SEMA KWA MAMLAKA YOTE

 



                     
  SEMA KWA MAMLAKA YOTE 

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu 

Leo naomba kuwakumbusha watumishi wa Mungu wanaotamani na wale wanaotembea chini ya kusudi la Mungu. 

  Kimsingi ni kusudi na mpango wa Mungu kabisa kwamba kila mtu awe ndani ya kusudi lake. 

Watu wengi wamepokea karama na agizo kutoka kwa Mungu, na wengine wana huduma tofauti tofauti ambazo Mungu huwapa kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo yaani Kanisa. 

Soma hapa👇

Waefeso 4:11-12

[11]Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

[12]kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

Sasa ni lazima ujue kuwa kila mtu aliyeokoka, amepewa jukumu lake ndani ya kanisa kama vile ambavyo kila kiungo cha mwili kilivyo kila kimoja na jukumu lake, na hakuna kiungo chenye thamani kubwa kuliko kingine. 

Soma hapa👇

1 Wakorintho 12:21-22

[21]Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.

[22]Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi.

Lakini kuna jambo baya sana ambalo, shetani ameliweka kwa vijana na watu wengi ambao wanaaminiwa kuwa na nguvu ya Mungu. 

👉Shetani siku hizi anawaaminisha vijana kuwa kumtumikia Mungu ni uzeeni, na ujanani ni kula maisha. 

👉Wengine amewadanganya kwa kuwaambia hakuna ajuaye habari za jehanamu, mbingu, na shetani, kwahiyo wanachotakiwa ni kula na kunywa maana kesho watakufa. 

Lakini Biblia inadai kuwa vijana ndiyo wenye nguvu ya Mungu, na mahali pengine inasema, saa sahihi ya mtu kumtafuta Mungu ni ujanani ( Muhubiri 12:1 ) 

Na wale waliyopo ndani ya kanisa wanaojiita wakristo, wamekosa tofauti na watu wa mataifa, wasio na wokovu. 

  👉Ni lazima ujue kuwa Mungu siyo mwanadamu, ambaye tunaweza kuwa tunamchezea tunavyotaka, na kumdhihaki. 

👉Ni lazima ujue kuwa unapokuwa katika maisha yako, kuna kipindi neema na huruma ya Mungu unayoiaona hutaiona kamwe 

👉Yale yote unayoyaona ni mema ambayo asili yake ni shetani, basi kwa hayohayo ndiyo utakayohukumiwa. 

Soma hapa👇

Mhubiri 11:9

[9]Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.

Unaona hapo Biblia inasema na kijana, mtu mwenye nguvu kwamba aendelee tu kutembea katika kile kitu anachokipenda kimwili na tamaa ambazo anaziendea, lakini kwa hayo Mungu atamleta hukumuni. 

Lakini kama wewe ni mmoja ya watu wa Mungu wenye kujua kusudi la Mungu na upo tayari kwa kazi ya Mungu, ni lazima ujue kuwa kwasasa 

👉utadharauliwa sana, 

👉utaonekana mshamba sana, 

👉utadhihakiwa sana, 

👉utachekwa sana, 

👉utapingwa sana na wengine kukusengenya na kukusema vibaya 

Na ni lazima ujue watakao kufanyia mabaya zaidi ni wale ambao wanajiita wakristo wenzako

👉Jiandae kupokea kejeli na dharau kutoka kwa hao watu wa dini

👉Kama ni binti basi utachekwa sana na wenzako na kuonekana huna jipya

👉Kama ni kijana utaonekana, umepotea sana huna la kufanya 

Lakini, usiogope maana kuna wakati unakuja na hata sasa umewadia ambapo yule anayeonekana mshamba leo, ndiye atakayeonekana mjanja na wengi watatamani kuwa kama yeye lakini muda huo hautakuwepo. 

👉Maana hata Mungu mwenyewe atawakataa

Soma hapa👇

Luka 13:25-27

[25]Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

[26]ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

[27]Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

Wewe mtu wa Mungu unayemuheshimu Mungu na kushirikiana na watakatifu walio duniani katika kuujenga mwili wa Kristo, nakusihi endelea katika imani hiyohiyo, na kuendelea kuisema kweli ya kristo kwa mamlaka yote

Soma hapa👇

Tito 2:15

[15]Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.

Unaona hapo, umepewa kusema na kulitaja jina la Bwana, kuonya bila kujali watakavyosema, kufundisha neno la Mungu KWA MAMLAKA YOTE ikiwa na maana kuwa Mungu yupo pamoja na wewe.

   Nakusihi usijaribu kuwafuata hao wajiitao watu wa dini lakini wanatembea katika udhalimu.

Lakini Paulo alimwambia Tito apundishe, akaripie na kuonya kwa mamlaka yote na Mtu yeyote asimdharau. 

😔Hebu jiulize sisi tumepewa agizo la kufanya kwa mamlaka ya Mungu, je nini adhabu ya mtu anayetudharau? 

     👉Biblia imeweka bayana juu ya ghadhabu ya Mungu juu ya wanaomdhihaki yeye na kumdharau. 

Wewe yakupaa kujua kuwa:

Unapochukua jukumu la kutembea na Mungu, basi jua kabisa kuwa mamlaka yote na moyo wa Mungu upo pamoja na wewe. 

Mungu akubariki sana


Taifa Teule Ministry

Mwl / Ev Mathayo Sudai

0744474230 / 0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI