JE MUME WAKO ANAKULINDA?
JE MUME WAKO ANAKULINDA?
Bwana Yesu asifiwe Mwanzo 20:1-8
Leo naomba ujifunze jinsi ambavyo, ulinzi na usalama wako upo kwa yule anayekuoa.
Hebu soma hapa 👇
[1]Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.
[2]Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara.
[3]Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.
[4]Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki?
[5]Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi.
[6]Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.
[7]Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.
[8]Abimeleki akaamka asubuhi na mapema, akawaita watumwa wake wote, akawaambia maneno hayo yote masikioni mwao, nao watu hao wakaogopa sana.
Nadhani umeielewa hiyo habari,🤔
Sasa ukisoma vizuri hapo utagundua kwamba Sara mke wa Ibrahimu, angeweza kuingia hatarini, pengine kuguswa na mume ambaye si wake, pengine, angedhalilika na kuvunjiwa heshima na huyu mfalme wa Gerari ambaye alitaka kulala naye siku ile.
👉Lakini Mungu mwenyewe ndiye aliyeingilia kati kwa kumwambia mfalme asijaribu hata kumgusa huyo mwanamke, kwasababu atakapofanya hatua hiyo basi atakuwa amekaribisha matatizo kwenye familia yake yote.
👉Lakini tunaona sara hakulala, au hakufanya mapenzi na mfalme aliyekuwa amemchukua kwa nguvu aliyonayo kama mfalme.
Sasa unaweza kujiuliza ni nini kilichomfanya sara kuwa salama? Utagundua ni AINA YA MUME ALIYEKUWA NAYE.
kwasababu tu Ibrahimu ana mahusiano mazuri na Mungu, mkewe hakuguswa...
Na mfalme alipata onyo kali kutoka kwa Mungu,,, yote hayo ni kwasababu Ibrahimu alikuwa mtu mwema mwenye mahusiano na Mungu.
Ibrahimu hakutumia nguvu yoyote ya kumfanya mkewe awe salama lakini, mahusiano yake na Mungu tu, ndiyo yaliyomlinda mke wake
Soma hapa👇
1 Petro 1:5
[5]Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
Sasa kama binti ndani ya Kristo ni lazima ujifunze kuwa Mume ndiye kichwa cha familia na ndiye mwangalizi na mlinzi wa familia yako.
👉Usijaribu kwenda kwa mtu ambaye unajua kabisa kwamba roho yako haitakuwa salama chini yake.
👉Haina maana ya kuishi maisha ya furaha, duniani halafu roho yako haiko salama.
👉Heshimu sana mahusiano yako na Mungu usimruhusu shetani akakupoteza kwa sababu ya mtu ambaye hawezi kukulinda.
🏓Wengi wanadhani mume anayeweza kumlinda ni yule mwenye pesa., kwamba akitaka chochote anapewa kwa wakati.
👉Lakini fikiria kipindi sara anakutana na hatari ile, Ibrahimu alikuwa na pesa gani, au alikuwa na mali gani?
Ibrahumu hapo alikuwa hana kitu kabisa, na alienda kwenye nchi ya gerari kwasababu ya njaa....
Lakini tunaona sala alilindwa na aina ya mume aliyenaye siyo kiwango cha pesa alichonacho mumewe.
Fahamu mambo haya👇
Mwanaume anaweza kuwa na pesa na mali lakini
👉Asiweze kukulinda
👉Asiweze kuwa na Mungu
👉Asijue jinsi ya kuitunza nyumba yake
👉Asiwe na akili ya kutambua thamani ya mkewe
👉Asiwe na maisha marefu
👉Asiwe na upendo kwako na kwa wazazi wako
👉Asiwapende ndugu zako
Mwanaume asiyekuwa na uwezo wa kusimama kama kichwa cha familia yako, basi jua hiyo familia haina kiongozi
👉Na kwasababu wewe ni mtu uliyeokoka, basi uongozi ni lazima uwepo wa kimwili na kiroho, mbali na hapo furaha unayoitaka hutaiona, amani unayoitafuta hutaiona.
🏓Usijaribu kutumia hisia za kimwili na tamaa au shauku ya kuolewa tu, pale uhapotafuta au unapotaka kuolewa na mtu, bali tumia hekima na jicho sahihi kuangalia kama utakuwa salama wewe na watoto wako utakapokuwa chini ya mwanaume huyo au la!
Ngoja nikusaidie hatari inayoendelea duniani kwa mabinti waliookoka.
Ni hivi👇
Mtu yeyote aliyeokoka na kumwabudu Mungu, huwa ni lazima awe na hazina fulani ( potential ) ya Mungu ndani yake.
🤔Na shetani hutafuta sana kuiondoa hiyo karama, au hicho kibali, au hicho kipawa, au hiyo sura ya Mungu iliyo ndani yako.
Sasa kama wewe upo hivyo ni lazima ujue kuwa wakati mwingine shetani hatakuja mwenyewe kukuharibu, bali atatumia mtu fulani ambaye atakuja kwa sura nzuri kabisa.
Na mara zote shetani huangalia uhitaji alionao mtu ndipo humjaribu sawasawa na uhitaji wake.
Na ndiyo maana hata Yesu alipokuwa nyikani amefunga siku 40,,, ile ya mwisho aliona njaa, na palepale baada ya kuona njaa ndipo shetani akaja kumjaribu kwa chakula, akamwambia KAMA WEWE MWANA WA MUNGU GEUZA MAWE HAYABO YAWE MKATE.
ni lazima ujue kuwa shetani alikuwa anajua kwamba Yesu anahitaji chakula na ndiyo maana akamgaribu vilevile.
Sasa hata wewe shetani anaweza akaina tamaa au haja uliyonayo ya kuingia ndani ya ndoa, hivyo ni lazima uwe makini,
👉Pengine anaweza kuja mtu ambaye anaenda sawa na uhitaji wako, na shetani atafanya hivyo ili kukupoteza.
Kuwa makini na mume unayemchagua, ni lazima uhakikishe kuwa roho yako na maisha yako yatakuwa salama chini yake.
Mume wako akiwa mlinzi wako na kichwa cha familia basi
👉Furaha itakuwa ndiyo kiini cha ndoa yako
👉Maelewano kwenu itakuwa ndiyo desturi yenu
👉Amani itakuwa ndiyo sura ya nyumba yenu
👉Mafanikio itakuwa ni kawaida kwenu
👉Upendo kwenu utakuwa ni pambo la nyumba
👉Utakatifu utakuwa ni njia yenu
Na Mungu atawabariki sana sawasawa na neno lake.
Mungu akupe moyo wa kuishi haya, kwa jina La YESU.
Taifa Teule Ministry
Mwl / Ev Mathayo Sudai
0744474230 / 0628187291
Maoni
Chapisha Maoni