USISHUPAZE SHINGO YAKO
USISHUPAZE SHINGO YAKO
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.
Leo ni siku nyingine njema kwako na kwangu pia kwa msaada wa Mungu.
Lakini leo naomba nikushirikishe jambo ambalo ni msingi wa wewe kuipinga njia ya upotevu.
Soma hapa👇
Mithali 29:1
[1]Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo,
Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.
Biblia inatoa jibu na msingi wa nini kinatokea kwa mtu anaposhindwa kuisikia sauti ya Mungu inapomwita.
👉kabla ya yote natamani kila mtu ajue kuwa Mungu huwa hana watu maalumu anao wahitaji isipokuwa anawataka wote ambao wataitii na kuifuata sauti yake.
pengine watu hujiuliza mbona hawatumiwi na Mungu?
Jibu ni kwamba hawajakaa katika njia ya kutumiwa.
Kwasababu Mungu huwa anataka kwanza, mtu amtii ndipo a mtume.
unapotii wito wa kuwa mtakatifu basi unakuwa umetimiza sifa za Mungu kukutumia kwa namna apendavyo yeye.
Lakini hapa nahitaji niseme na wewe kwa namna ya ugumu ulipo ndani ya mwanadamu pale anapoitwa na Mungu kupitia kupitia Yesu Kristo.
wito mkuu kuliko wito wote ni KUWA MTAKATIFU.
Kwasababu ndiyo wito unaomfanya mtu kwa na sura ya kufanana na Mungu na mfano wa Mungu.
Soma hapa👇
Mambo ya Walawi 20:7
[7]Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
1 Petro 1:16
[16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Usipokuwa na hii sifa basi huna sura ya Mungu, japo utasema umeumbwa kwa mfano na kwa sura ya Mungu lakini ndani yako sura ya Kristo haipo.
huu ni wito ambao unamfanya mtu kuzungumza na Mungu, kumuona Mungu, na kumshinda shetani
Soma hapa👇
Waebrania 12:14
[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Sasa ni lazima ujue kuwa haya ni maneno ya kweli na Amina kwa watu wote.
👉 Lakini katika Mithali anasema.. " Aonywaye mara nyingi na kushupaza shingo, Atavunjika ghafla Wala hatapata dawa.
Je hapa anasema kuhusu nini?
👉Ni Mala nyingi umeonywa na Sauti ya Mungu kuhusu kujitenga na dhambi.
👉Ni mara nyingi umeonywa na Mungu kuhusu kuyafanya mapenzi na maagizo ya Mungu.
👉Kuna wengine husemeshwa na Mungu kuhusu mwenendo wao lakini hawataki kusikia.
👉wengine wamehubiriwa na Mungu kupitia watumishi mbalimbali lakini wameona ngoja wale ujana wataokoka siku nyingine.
pasipo kujua kuwa pengine hata siku hiyo wanayoipanga wao kuja kumuheshimu na kumtii Kristo, pengine wanaweza wasiione.
Ni lazima tujue pale Roho mtakatifu anapotutaka na kutuita kutubu na kuwa watakatifu kupitia njia mbalimbali ni kwa kumtii.
👉Waliopo jehanamu saa hii ni watu wa kila namna, cha kutisha ni mpaka wadogo kabisa ambao ukijua unaweza ukashangaa, wapo wale ambao huku walionekana watumishi wa Mungu na kumbe walikuwa wanafanya upotoshaji wa neno kwa maslahi yao ambapo wrliijua kweli yote lakini waliiacha na kusababisha roho za wengi kupoteza mwelekeo.
wapo mabinti ambao wengi walibembelezwa sana na Mungu, akiwaambia wamtii yeye wajitenge na dunia lakini waliona kuwa watamtumikia Mungu kesho, Bahati Mbaya sana kesho hawakuiona.
Na unajua ni nini wanakifanya sasa ivi kule jehanamu?
Lakini kwanini hayo yote yanawapata,.... ni kwasababu walionywa mara nyingi lakini hawakutaka mwisho wa siku walikufa na moja kwa moja jehanamu.
👉pale walipo wanalia kilio cha ajabu ambapo ukipata neema ya kusikia sauti zao basi utaelewa kwamba ni sauti ambazo hukuwahi kuzisikia toka umezalia lakini kingine ni moto ambao unapanda kutoka chini yao mpaka juu huku, wakimuomba sana Yesu awape nafasi ya pili na kwamba watamtumikia na kumtii kwa gharama zote.
Je unajua jibu ambalo Yesu huwajibu.... Yesu Kwa huruma, uchungu na kwa upendo mkubwa huwaambia hivi👇
" ULIPOKUWA DUNIA NILIKUITA NA KUKUPENDA LAKINI HUKUTAKA KUNIELEWA NA KUNITUMIKIA, NILITUMA WATUMISHI WANGU WENGI KWAKO ILI UGEUKE LAKINI ULICHAGUA KUIPENDA DUNIA KULIKO MIMI SASA HUKUMU IMEKWISHA WEKWA TAYARI NA BABA YANGU."
Kisha baada ya maneno hayo unajua wao humjibu nini?
Wengine huendelea kulia kwa kujuta juto Kubwa, lakini wengine humlaani na kumtukana.
👉lakini hayo yote hayana msaada wowote kwao na hayana msaada maana walipokuwa hai walikuwa na nafasi kubwa lakini hawakutaka kusikia, waliendelea kushupaza shingo mwisho wa siku walivunjika na leo hii hawana dawa.
Na Mimi nakusihi wewe uliyepo ndani ya kundi hili kwamba, Jehanamu ipo na Yesu, hataki uende kule na ndiyo maana anakuonya muda wote kwamba usiende kule.
Jambo ambalo unatakiwa kulijua pia ni kwamba waliopo jehanamu muda huu wanakumbukumbu ya kila kitu ambacho walikuwa wanakifanya yaani mpaka kilichowapeleka jehanamu wanakijua na ndiyo maana wanajuta lakini pia hakuna hata mmoja asiyejua kwanini yupo pale na ndiyo maana Biblia inasema hakuna mtu atakayekuwa na udhuru mbele ya hukumu ya Mungu.
Soma hapa👇
Warumi 1:20
[20]Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;
Kwahiyo hata habari hii ambayo ninakupa kama mjumbe tu, ukishindwa kutii na ukaamua kumfuata shetani na njia zake basi jua, ukifa utafika na utajuta kwamba kwa nini sikutii kile nilichoambiwa.
Mungu akupe neema ya kujua kilichopo jehanamu.
Lakini leo nakusihi, usikukubali kuifuata dunia na tamaa zake maana zote zinalenga upotevu kwako.
👉leo hii unaweza kujiona kuwa una kila kitu na huna haja na Mungu lakini nikwambie kwamba hayo ni mawazo mabovu sana na ni mawazo ya shetani aliyejiinua kwako mpaka Unaona kazi zake ni bora kuliko Mungu.
Leo nakupa wito wa kugeuka na kuacha kuifuata dunia na tamaa zake bali mfuate Yesu yeye ndiye njia ya kukufikisha kwa Mungu.
Yohana 14:6
[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
USISHUPAZE SHINGO MAANA MBELE YAKO KUNA HATARI
Na habari hii ni kweli kabisa wala si ya kufikirika.
👉usikubali kuwa mmoja wa watakaojuta na kulia kilio cha ajabu sana.
Basi kama Unaona kwamba huna mahusiano mazuri na Mungu na kwamba umependa kazi za shetani na tamaa zake, basi tubu kwa imani kwa maombi haya na Mungu atakurehemu kabisa.
Hapo ulipo kama upo mazingira mabaya basi jitenge kidogo, tafakari habari za kifo chako, je itakuwaje, na ukifa unaelekea wapi,? dhamilia kuacha njia zako mbaya,
Kisha Sema sala hii kwa imani👇
BABA KATIKA JINA LA YESU, NIMEKUJA MBELE ZAKO, NIKIJUA KABISA KUWA NIMEKUTENDA DHAMBI KWA MAWAZO YANGU, MANENO YANGU PIA NA MATENDO YANGU. LAKINI LEO NAKUGEUKIA WEWE BWANA, NAHITAJI MSAADA WAKO NA NIOSHE KWA DAMU YAKO YESU. NIFANYE KUWA MMOJA WA WANA WAKO. NIAMINI KUWA WEWE NI MWANA WA MUNGU NA ULIKUFA MSALABANI KWA DHAMBI ZANGU. NA LEO NAOMBA HISRMEHE DHAMBI ZANGU KWA JINA LA YESU. ASANTE KWA SABABU REHEMA ZAKO NI NYINGI, ASANTE KWASABABU UMENISAMEHE DHAMBI ZANGU PIA BWANA NINAOMBA NGUVU YA KUSHINDA NJIA ZA SHETANI ILI NIKUPENDEZE WEWE TU MUNGU WANGU, NINAOMBA NIKIAMINI KUWA UMENIOSHA KWA DAMU YAKO YESU NA UMESIKIA MAOMBI YANGU KWA JINA LA YESU. AMINA.
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl / Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Ubarikiwe Sana kwa somo hili Hakika nimeona uwepo wa Mungu ndani ya somo hili, Mungu utusaidie kuyaishi maneno yako Amina
JibuFutaAMINA.
JibuFuta