MAMBO 8 YA KUYASHIKA ILI UWE MKE KAMILI

  MAMBO 8 YA KUYASHIKA ILI UWE MKE KAMILI

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu. 

Leo naomba tuziangalie sifa za Mke kamili. 

Kuna mke ambaye ndani ya familia, anaweza kuonekana, ana mapungufu mengi mbele ya Mume wake, siyo kwasababu, mume hajatulia bali kuna wakati fulani, mwanaume huwa anaangalia namna ambavyo mwanamke anajiweka. 

Kwa asilimia kubwa mke mwema na aliyekamilika lazima ajitahidi kulingana na maandiko ni lazima ajitahidi kuwa na sifa hizi hapa👇

1: MKRISTO ANAYEWAJIBIKA NDANI YA UKRISTO

Mke mwema ni lazima amche, na hata kumtumikia katika nafasi yoyote aliyombariki. 

👉Mke anayemtii Mungu nr ni mkristo sawasaw, basi anauwezo mkubwa wa kudumu, katika fulaha ya ndoa na hata kuishi maisha ya ushindi. 

   đź‘‰Si sawa na wale wanawake ambao Ayubu aliwaita, WAPUMBAVU ambao hata kuongea na kuwaza kwao ni udhalimu mtupu., wameishikilia dunia tu, wazinzi, wana vinywa vichafu na mambo kama hayo. 

2: ANAYEFANYA KAZI

 yaani mwenye uwezo wa kutafuta kipato, hakuna mahali ambapo Biblia imemtaka mke mwema awe wa kukaa nyumbani, kama mama wa nyumbani bali anafaa sana awe mwenye uwezo wa kuchakalika, huku na kule,... Na Biblia inakiri kuwa akiwa hivyo hata mume wake atamfurahia. 

Soma hapa 👇

Mithali 31:10-19

[10]Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? 

Maana kima chake chapita kima cha marijani.

[11]Moyo wa mumewe humwamini, 

Wala hatakosa kupata mapato.

[12]Humtendea mema wala si mabaya, 

Siku zote za maisha yake.

[13]Hutafuta sufu na kitani; 

Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.

[14]Afanana na merikebu za biashara; 

Huleta chakula chake kutoka mbali.

[15]Tena huamka, kabla haujaisha usiku; 

Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; 

Na wajakazi wake sehemu zao.

[16]Huangalia shamba, akalinunua; 

Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

[17]Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; 

Hutia mikono yake nguvu.

[18]Huona kama bidhaa yake ina faida; 

Taa yake haizimiki usiku.

[19]Hutia mikono yake katika kusokota; 

Na mikono yake huishika pia.


3: MAMA

Pia mke ile uwe kamili, basi hutakiwi kuwa mwanamke tu, bali unatakiwa kuwa mama. 

👉Si kila mwamke anaweza kuwa mama, bali mke mwema ni mama. 

👉Nafasi yake kama mama inaonekana pale anapowalea watoto katika njia salama, anauwezo wa kuwaonya pale wanapikosea na pia kuwapongeza pale wanapofanya vizuri. 

👉Mama huwa macho kutoruhusu ubaya kuingia ndani ya nyumba yake, 

👉Humlinda, humtetea mumewe na kumuombea


4:MWENZI WA NDOA

Pia mke ili uwe kamili, basi ni lazima binti ujiandae katika ndoa yako, uwe mtu ambaye atamuenzi mumewe, katika upendo, faraja, na pia kumtimizia mahitaji mume wake kama anavyohitaji. 

👉Binti lazima ufahamu, ndoa nyingi huwa zinafunjika, kwa sababu moja nyeti ambayo ni kushindwa kuwa mwenzi kati ya mume au mke kwa mwenzake. 

👉Hapa ninazungumza kwa habari ya TENDO LA NDOA,.... Hili nalo humfanya mwanamke kupendwa na mumewe, kufurahiwa na hata kuheshimiwa sana na mumewe. 

👉Hapa ndipo binti kwenye ndoa yako, hutatakiwa kufanya tofauti maana, Mungu ameumba namna hii kama njia ya watu kuzaliwa na wanandoa kufurahiana kwa furaha kuu. 

👉Ni lazima ujue kuwa hata kama mume wako atakuwa mkali sana, hatulii, mgomvi,,,, basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kutulia katika ndoa na kukuheshime sana pale tu utakapokuwa na mahusiano mazuri na yeye kwenye tendo la ndoa


5: MPISHI,

Pia ni lazima ujue kuwa mpishi mwenye uwezo wa kupika chakula kizuri na kitamu

👉Kuna visa vingi na malalamiko mengi kwenye ndoa, pale ambapo mwanaume anakuwa hali chakula cha nyumbani kwake na hata kusababisha mambo mengine. 

