HUWEZI KUMUHONGA MUNGU

.            HUWEZI KUMUHONGA MUNGU

BWANA Yesu asifiwe watu wa Mungu. 

Leo ni siku nyingine naomba kuchukua nafasi na kibali cha kukujulisha na kukukumbusha jambo moja la msingi linalompendeza Mungu, ambalo wengi wamedanganywa na kupoteza kwa kudokuelewa. 

Soma hapa 👇

Mithali 21:3

[3]Kutenda haki na hukumu 

Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.

Unaona hapo, Biblia inasema kuwa kitu kinachompendeza Mungu ni haki na hukumu kuliko hata sadaka. kutenda haki ni kufanya sawa na mapenzi ya Mungu, au kufanya yampendezayo yeye na Hukumu ni kutenda sawasawa na amri yake

👉kwa utendaji huo ndipo Mungu anatuona sisi kuwa ni bora sana. 

kufanya haki na hukumu za Mungu kunatufanya kukubaliwa kuliko hata utoaji wa sadaka zetu

👉Tukisema tutoe sadaka angali tunafanya mambo yasiyompendeza Mungu, bado hatujampendeza Mungu zaidi kwamba tunakuwa tunafanya jambo linalomchukiza yeye. 

Soma hapa👇

Mithali 21:27

[27]Sadaka ya wasio haki ni chukizo; 

Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!

Unaona kumbe ukitoa sadaka huku hutaki kufanya mapenzi ya Mungu, basi ni machukizo mbele za Mungu.

👉Wengine hudhani kuwa wanaweza kuingia mbinguni au wanaweza kumpendeza Mungu kwa utoaji wao wa sadaka, kumbe hawajui ndipo wanamchukiza Mungu.

👉utoaji wa sadaka una maana kubwa na baraka nyingi endapo mtoaji wa sadaka hiyo ni mtenda haki na kuzishika hukumu za Mungu. na ndiyo maana YESU akasema hata kama kuna mtu umechukizana naye, umedukanana naye, unamchukia,.... basi usitie sadaka mpaka upatane nae akiwa na maana kwamba Jitakaseni kabla ya kutoa sadaka.

Soma hapa👇

Mathayo 5:23-24

[23]Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

[24]iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.

Hapo Yesu alisema hivyo akiwa na maana kuwa unapotoa sadaka usiwe na hila na ndipo sadaka yako itakuwa na maana mbele za Mungu.

👉lakini siku hizi kuna watu ambao wanadhani wanaweza kumuhonga Mungu pesa zao,, kwamba wafanye dhambi na kuishi katika tamaa na kuzitenda huku wakidhani kuwa atatoa sadaka tu nao watakuwa salama... HUO NI UONGO WALIODANGANYA NA SHETANI MWENYEWE,yaani ni uongo kutoka katika shimo la kuzimu.

Binafsi Kuna kanisa moja nilishawahi kwenda kusali kipindi cha nyuma,,, sasa mchungaji alipokuwa anahubiri akafika kwenye kipengele cha watu kumtolea Mungu sadaka. akasema kwamba 

👉 " Watu wa kanisani hawabarikiwi kwasababu hawatoi sadaka na ndiyo maana watu wa dunia hata majambazi wanafanikiwa kwasababu wanamuomba Mungu lakini pia wanatoa sadaka na ndiyo maana wanabarikiwa na Mungu". 

Sasa hapo kwenye kipengele cha jambazi kufanikiwa kwasababu ya utoaji wake wa sadaka. ni jambo ambalo halipo kabisa, kwasababu sadaka yake ni chukizo mbele za Mungu. 

yaani hata kwa hali ya kawaida kabisa👉inawezekanaje umempora mwenzako mali pengine ukamuua kabisa, halafu eti utoe sadaka yako kwa Mungu aliye hai na yeye akubariki. HILO SIYO SAWA. 

MUNGU HAHONGWI HIVYO.

Na sadaka ya mtu wa dunia anapoitoa inakuwa chukizo mbele za Mungu kwasababu ni chukizo. 

Na nichukizo kwasababu ni sadaka ya miungu na imetolewa kwenye madhabahu ya Mungu. 

Ni hivi👇

Mtu asipotaka kutenda haki ya Mungu bali akajihusisha na mambo ya dunia tafsiri yake ni kwamba anaiabudu na kuitumikia miungu yake ambayo pengine hata yeye haijui, na amekuwa ni mtumwa wa hiyo kama lisemavyo neno la Mungu kwamba atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 

👉sasa sadaka ya mtu wa miungu, hutoa kwa miungu yake. na ndiyo maana sadaka hii inapotolewa mbele ya madhabahu ya Mungu inakuwa chukizo. 

   Kwasababu sadaka ya Mungu ni ishara ya upendo kwa Mungu, utii kwa Mungu na shukrani kwa Mungu. 

👉sasa haiwezi kubeba maana hizo kama muhusika hana vitu hivyo badala yake inamchukiza Mungu. 

🙁Wengine huwa wanaenda kanisani, unapofika Muda wa sadaka wanaona kuwa watu watawaonaje, kwahiyo wanaamua kutoa sadaka tu bila hata kujua nini maana ya hicho wanachokifanya.

👉Na ndiyo maana kabla ya kutoa sadaka yako, chukua muda kidogo wa kusemezana na Mungu wako, jichunguze mahali ambapo pengine haupo sawa, kisha omba rehema, kisha iombee sadaka yako na ndipo uitoe.

👉kwa namna hii utaweza kukutana na baraka nyingi za sadaka yako na maombi yako maana itakuwa ni sadaka iliyoambatana na utii wa moyo wako mbele za Mungu.


Soma hapa👇

1 Samweli 15:22

[22]Naye Samweli akasema, 

je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu 

Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? 

Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, 

Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Na ndiyo maana hata Mungu alishawahi kuzikataa sadaka za wana wa israeli pamoja na ibada zao kwasababu walikuwa wanaenenda dhambini huku wakioa sadaka zao wakijidhani kuwa Mungu atawahesabia haki kwa sadaka zao tu

👉ailzichukia sadaka zao

👉ailzichukia nyimbo zao

👉alizichukia sherehe na sikukuu zao pia 


Soma hapa👇

Amosi 5:21-27

[21]Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.

[22]Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.

[23]Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu.

[24]Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu.

[25]Je! Mliniletea dhabihu na sadaka jangwani muda wa miaka arobaini, enyi nyumba ya Israeli?

[26]Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyizia wenyewe.

[27]Kwa sababu hiyo nitawahamisha, hali ya kufungwa, mwende mbali kupita Dameski, asema BWANA, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.

TENGENEZA MOYO WAKO, UTOE MOYO WAKO KWENYE MAMBO YA DUNIA UELEKEZE KWA MUNGU, ndipo utakapompendeza Bwana maana yeye anakutaka wewe zaidi kuliko hata sadaka zako. 

Mungu akubariki sana

Taifa Teule Ministry 

Mwl / Ev Mathayo Sudai 

0744474230 /0628187291 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI