KINYWA CHAKO NDICHO MWAMUZI WA NINI KIKUKUTE
KINYWA CHAKO NDICHO MWAMUZI WA NINI KIKUKUTE
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.
Leo naomba tujifunze kitu kuhusu habari YA KINYWA.
Tunaposema habari ya kinywa moja kwa moja tunahusisha na kuambatanisha habari ya mtu kunena kitu chochote kile bila kujali mazingira, hisia, kazi yake na utambuzi wa kile anachokisema.
👉Kinywa ni kinywa tu, na kila kinywa kina nguvu ya kuandaa maisha ya mtu au njia ya mtu kupita yeye mwenyewe.
Kinywa kimewekwa kutoa sauti za lugha fulani ampapo kila lugha za sauti hizo huwa ina maana katika ulimwengu wa roho.
👉Yani hakuna sauti isiyo na maana👇
1 Wakorintho 14:10
[10]Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hakuna moja isiyo na maana.
Sasa ni lazima ujue kuwa hata maneno na lugha zetu zinabeba maana na mamlaka fulani katika ulimwengu fulani.
👉Kinywa kuzaa madhara au uzima, inategemeana na muhusika ana nena kitu gani
Soma hapa👇
Mithali 18:21
[21]Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;
Na wao waupendao watakula matunda yake..
👉Kwahiyo, kutembea kwenye utumwa wa shetani na mauti, au kuwa na uzima, ihategemea unakiri nini na kinywa chako kipo kwenye mamlaka gani.
👉Kinachopatikana kwenye maisha yako kama matunda ni matokeo ya kinywa chako.
Soma hapa👇
Mithali 18:20
[20]Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake;
Atashiba mazao ya midomo yake.
Ukifuatilia vizuri utakuja kujua kuwa, hutakiwi kuwa mtu wa kuzungumza, kufakufa na uharibifu kwasababu kinywa ndicho huwa kinapanga maisha ya mtu ya baadae na nini kimkute au akipate.
Kinywa ndicho kilichofanya haya👇
👉Kuumba wanyama na mimea
👉Kufanya nuru iwe ulimweguni pale ambapo dunia ilipokuwa giza tupu
Soma hapa👇
Mwanzo 1:3
[3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
Mungu, AKASEMA, yaani alitamka kwa kinywa.
👉Kumlaani mwnadamu
Soma hapa👇
Mwanzo 3:16-17
[16]Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
[17]Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
Na mengine mengi kama vile tunavyoisoma Biblia.
Lakini kumbuka mtu aliyeokoka, ana nguvu ile ile ambayo Mungu aliitumia kumfufua Kristo dhidi ya mauti.
Nguvu ile ile ndiyo anayo mtu aliyeokoka, soma hapa 👇
Warumi 8:11
[11]Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Ni lazima ufahamu hivi👇
Kila neno ambalo linatoka kwenye kinywa cha mtu, huwa linatekelezwa na roho iliyopo nyuma ya maneno hayo.
👉Kimsingi, maneno tu peke yake si kitu, lakini kwasababu nyuma ya kila neno kuna roho inayolitekeleza neno hilo, basi yakupasa kuwa makini sana na kile unachokitamka.
Kwasababu unapotamka tu, ile roho nyuma ya ulichokisema inaanza kutenda kazi
👉Kama umenena uharibifu, basi ile roho ya uharibifu nyuma ya maneno yako inaanza KUTEKELEZA neno lako.
👉Kama umenena uzima basi roho ya uzima inaanza kufanya kazi
👉Kama umenena laana, basi ile roho ya laana inaanza kutenda kazi.
Na ndiyo maana Kristo alitufundisha kupitia yeye mwenyewe kwamba kila neno lina roho nyuma yake.
Soma hapa👇
Yohana 6:63
[63]Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Kumbe unaweza kuona ni maneno tu lakini si hivyo, hayo maneno ni roho kabisr na ndiyo inayotekeleza kile unachokitoa kupitia kinywa chako.
đź‘ŹKinachotokea ni hiki........ Unapotoa maneno fulani huwa yanapokelea na anga( ulimwengu wa roho) na yanapopokelewa,... Kumbuka kila sauti ina maana, na ina mamlaka fulani, hivyo ikipokelewa inafanya mambo fulani kusogea, kutendeka, kuchakatwa kwa ajili yako sawasawa na ulivyotamka.
👉 Na baada ya kuwa mchakato umekamilika kwenye ulimwengu wa roho, majibu yake yanarudi kwa muhusika, na ndiyo maana, tunavuna tulivyovipanda wenyewe.
Wagalatia 6:7
....... ; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
Na ndiyo maana tumeona kwenye mithali kuwa kila mtu anakula na kushiba matunda ya kinywa chake mwenyewe.
Kumbuka: Haijalishi unachokitamka ni kizuri au kibaya,,, ni lazima kipokelewe kwenye ulimwengu wa roho( anga) na majibu yanarudi kama kawaida.
👉Na ndiyo maana unatakiwa kuwa mtu wa kunena mazuri tu wala usijaribu kujinena uharibifu maana utavuna matunda yake.
Na ndiyo maana Biblia inasema hivi👇
Yakobo 3:10-12
[10]Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
[11]Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
[12]Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.
👉Wakati mwingine shetani hukuonyesha hali ngumu ya maisha kwa macho ya nyama yasiyoona kitu mbali na vile unavyoona mwilini.
👉Huwa anaweza kukuonyesha hali mbaya ya ugonjwa,
👉Hali mbaya ya kifamilia
👉Hali ya kutokuwa na faraja.
Na hufanya hivyo kwasababu anajua hana uwezo wa kukuangamiza wewe, ila anachokitaka uanze kujiangamiza mwenyewe kwa yale utakayoanza kuyatamka kulingana na kile unachokioa, kwahiyo anakuwa amekutega na ndiyo maana ya maneno haya 👇
Mithali 6:2
[2]Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako,
Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
Basi kuwa makini na kile unachokisema, na usije ukajaribu kumtafuta mchawi aliyekuroga kama una desturi ya kunena kushindwa, ni lazima ujue wewe ndo mchawi anaekuroga wewe.
Yaan unajiangamiza mwenyewe huku shetani akiwa amekaa pembeni akiangalia mkristo asiyejua kutumia kinywa anavyojiangamiza mwenyewe.
Leo yafute maneno uliyojitamkia ambayo ni ya kushindwa kwa damu ya Yesu na anza kutengeneza desturi ya kusema mambo yenye uzima kwako
Mungu akubariki
Taifa Teule Ministry
Mwl / Ev Mathayo Sudai
0744474230 / 0628187291
Maoni
Chapisha Maoni