👉Huona ni heli akanunue chakula hotelini kuliko nyumbani kwake. Mh NI HATARI

👉Ni lazima ujue kuwa moja ya sababu ya ndoa ni mume kupata msaidizi..... Sasa kama msaidizi hajui hata kupika chakula kizuri kwa ajili ya mumewe, basi hata wewe unaweza kujiuliza, anaitwa msaidizi wa kusaidia nini? 

  đź‘ŹSina maana kuwa neno msaidizi linasimama kwenye chakula tu, HAPANA, ila upishi ni moja ya vitu unavyotakiwa kujua jinsi ya kumuandalia.  

      Siri nyeti ni hii👇

Ukiwa kwenye ndoa yako, hata kama kuna mfanya kazi wa ndani, anayeandaa chakula,... Jitahidi sana chakula cha mumeo ukiandae wewe kwa uzuri kabisa, na pia mnawishe mikono wewe mwenyewe, mlishe kwa kiasi cha awali ikibidi, pia penda sana kula pamoja na mumeo pamoja. 

👉Hii humfanya mwanaume kukupenda na kukuamini sana. 

Lakini hatari ni kwa mabinti wa leo wasioelewa haya mambo.... Yani unakuta chakula alichokula mumewe hakijui, hajaandaa yeye, na wakati mwingine hata wakati mumewe anakula yeye hayupo, kabisa yupo zake kwa wale anaowaita mashoga zake. 

👉Jitahidi kumfanya mumeo ajione kuwa ana Bahati kuwa na wewe, aamini kuwa hajakosea kukuoa wewe na atakuwa anakufurahia

  Utakuta hata kama kuna siku haupo kidogo, utashangaa anakupigia hata simu akitamani uwe naye pamoja mle wote chakula. 

6: MTUNZA MJI

Wanaume hupenda kuoa kwa sababu nyingi walizonazo wao, na wengine hupenda kuoa,, pamoja na sababu yake fulani lakini pia ni kwa lengo la kuwa na heshima au kutengeneza heshima ya nyumba. 

👉Kuna mambo fulani mwanaume hawezi kufanya mpaka awe ameoa. 

👉Kuna baadhi ya majukumu ya kanisa, kijana haruhusiwi kuyafanya mpaka awe ameoa. 

👉Kwahiyo kuoa kunajenga heshima ya mtu, na hasa pale anapopata mki kamili anayejua kutunza nyumba yao

👉Kuna familia mwanaume anashindwa hata kuja na rafiki zake nyumbani kwasababu anahofia pengine atakuta mazingira hayajakaa vizuri, katika hali ya usafi, mpangilia mzuri. N. K

👉Kuna nyumba unaweza ukaingia, ukashangaa viatu vipo pamoja na vyombo vya kupikia, mara unaina vijiko vipo kwenye makochi, au unaona ndo ya maji ya kunywa imefunguliwa na mfuniko wake upo chini wala hakuna anayeufuatili. 


7: MSAFI

pia mke ni lazima uwe msafi, uwe unafua mavazi yako na ya mumeo. Uwe mrembo, ambaye huruhusu hata nywele zako zikae shagarabagara, zimefumuka, chafu, utakuta hata unapopika hujafunika kichwa, nywele inadondokea chakula na mambo kama hayo. 

👉Binti ni lazima ujifunze kuwa msafi na iwe desturi yako muda wote. Hii itakuwa inamvutia sana mumewako, na ataona kuwa na wewe ni kuwa na vyote. 

8: MKARIBISHAJI

Hili hata halihitaji elimu kubwa ili kulielewa.

Japo huwa ni tatizo linapifika kwa wanawake wasiojua jinsi ya kuwa kamili.

  Mke mkaribishaji, anafanya hata jamii kumpenda nq kumfurahia

👉Ukiona mke si mkaribisha, basi kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuwa na sifa hizi👇

👉Mchoyo

👉Mbinafsi

👉Ana chuki

👉Mvivu

👉Hupenda kujitenga

👉Ana roho ya wivu.

Kwa sifa hizi 6 basi zinauwezo wr kumfanya mke kuwa mke mwema na mkamilifu kwenye ndoa yake, na anaweza kuishi bila kuwa na mgogoro, hata kidogo, atakapokutana na mume mwenye hekima.

Tamani kuwa mke kamili

Mungu akubaaiki sana binti ndani ya Kristo


Taifa Teule Ministry

Mwl / Ev Mathayo Sudai

0744474230 / 0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI