MWANAMKE NI JESHI KUBWA
MWANAMKE NI JESHI KUBWA 🩸Jeshi kubwa, ni jeshi lenye nguvu kuliko majeshi mengine.kiutendaji, ki-msimamo, hata kimbinu pia, Tena Ni jeshi linalotegemewa Sana , ndilo jeshi kubwa. 🩸kwanini tunasema mwanamke Ni jeshi kubwa soma hapa,👇 Yeremia 9:20 [20]Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia. 🩸Mwanamke ametajwa kama shujaa wa kuomboleza mbele za Mungu. na moja kwa moja maombi ndio jiko kuu la mkristo halisi , Ni sawa na Nyumba lazima iwe na jiko, huko jikoni kunatoka chakula, huko jikoni Kuna Moto, huko jikoni Kuna vifaa vyote vinavosababisha chakula kikamilike na kuliwa😋. 🩸Mwanamke anafananishwa na jiko ndani ya Nyumba Na wakati mwingine ulishawahi kusikia watu wakimwita mwanamke Kama JIKO😃. 😇Mfano mwanamume anapo Oa utasikia Amepata Jiko. kwanini mwanamke an...