mtakatifu kwa kutuamsha salama Ni kwa Neema yako tu Jehovah tumeiona siku mpya.

Ni asubuhi nyingine tena Mungu tunaomba Ulinzi wako kwa familia zetu, kwa kazi zetu na jaamii yetu,mkono wako Baba usipungue kwenye maisha Yetu bariki na kazi za mikono yetu maana wewe ndiwe utupaye faida sawasawa na 

*Isaya 48:17*

[17]BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

Tufunike kwa damu yako takatifu, Shetani asitupate kwa jina la Yesu.

Leo Ni siku ya Ibada tunaomba ututangulie Baba katika Nyumba zetu za ibada ukatupe ushirika wa pamoja nawe kwa utukufu wa jina la Yesu nimeomba na kuamini Amen🙏.

*Mungu akubariki Sana*


Taifa Teule Ministry

Mwl Beata Silwimba

0620507212 / 0742442164 

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI