WOKOVU TULIOPATA NI KWA NEEMA TU.

                   WOKOVU TULIOPATA NI KWA NEEMA TU.

*Waefeso 2:4-7*

[4]Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;

[5]hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

[6]Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

[7]ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.

Sisi  tu kazi ya mikono yake Mungu, tuliumbwa  ili tuyatende matendo mema, tangu awali Mungu aliyatengeneza ili iwe mwongozo wa maisha ya mwanadamu daima.

Lakini baada ya mwanadamu huyo kufanya dhambi akaenda kinyume na yale aliyowekewa ili aenende nayo, Shetani akatuchukua mateka kutoka kwenye miliki ya Mungu ( pale Edeni), akatufanya kuwa watumwa wa dambi😭 mwanadamu akamchukiza Mungu.

Sifa ya Mungu ni Mwenye upendo kwaa mwanadamu.

Ni Mwenye huruma nyingi.

Ni Mungu asiyependa mwanadamu aliyemuumba kwa mfano wake ateseke.

Ni Mungu anayejua kumsamehe Mtu makosa yake si Kama mwanadamu.

Mungu akaona mwanadamu aliyemfanya yeye mwenyewe anateseka na amekuwa chini ya utawala mwingine, akaamua kuingia gharama ya kutukomboa kupitia mwanaye mpendwa Yesu kristo ili Mimi na wewe tuwekwe huru baada ya  Umateka wa shetani😭

Ni dhahiri Kwamba ukombozi huu ulikuja kwa kila atakaye Amini na kukubali kuwa mateka kwa Mungu na si kwa Shetani.

Ndiyo maana iliachiliwa Neema hii ili kwa atakayeamini aambatane na Neema hii daima.

Mimi na wewe tulipata ukombozi huu kupitia ile Neema. Ndiyo maana hata sasa twadiriki kusema Yesu ni Bwana, tena ni mwokozi wetu

Lakini kwa wewe ambaye bado hujapata Neema hii ya kutoka kwenye Umateka wa dhambi acha kupoteza Muda na kujifariji kwamba ipo namna utaokolewa, hakuna namna nyingine zaidi ya kumkubali Yesu na kumwamini ili akutoe kwenye utumwa huo ulionao wa dhambi.

kumbuka upo wakati unakuja tena u karibu Sana  Neema hii itakoma. kubali leo Yesu akuhesabie haki ya kuitwa mteule wake.

*Waebrania 2:3*

[3]sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

Thamini wokovu ulioupata bure bila gharama bali kwa Neema ya Mungu tu.

Hakuna namna ya kupona na Ghadhabu ya Mungu pasipo kuthamini upendo wa Yesu.

Moyo wako umeuelekeza wapi ?

Upendo wako umeuelekeza wapi ?

Je ! ulivyookoka tu inatosha ?

Nini kimekutenga na Upendo wa Mungu.?

*Warumi 8:35*

[35]Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?

Je ni Mchumba /Mke / Mume,

Je ni kazi / utajiri wa dunia hii,

Je ni anasa na kujifurahisha mioyo yetu ndivyo vitutenge na wewe Mungu ? Hapana! hakuna cha kututenga na wewe Mungu , tumejitoa maisha yetu yawe sadaka mbele zako.

Sisi tu watumwa kwako, mtumwa hufuata Sheria za Bwana wake.

Chochote kisitutenge na upendo wa Kristo Yesu 

Kubali kuingia gharama ili utunze hiyo Neema uliyoipata, Jizoweshe tabia ya Mbinguni ili Bwana akudhihirishe katika utukufu wake siku ile.

Je ni heri kuipata dunia yote na utajiri wake halafu ukamkosa Mungu😭?

Hakuna hasara Kubwa utakayopata baada ya kumkosa Mungu ni zaidi ya hasara unayoweza kuipata kwenye Biashara zako / Mambo yako ya msingi

Ni zaidi ya hasara unayoweza kuipata unapowapoteza wapendwa wako wa karibu😔 

Ukimpoteza Yesu ni hasara Kubwa ambayo usitarajie kuipata kamwe maisha yako yote.

Hakuna faida Kubwa tunayoipata zaidi ya kumshika YESU.

Maisha bila Yesu ni bure na kujitaabisha na dunia, na mwisho wake ni mauti ya milele.


*TUOMBE*

EE MUNGU TUNAKUSIFU JINA LAKO LIMETUKUKA SANA, TUNAKUABUDU TUNAKUHESHIMU TENA TUNAYENYEKEA KWAKO MAANA WEWE NDIWE MUNGU WETU MWEMA.

TUNAKUSHUKURU KWA MAISHA HAYA ULIYOTUPA, TUMEOKOLEWA KWA NEEMA TU TENA TUMETAKASWA KWA DAMU ISIYOHARIBIKA DAMU YA YESU KRISTO SIFA NA UTUKUFU TUNAKUPA WEWE TU ADONAI🙌

MAISHA YETU BILA WEWE SI KITU KABISA ,HATUNA CHA KUTUTENGA NA WEWE YESU. TUNAOMBA UTUKUMBATIE BABAWA YATIMA, WEWE NI MUME WA WAJANE😭 TUNALISIFU JINA LAKO.

TUNAKUSHUKURU KWA UPENDO WAKO MKUU UMETULINDA DHIDI YA SHETANI KWA MWEZI MZIMA LEO NI MWANZO WA MWEZI MAY,TUNAJIKABIDHI KWAKO BWANA USITUPUNGUKIE TUSAIDIE KUKAA KATIKA MAPENZI YAKO. 

FAMILIA,KAZI, BIASHARA, HUDUMA,WATOTO WETU UWE MSAADA WA KARIBU.

BABA NINAKUSSHUKURU MAANA UMESIKIA KUOMBA KWETU AMEN🙏

*Mungu akubariki Sana*

Taifa Teule Ministry

Mwl Beata Silwimba 

0742442164 / 0620507212.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI