MAMBO 8 YANAYOPIMA UAMINIFU WAKO KWENYE MAHUSIANO.
MAMBO 8 YANAYOPIMA UAMINIFU WAKO KWENYE MAHUSIANO.
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.
Leo naomba kuja na ujumbe huu wa jambo ambalo kwa maisha ya uchumba na ndoa nyingi, limekuwa ni tatizo ambalo linawafanya wengi kufikia talaka.
Jambo hilo ni UAMINIFU ndani ya uchumba au ndoa.
Uaminifu kiufupi ni uwezo wa kuaminiwa.
Kuna mtu anaweza akakupa kitu chake cha thamani, kukukopesha fedha, huku akijua kuwa utamrejeshea tu, kwasababu ya sifa yako ya uaminifu.
Ukiwa mwaminifu katika uchumba wako, au ndoa yako, utakuta hata mwenzako ana uwezo mkubwa sana wa kukuamini na hata kupunguza yale matatizo yanayotokana na kukosa uaminifu.
👉Wengi huwa si waaminifu kwenye mahusiano yao kwasababu huwa hawana malengo na wale ambao wapo nao kwenye mahusiano.
🤔Ukiona upo kwenye mahusiano na mtu ambayo hayana malengo yoyote, basi uwe na asilimia 100 kwamba pengine haupo pekeyako. Na ndiyo maana hana malengo na wewe. Na pengine kuna mtu ambaye ana malengo naye ya ndoa....Na hilo ni jibu kabisa kwamba mpo wengi.
đź‘ŹNatamani sana mabinti ndani ya Kristo muelewe nini maana ya uaminifu kwenye uchumba na jinsi ya kuangalia uaminifu wa huyo mchumba ambaye pengine ameshakwambia kuwa atakuoa.
🤔Kataa sana kuwa mke wa pili,.... Kama unaona mpo wengi basi ni lazima ujue kuwa, ndoa ya namna hiyo haimpendezi Mungu hata mara moja....
Sasa ili ujue kuwa kuna hali nzuri kwenye mahusiano yako kama binti uliyeokoka ni lazima suala la uaminifu baina yenu liwepo kwa ukubwa wote.
👉Mmoja akikosa kuwa mwaminifu, kwa mwenzake basi kuna uwezo wa kuchafua malazi, na kupoteza heshima ya ndoa
Soma hapa👇
Waebrania 13:4
[4]Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Ukikosea kwenye jambo hilo basi jua kuna adhabu mbele za Mungu.
Jifunze kuwa mwaminifu, na mfunze mwenzako, mrekebishe pia kama unaweza kumrekebisha katika jambo la uaminifu.
👉Kukosa uaminifu ni mlango wr kuruhusu shetani aharibu mambo yenu yote, ndani ya nyumba au uchumba.
👉Mwaminifu anaweza kukaa na mchumba kwa muda mrefu, hata kama atachelewa kuingia kwenye ndoa, bado hataweza kutoka nje ya mipango aliyoiweka yeye na mchumba wake.
👉Mtu ambaye hana uaminifu, anauwezekano mkubwa sana wa kutafuta mtu mwingine pale ambapo mwenza wake hatakuwepo. Au katika hali fulani ya ugumu ambayo mwenzake atakuwa anapitia.
TAFAKARI KIDOGO.
Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini, kuna mambo fulani ulishawahi kuyaomba kwa Mungu, na yeye alisikia lakini bado hajakupa?
Jibu ni kwamba hata Mungu huwa anapenda sana watu wake wawe waaminifu, na uaminifu hupimwa kwa uvumilivu na ndiyo maana kuna wakati Mungu anataka kutuaona je, tuna uaminifu wa kutokutafuta miungu mingine na njia zingine za kufanikiwa pale ambapo tutapita kwenye ugumu wa maisha.?
Pengine umeomba sana kuhusu ndoa, lakini je wewe ni mwaminifu.
👉Kuna watu huwa wanapanga hata kuacha kumuabudu Mungu, kwasababu tu waliomba kuolewa na hawajaolewa.
🙏Binti yangu nakujulisha leo kuwa ukipanga kumuacha Mungu, kama hatokupatia kile unachokitaka kwa wakati fulani,,,, basi nakushauri hata usijisumbue sana kuomba, kwasababu huko ni kumjaribu Mungu na Mungu huwa hajaribiwi.
Inatakiwa uombe hata kama unaona majibu yanachelewa,...
