BWANA TUONGEZEE IMANI
TAIFA TEULE MINISTRY MORNING GLORY
Day : Growing up Friday
Date: 28 April 2023
Na Beata Silwimba
Title : BWANA TUONGEZEE IMANI
Luka 17:5-6
[5]Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.[6]Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
Petro akasema Bwana tuongeee Imani.
Shalom👏
Unajua ni kwanini Hawa wanafunzi wa Yesu walimwambia Bwana tuongezee Imani???🤔
Yesu alikuwa na hawa wanafunzi (yaani Mitume) kwa muda mrefu Sana na walikuwa wameshajifunza Mambo mengi kuhusu Yesu, na tayari walikuwa wamewamini na kumjua Kwamba yeye ndiye Kristo.
Kwa mtazamo huo ni wazi Kwamba Kama ni Imani walikuwa nayo kwa sehemu.
Kama ni Mamlaka tayari walikuwa nayo ya kumkemea pepo n.k
Kama ni upako walikuwa nao hata wa kuwashuhudia wengine waweze kumwamini kristo Kama wao walivyo mwamini.
Lakini kwa kawaida tu nimewaza Sana kwa naamna walivyokuwa inawezekanaje wakasema Bwana tuongezee Imani??🤔
Halafu Jambo lenyewe Ni kumsamehe MTU Saba Mara sabini, Lakini zaidi ya kumsamehe mtu so Hilo tu, Bali yapo mengi tunakutana nayo majaribu, tunaomba baraka kubwa, tunakutana naa changamoto nyingi ambazo kwa Imani zetu tulizonazo sasa hatuwezi kushinda au kustahimili Vita ya Shetani.
Anhaaa nikajifunza kitu hapo ;✍️
Yapo Mambo unaweza ukakutana nayo yanayohitaji Imani kubwa Sana ili kushinda au kuyapokea.
Kumbe kuna wakati hatupaswi kuomba mambo fulani fulani tu kwa Mungu.
Mfano ;
Mungu naomba upako wa kutumika
Mungu naomba Mke mwema💃
Mungu naomba Mume Bora
Mungu naomba Mali na Utajiri
Mungu naomba afya njema, ulinzi wa Mungu🤔 hivyo pekeyake havitoshi ili kuweze kukua kiroho lazima ukutane na majaribu makubwa ambayo yatafanyika daraja la kukupeleka mahali fulani penye utukufu mkubwa😁
Yamkini umeomba Mambo fulani na hujampokea mpaka Sasa kwa sababu Imani ya kuyabeba majibu yako ni ndogo, hivyo Mungu anasubiria Imani yako Ikue ndipo akupe hitaji lako🤔🙆
Kumbe kwa Imani hiyo uliyonayo huwezi kuyashinda mambo fulani,
Huwezi kustahimili situation fulani kwenye maisha yako,
Huwezi kuzifikia baraka fulani mpaka uwe na Imani Kubwa kiwango fulani 🙌 wangapi wananielewa hapa😁
Kumbe tunapaswa kuomba Sana na kusoma/kusikiliza sana neno la Mungu ili tuifikie Imani kubwa kwasababu ili kwamba tufikie Mambo makubwa lazima tuwe na Imani kubwa ya kuyabeba/kuyapata mambo hayo pasipo kumkosea Mungu.
Unaweza kuomba pesa pekeyake na utajiri halafu kumbe Imani ya kuishi ukiwa ndani ya hiyo baraka ni ndogo unajikuta unapata kiburi na Roho ya kupenda fedha, tayari unamsahau Mungu bila kupenda/ kujua.
Umeomba ndoa yenye furaha Kweli Mungu amekupa lakini furaha inazidi Imani yako unalewa na ile furaha unamsahau Mungu.
Bwana atakupa afya njema na atakulinda kweli na ajali na kila namna ya hatari lakini utajiinua na kuona wengine wanaopata Shida Basi hawana nguvu za Rohoni/ hawajamshika Mungu wa kweli, ukajiinua bila wewe kujua kwamba hivyo unavyoenenda unajiinua
Utanishangaa kusema hayo lakini ajidhaniayekuwa amesimama na aangalie asianguke.
*1Wakorinto 10:12*
Tunamwitaji Mungu kwa ukubwa Sana pamoja na mafanikio yote tuliyonayo.
Tunahitaji Imani kubwa ili itusitili wakati wa dhambi inapokujia uwe na uwezo wa kuikimbia na kumpinga Shetani.
Petro na wenzake walikuwaa na Mungu mwenyewe yaani Yesu karibu lakini Kuna namna wakaona hapana hapa kwa namna hii Bwana utuongezee Imani, waliomba jambo hilo pasipo hata kujua kwamba imani inaletwaje. lakini leo ni lazima ujue kuwa unatakiwa kusikia sana sauti ya Mungu kwa yale yote aliyokuambia na akuambiayo ili imani yako ikue....
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo
Hatujui Kesho yetu, anajua Mungu.
*Ni maombi yangu kwamba utafanya juhudi ili imani yako iongezeke na uweze kubeba mambo makubwa pia ili uwe na UWEZO wa kuishinda dunia na kumpendeza Mungu.
*TUOMBE*
Mwenyezi Mungu Baba wa Mbinguni wewe ni wa Rehema tunakujua, Tena wewe ni Mungu wa kweli, na unatujua vyema na unajua hata yaliyo sirini mwetu, Yale tuyawazayo, tunenayo na tunayotenda kwa SIRI Bwana unatujua.Tunaomba uturehemu Bwana utusafishe kwa damu yako takatifu tuenende sawa na Neno lako Mungu🙌.Tunakushukuru kwa maana wewe ni Mungu utupaye vyote umetujalia Neema ya ajabu Sana kuiona siku ya leo, Ni upendeleo wa ajabu Sana Bwana umetupa sisi na familia zetu, hatuna Cha kukurudishia Bwana Bali pokea sifa za mioyo yetu.
tunaomba utupe neema ya kulisikia neno lako na kulitafakari ili tuzidi kukua kiroho na kimwili kwa utukufu wa jina lako🙌
Wema wako uende nasi siku zote, Sasa na hata milele Amina🙏
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl Beata Silwimba
0620507212 / 0742442164
Maoni
Chapisha Maoni