MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU
Bwana Yesu asifiwe wewe uliyependwa Sana na Mungu mwenyewe👏Nikualike katika Somo hili tujifunze pamoja kuhusu moyo wa mwanadamu na mtazamo wake.
kwanza tujue nini maana ya moyo?
zipo maana mbili za moyo;
Maana ya kwanza ya kawaida
Moyo ni kuingo Cha mwili chenye mishipa ya damu inayosukuma damu kwenda katika sehemu mbalimbali za mwili.
Maana ya pili ya Kiroho na hii ndiyo tutakayoiangalia Sana katika Somo hili.
Moyo ni sehemu yetu ya Kiroho ambayo Imani, hisia na matamanio hukaa.
Kwa maana hiyo tunapata kuelewa kabisa kwamba Mambo mengi yanayotokea kwenye maisha yako chanzo chake ni kwenye moyo.
Mambo fulani yaliyokupata yawe mazuri au mabaya chanzo chake ni kwenye moyo wa mwanadamu.
Tabia fulani ulizonazo zinaanzia ndani ya moyo wako.
Kumbe kila kinachotokea mwanzo wake ni kwenye moyo.
Tena moyo ni Hazina ya Mambo mengi, hutunza mambo yote uliyoyaruhusu yakae ndani yako.
*Luka 6:45*
[45]Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Soma tena.
Matendo ya Mitume 5:3
Mathayo 12:34
Lakini ili moyo utunze mambo fulani inategemeana na nini moyo umedhamilia kutunza✍️
Moyo wako unatazamia nini,
Moyo wako unaamini nini,
Moyo wako umejiandaaje kupokea mambo.
Moyo wako unatazamia nini kuhusu mambo?
Mithali 16:1-3
[1]Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;
Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.
[2]Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;
Bali BWANA huzipima roho za watu.
[3]Mkabidhi BWANA kazi zako,
Na mawazo yako yatathibitika.
Msingi wa somo letu uko hapa👆
Neno la Mungu linasema MAANDALIO ya moyoni ya mwanadamu Bali jawabu la ULIMI HUTOKA KWA BWANA. Lina maana kwamba vile ulivyovijaza ndani yako ndiyo vinavyokuendesha wewe Wala usimlaumu Shetani, bali Moyo wako ndiyo uliokubali Shetani auendeshe Moyo wako.
Nikiwa na maana kwamba wewe unauwezo wa kuzuwia mawazo ya Shetani yasikae ndani ya Moyo wako kulingana na vile ulivyouruhusu Moyo wako kutunza yaliyo mema.
Bwana huyathibitisha mawazo mema ya Mtu kulingana na Moyo wake unamtazamo gani kuhusu hayo mawazo yake, ndipo Bwana hithibitisha Neno lake hapo.
Moyo wa Mtu unaowaza mambo yake yasiyomuhusisha Mungu , Mungu humwacha MTU huyo akaendelea katika upotevu wake na hata kumkatilia Mbali.
Tabia ya Mungu huwa anasubiria MAANDALIO ya moyo wako ndipo huangalia nini akujibu kulingana na mtazamo wako
Umeuruhusu moyo wako kuyajaza mambo gani?
Moyo wako Unamtazamo gani kuhusu mambo yafuatayo??
*Neno la Mungu*
Zaburi 119:105,107
[105]Neno lako ni taa ya miguu yangu,
Na mwanga wa njia yangu.
[107]Nimeteswa mno;
Ee BWANA, unihuishe sawasawa na neno lako.
Je Moyo wako unaamini kwamba Neno la Kristo ndio kiongozi wa maisha ya mwanadamu aliyeamua kumfuata Kristo? Kama mtazamo wako upo hivyo ,je unafuata kile Mungu ameagiza katika Neno lake? (unaziishi Sheria za Mungu?)
Ukiona unaishi kwa mwongozo wa dunia hii Wala wewe so wakristo maana walio wa kristo huongozwa na yeye yaani Neno la Kristo
*Moyo wako unatazamia nini kuhusu Uponyaji*
Mungu wetu ni Mungu wa kuponya na kuokoa.
Moyo wako una mtazamo gani kuhusu Uponyaji🤔
mfano wewe ukiumwa huwa unakuwa na mtazamo gani kuhusu Mungu kukuponya?
Mfano ugonjwa huohuo wa kisukari, presha, Ukimwi, kisonono n.k alioumwa MTU fulani na pengine hakupona akafariki kwa ugonjwa huo huo, au pengine hajapona mpaka leo. Wewe Unamtazamo gani kuhusu Uponyaji wa Mungu? au mpaka upate Tiba fulani ndipo uamini unapona? wengi huangamia kwa kutokuamini uponyaji ulio katika Jina, na Damu ya Yesu Kristo.
Acha kuishi kwa mashaka ishi kwa Kuamini nguvu ya uponyaji iliyo ndani ya Yesu Kristo.
✍️kasome habari za Yule mama aliyetokwa na Damu miaka kumi na miwili
Marko 5:25-34
✍️Soma tena habari za Yule Mwenye kupooza miaka therathini na minane.
Yohana 5:5-9.
*Una Mtazamo gani kuhusu Watu.*
Je watu wote Ni wabaya tu, HAKUNA mwema?
Je wote wanatenda dhambi tu hakuna Mtakatifu hapa duniani?
Unawatazamaje watu,
Je unaona HAKUNA anayeweza kukusaidia chochote,
Je umewakatia tamaa watu wote kwamba huwezi kushirikiana nao katika Jambo lolote?
Naskushauri, uwe na mtazamo chanya kwa watu, ili uweze kushirikiana nao katika shughuli mbali mbali na katika kuijenga mwili wa kristo.
Japo wapo waisraeli (wayahudi ) hawakumuamini Yesu ,wakamtesa Yesu mpaka kufa lakini , wapo ambao walikuwa wanafunzi wake na walimwamini na kuyafuata mafundisho yake.
*Una mtazamo gani kuhusu Mahusiano ,Uchumba
Hadi Ndoa?*
Mithali 18:22
[22]Apataye mke apata kitu chema;
Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
Moyo wako unatazamia nini kuhusu Ndoa, kwanini umeweka mtazamo hasi kuhusu Ndoa, Je wanaume wote hawafai !? ,Je wanawake wote siyo wema ,je HAKUNA mwaminifu ambaye anaweza kukufaa wewe jibu ni hapana Wanaume Bora na Wake wema wapo wengi sana.
"Na ili uone fulsa lazima na wewe uwe kwenye uwanja wa filsa"
Nikiwa na maana kwamba ili umuone Mume au mke mwema kwenye maisha yako Anza wewe kuwa mwema ndipo utampata mwema.
Usitegeme kupata chema wakati wewe siyo mwema,
Mungu akasema nitakupa wa kufanana naye.
acha kuwatazama wanawake au wanaume kuwa wote wameharibika, ukiona humuoni mtu mwema Basi na wewe siyo mwema jitengeneze kwanza ndipo utaona mema.
Mwanzo 2:18
[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
*Una Mtazamo gani kuhusu kubarikiwa*
Kufanikiwa / kubarikiwa ni kwa watu wote,
Baraka ( Utajiri na Mali, Hekima na Maarifa) Hawajaolewa watu fulani bali tumeahidiwa watu wote .
Mwanzo 22:17-18
[17]katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
[18]na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Soma. Mwanzo 26:24
Kubarikiwa kumejikita katika Kumtii Mungu na kufanya kazi kwa bidii.
Kumbuka , halafu Elewa na uishi hivyo kwamba "Wewe siyo Masikini. Fanya kazi ,jitume katika kazi ya Mungu na Bwana Atalithibitisha Neno lake.
1 Mambo ya Nyakati 29:12
[12]Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.
*Una mtazamo gani kuhusu Ufalme wa Mungu*
Ufalme wa Mbinguni unatekwa na wenye nguvu za Rohoni.
Unatazqmini nini kuhusu kuja kwa Mwana wa Adamu mara ya pili?,
Moyo wako umejiandaaje?
Je bado unaona unao Muda mwingi wa kudumu katika Mazoea ya dhambi, Je hamjui miili yenu Ni hekelu la Roho Mtakatifu?
1 Wakorintho 6:18-20
[18]Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
[19]Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
[20]maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
*KUMBUKA MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU BALI JAWABU LA ULIMI HUTOKA KWA BWANA.*
Vile Moyo wako unavyotazamia na kuamini kuhusu mambo ndiyo ilivyo.
na hapo utaweza kujitafakari na kujielewa wewe Ni Nani na unaenda wapi.
Mungu akubariki Sana.👏
Taifa Teule Ministry
Mwl Beata Silwimba
0620507212 /0742442164
Maoni
Chapisha Maoni