👉Lazima ujue kuwa majibu ya Mungu huwa hayachelewi bali huja kwa wakati.
ENDELEA KUWA MWAMINIFU.
👉Mungu mwenyewe anahitaji sisi tuwe waamnifu kwake kwa gharama yoyote, kwamba tusije tukamuacha yeye na kufuata njia zingine mbaya.
Soma hapa👇
Ufunuo wa Yohana 2:10
....................... Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
Kuna mambo fulani ambayo huwa yanampima mtu kama je, ana uaminifua au hana ndani ya mahusiano ya uchumba au ndoa.
👉Pengine hujui kuwa mchumba wako ni mwaminifu au la! Au pengine hujui kewa wewe ni mwaminifu au la!. Basi ni lazima ujue uaminifu huonyeshwa na kutambulika kwenye mambo yafuatayo.
MAMBO 8 YANAYOPIMA UAMINIFU WAKO KWENYE MAHUSIANO.
1: UGONJWA
Ni jambo la kawaida kuona watu wanakimbia wapendwa, wapenzi, wachumba au wake na waume zao, kwa sababu ya ugonjwa fulani.
Ukiona unawaza kutafuta mchumba mwingine na kumuacha uliyenaye, eti kwasababu amepatwa na ugonjwa fulani, basi jua wewe si mwaminifu
2: UKOSEFU WA KAZI
Kuna watu wengine huwa wanapambana na maisha kwenye, kazi fulani lakini pale wanapopoteza au kukosa kazi utakuta wachumba wao wanawakimbia na kutafuta wengine wenye pesa. Huu nao ni ukosefu wa uaminifu
3: KUTOKUWA PAMOJA KWA MUDA MREFU
Tena hapa huwa pana shida sana. Kuna mabinti wengine, huwa hawawezi kukaa bila kujihusisha na ngono, au kuwa karibu na wachumba wao jambo linalopelekea kushindwa kujizuia na kuamua kuwa na mahusiano na mtu mwingine.
Kuna kazi ambazo zinaweza kupelekea watu kuwa mbali kwa kitambo kidogo, kama vile. Madereva wa masafa marefu., Maaskari, wafanyakazi wa ndege, na pia wafanya biashara wakubwa.
👉Kama ukikosa uaminifu basi jua utakuwa na mahusiano ya kingono na watu wengi pale ambapo utashindwa kuwa mwaminifu kwa mchumba au mume wako.
4: UMASKINI
Ni lazima ujue kuwa maisha na kipato ni baraka kutoka kwa Mungu, na hivyo haipaswi kabisa wewe kukosa uaminifu kwa mwenzako pale ambapo kipato kitakosekana.
👉Usijaribu kukosr uaminifu kwa mwenza wako, eti kwasababu kuna hali ngumu ya maisha umekutana nayo.
👉Ni jambo la kusikitisha, mabinti waliokoka kuamua kuvunja hata amri ya Mungu na kumsaliti mchumba wake au mume wake, eti kwasababu alikosa pesa kwa muda fulani.
👉Usijaribu kuulinganisha mwili wako na kitu chochote, wewe ni wa thamani sana, hakuna kitu kinachoweza kukununua wewe kwa maana ulishanunuliwa kwr bei ipitayo bei zote yaani DAMU YA YESU. Hivyo usimruhusu mtu akakuchezea kwa tamaa ya Mali na pesa na hata ukajikuta umekosa uaminifu kwa mwenza wako na kwa Mungu.
5: MAFANIKIO YA HARAKA.
Kuna mtu anaweza kuwa kwenye mahusiano na mtu wa kawaida tu, mwenye kipato cha kawaida kinachoendesha maisha yake vizuri tu,
Lakini anapotokea mtu mwingine, pengine ana gari, au pesa nyingi, au nyumba nyingi, au pengine ana elimu kubwa na sif fulani ambazo binti huyu anazitaka. Utashangaa dhafla binti anamsaliti na kumuacha mchumba wake na kuamua kuwa na huyu mwenye mali na sifa kubwa.
👉Yani kwa mtu ambaye anaelewa maana ya mahusiano na ndoa chini ya mwongozo wa Mungu, atagundua kwamba huyu binti, hakumuomba Mungu, wala hakuwa na maono yoyote pale alipoingia kwenye mahusiano, na ndiyo maana amehamisha mahusiano kwa mwingine mwenye mali.
Kwasababu kama kweli uliomba na ukampata uliyenaye, imekuwaje KUBADILIKA au je umeona maono mapya, na je kama umeona maono mampya, vipi kuhuyu yale uliyokuwa nayo mwanzo uliyapata wapi?
6: UZEE
Kwenye ndoa za siku hizi kuna mambo ya ajabu sana ambayo yanaonyesha kukosa uaminifu,
Eti utakuta mume au mke anaamua kutafuta mtu mwingine, na kuanza mahusiano naye eti kwasababu yule mume wake au mke wake amekewa mzee.
Wazee wengi siku hizi wanataka mabinti wadogo. Na kuna wanawake wengi siku hizi wanahitaji vijana wadogo, eti kwasababu waume zao wamezeeka.
🤔Kuwa makini sana maana unakosa uaminifu kwa Mungu na kwa mwenza wako. Utaingia jehanamu.
7: KUKOSA WATOTO KWA MUDA MREFU
Watoto nao ni baraka ambazo tunazipata kutoka kwa Mungu,
👉Pale ambapo utachelewa kupata watoto ndani ya ndoa yako, usijaribu, kupiga hatua kutafuta mtoto kwa jilani, japo kwa wanawake ni mara chache bali kwa wanaume ndipo penye shida.
👉Pale mtoto anapokawia kwa muda, huwa wanakosa uaminifu na kuamua kutoka nje ya ndoa jambo ambalo ni kosa kwa mkewe na mbele za Mungu, maana huo ni uzinzi na unawapeleka jehanamu.
Na mwanamke anapoona kuna tatizo kwa kukosa mtoto huwa anaweza kuwaza kufanya jambo lolote ili tu aiponye ndoa yake.
Kama vile Raheli aliamua kumwambia mumewe Yakobo alale na mjakazi ili tu apate mtoto
Soma hapa👇
Mwanzo 30:1-3
[1]Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.
[2]Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?
[3]Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye.
Sasa ni lazima ujue kuwa kukosa mtoto, si kwamba utakuwa umelogwa tu, hapana pengine Mungu huwa anaamua kufunga kizazi cha mtu kwa kusudi fulani.
Hivyo linapotokea tatizo kama hilo, usijaribu kutoka nje ya mstari bali sema na Mungu tu, yeye ndiye anayejua vyote.
8: UHITAJI WA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA
Yaani ni lazima ujue mchumba ambaye anakutaka ufanye naye ngono kabla ya ndoa🙂🙂 ni mbaya sana kwasababu zifuatazo
👉Hamuheshimu Mungu
👉Haoni shida kuharibu uhusiano wako na Mungu
👉Anakuuza kwenye mikono ya shetani na kukufanya kuwa mfungwa wa dhambi.
Kwasababu Biblia inasema ataendaye dhambi ni Mtumwa wa dhambi
Soma hapa👇
Yohana 8:34
[34]Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
Sasa kuna watu ambao huwa wanapohitaji kufanya tendo la ndoa, kabla ya ndoa, na wachumba wao wanapokataa, basi wanaamua kutafuta mtu mwingine ambao wataweza kuwatimizia haja yao.
Binti, ni heri kumuacha huyo mtu kuliko kukubali kufanya uasherati na kujifanya adui wa Mungu, eti kwasababu ya kulinda mahusiano na mtu asiyekuwa na adabu mbele za Mungu.
Yaani ni lazima ujue kuwa kabla ya ndoa yoyote ile ambayo wewe utaingia.... Tayari kuna ndoa iliyo kuu kati ya wewe na Kristo, na hii ni lazima iheshimiwe kuliko maelezo.
👉Sasa ukiamua kuivunja ndoa ya wewe na Kristo ili kujenga ndoa ya mtu na mtu basi jua, unafanya makosa.
🙂KATAA UASHERATI ili Utembee na Mungu
AMENI
Kwa haya mambo nane unaweza kabisa ukajipima na ukapima, uaminifu wa mchumba wako na mengine mengi ambayo yanafanana na haya.
Uaminifu ni tatazo kwa walio wengi na ndiyo maana kuna mtu unaweza ukaona anawapenzi wengi, na kila anapoenda anamuacha yule wa kwanza anapata mpya wa eneo hilo, mwingine anawachanganyachanganya tu.
Ukiona una tabia kama hizo kwanza jua kabisa
Umemkosea Mungu, na pia wewe si mwaminifu.
Mungu akubariki
Taifa Teule Ministry
Mwl / Ev Mathayo Sudai
0744474230 / 0628187291
Maoni
Chapisha Maoni