NGONO SIYO KIPAUMBELE CHA MABINTI NA VIJANA NDANI YA KRISTO


 NGONO SIYO KIPAUMBELE CHA MABINTI NA VIJANA NDANI YA KRISTO


Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.

  Napenda kuwajulisha, leo kuhusu jambo ambalo wengi wanalipenda na wengi wao wanajikuta hata wanafanya maamuzi mabaya ambayo ni kinyume cha amri na mapenzi ya Mungu.

Jambo lenyewe ni NGONO😯

👉Idadi kubwa ya watu wa dunia ya leo huwa wanaingia kwenye mahusiano na mtu, kwasababu ya hamu ya mwili ya kufanya ngono.

👉Kuna mtu unaweza ukamwambia, kuwa aina ya mpenzi aliyenaye, au aina ya njia anazotumia kupata Mume au mke siyo sahihi,

 unaweza ukamshauri kumuomba Mungu, lakini yeye unakuta ameshapata mtu wake ambaye pengine ameshamwambia atamuoa, akili yake haikuelewi kabisa na mwisho wa siku anakuja kwako tena kukuomba ushauri kwa yaliyomkuta.

Hali kama hiyo inawafanya vijana wengi kushindwa kuwatii wazazi wao, viongozi wao, au hata wachungaji wao na hata Mungu maana wengi wanaikutwa na hali hiyo matokeo yao ni kuacha kwenda kanisani, na kuona kana kwamba maisha na ku muabudu Mungu hakuna maana sana.

👉Hii yote ni kwasababu, wanapofikia kwenye kipindi fulani, wanakuwa na mihemko ya kingono, na wakati mwingine, utakuta wanajiita wakristo,... Sasa wanachokifanya ni kutamani kuolewa tu haraka kanisani ili awe na uhuru wa ngono.

👉Sasa ukiwa na lengo kama hilo, ni lazima ujue kuwa hisia za ndoa ulizonazo si sahihi.

😯Sisemi watu wasiwe na uhitaji wa kuingia ndani ya ndoa lakini chunga sana, ngono isiwe sababu ya kukosesha mbingu ., maana utafanya ngono mpaka uchoke bila hata kiasi,.... Na mwisho wake utayachoka maisha ya ndoa.

Sababu pekee inayofaa kukuingiza kwenye mahusiano ni lazima iwe ndani ya hizi hapa.👇

   1: KUTUMIA NDOA KUWA NJIA YA FURAHA YA MUNGU KUDHIHIRIKA. 

Ukiwa na familia nzuri, watoto wazuri, na utulivu ndani ya ndoa basi utakuwa na furaha sana kwenye maisha yako na siyo furaha tu pia furaha ya Mungu  itakuwa pamoja na wewe na familia yako itakuwa bora na yenye kuigwa


   2:KUUJENGA UFALME WA MUNGU KWA KUUBOMOA UFALME WA SHETANI, 

maana Biblia inasema ni heri kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa.

Maana yake kuwaka tamaa za ngono, kunafanya ufalme wa shetani kujengwa. Lakini ukiamua kuolewa au kuoa kwa wanaume na kuendelea na utakatifu basi unaujenga ufalme wa Mungu.

Hebu soma hapa👇

Mathayo 1:24-25

[24]Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;

[25]asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.

Unaona hapo, unamuona Mariamu mama wa Yesu na Yusufu, hawakuwa na mihemko ya kufanya ngono japo ndiyo walikuwa wameanza kuwa pamoja muda mfupi tu.

Lakini Biblia inasema hawakujihusisha na ngono mpaka alipozaliwa mtoto Yesu.

😯Hata wewe unaweza ukaona kwamba baada ya kuoana walikaa muda gani bila kushiriki ngono.?

  Je unafikiri walikuwa hawapendani?.... 

  Halafu linganisha na maneno ya vijana wa leo walio dhaifu ambao wanaamini kuwa, huwezi kukaa hata mwezi mmoja bila kufanya mapenzi au ngono na mtu.

🤔🤔Ukilijua hili utaelewa kuwa upendo ni zaidi ya ngono. 

  Na ukiona mtu anasema anakupenda kwa kukupa mapenzi na ngono kila siku, basi ni lazima uwe na macho ya kuona aina ya upendo alionaio kwako. 

         💕upendo ni zaidi ya ngono. 

   Na wengine wameokoka, na wanawachumba wao halafu unakuta mchumba wake anamwambia, wafanye ngono, naye anakubali kufanya akiogopa kuachwa na mchumba wake kwa kumkatalia. 

Hebu jiulize tu hata wewe ni upendo gani huo ambao mtu anakufarakanisha wewe na Mungu kwa kigezo kuwa anakupenda.? 

Huo ni upotevu🙏

  Na ukiona mchumba anakupa habari hizo kabla ya ndoa basi jua hakuwazii mema. 

Kwasababu mtu anayekupenda, hawezi akakubali kuona unapotea mbele ya uwepo wa Mungu, bali atakulea, atakufundisha na kukuombea uendelee kukua kiroho, ufahamu, na hekima ya kuongoza nyumba yako. 

Sisemi kuwa mapenzi ni mabaya, HAPANA! Ni jambo zuri tena sana kwa wana-ndoa na ndiyo maana Paulo alisema jambo hilo ni lazima liwepo

Soma hapa👇

1 Wakorintho 7:5

[5]Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

👏Lakini aliongezea kwa kusema hata waliopo kwenye ndoa wafanye lakini wawe na kiasi ili wasije wakashindwa kufanya mambo mengene ya Mungu, na kuwafanya kuongozwa na mwili tu, hata kumtenda Mungu dhambi. 

   Lakini kwa wale ambao hawajaingia kwenye ndoa bado, basi ni lazima muwe makini, 

Yaani usije ukajaribu kumpenda mtu au kuolewa na mtu kwa lengo la kutimiza haja ya ngono kwa kusema kwamba; utakuwa unafanya muda wowote unaopenda. 

👉Kumbuka ndoa ni zaidi ya ngono, ndoa ni idara ya Mungu mwenyewe inayoshughulika na kuyatimiza mapenzi ya Mungu siyo ya Mwili. 

👉Na pia hata mwanaume ambaye ana akili na anajitambua, Na kumuheshimu Mungu, huwa hana kipaumbele cha ngono kwenye uchumba wake. 

Anajua ni jambo ambali lipo kwa wakati wake na Mungu ameliandaa. Hutaona akikwambia kufanya ngono kabla ya wakati. 

Binti kama unaongozwa na ngono na mihemko ya ngono, jiulize utakubali kuongozwa na roho wa Mungu kweli.? 

  Kwasababu Biblia inasema anayeongozwa na Roho hawezi ongozwa na mwili na anayeongozwa na mwili vilevile hataweza kumtii Roho mtakatifu, na akashauri bora kuongozwa na Roho. 

Wagalatia 5:16-17

[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

[17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.


Leo nakualika🙏

Welcome to the house of Holiness 

Welcome to the family of Sonship

Welcome to the house of prayer 

Welcome to the family of incorruption

Welcome to the family of New Priesthood 

Welcome to the family of Truth


KUMBUKA MAJIRA YANAENDA MUNGU ANACHAGUA WALIO WAKE MUDA HUU! 

Je umeokoka,? au unahitaji kuokoka hapo ulipona kubatizwa ubatizo sahihi, basi piga simu kwa namba hizo chini👏

Mungu akubariki sana! 



Taifa Teule Ministry 

Mwl/ Ev Mathayo Sudai 

0744474230 / 0628187291

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI