NI DHAMBI KUPENDWA NA DUNIA..

 

NI DHAMBI KUPENDWA NA DUNIA.. 

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu. 

  Karibu katika ujumbe huu mfupi ambao naamini utakuweka kuwa huru kwenye dunia hii. 

😯Kuna watu ambao wameokoka lakini bado wanapewa shida na wale waliopo nje ya pale walipo wao. 

   Kuna mambo ambayo hayapaswi kukusumbua akili, hasa barda ya kujua asili yako. 

👉Haya ni maneno ambayo dhaifu na watu wenye michanganyo huwa hawapendi sana kuyasikia, 

   Lakini ni hivi👇

Unavyokuwa umeokoka na kutembea na Mungu vizuri, basi ni lazima ujue kuwa umejifanya kuwa tofauti na watu wa dunia hii, ambao wengi wao wameshikiria majina ya makanisa na dini zao bila hata kuyajua mapenzi ya Mungu 🙏

Ni lazima, wengi wao watakudharau na kukusengenya na wengine hata kusema kuwa unajifanya wa kiroho sana. 

Hebu soma hapa👇

Yohana 15:20

[20]Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.

Sasa hayo ni maneno ya Yesu mwenyewe alipokuwa anawaasa wanafunzi wake juu ya kile watakachokutana nacho baada ya yeye kuondoka mbele ya macho yao. 

Wewe kama ni mkristo ambaye umelishika na unalishika neno la Mungu, basi ni lazima lishike na hili kwamba walichomfanyia mkombozi wetu, ndicho watakachotufanyia. 

👉Kuna ambao walimkubali, basi wapo pia ambao wameishika kweli ya Mungu watatukubali katika wokovu tulionao

👉Pia kuna kundi kubwa la watu ambao lilimkataa hivyo ni lazima ujue kuwa wapo wengi sana ambao watakudharau, watakutukana, na wengine watakusengenya na wengine watakwambia maneno ya kukudhihaki. 

Hebu usijaribu, Kuyahesabu matukano, na dharau zao, maana watakusononesha na kukufanya usipige hatua nyingine. 

😯Kuba watu wengi huwa wahashindwa kuchukua hatua ambayo ni agizo la Mungu kwa kuwaza kewa watu watawaonaje, au itakuwaje kama watu watawashangaa. 

Kumbuka Mungu anatuagiza kulitenda na lenye kumpendeza MACHONI PAKE 

👉Sasa tuhapohangaika kewapendeza watu na kumuacha Mungu basi jua ni makosa makubwa na hakuna kitu tunacnokifanya. 

Hebu USIOGOPE kumtaja Yesu kwenye maisha yako

👉Usiogope kuwaambia watu kuwa umeokoka. 

Naomba nikwambie jambo moja ambalo pengine hukuwahi kuambiwa. Ni hivi👇

NI DHAMBI KUPENDWA NA DUNIA. 🤔

Mh, 

Yohana 15:18-19

[18]Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.

[19]Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.

Biblia inasema, tungekuwa wa dunia hii basi ulimwengu ungetupendwa. Na mimi leo nakwambia ulimwengu ukikupenda basi ni lazima ukae ujiulize umekosea wapi. 

  NI KOSA KUPENDWA NA DUNIA. 

hatujatumwa kuwapendeza watu, bali kumpendeza Mungu tu, na hivyo kila tutakalo lifanya kwa kumpendeza Mungu,.... Haijalishi ni baya kwa wao, hilo kwetu siyo tatizo na hatuna haja ya kuliona kuwa tatizo. 

Sisi ni taifa la Mungu ambalo tunafanya mapenzi ya Baba yetu bila kutarajia pongezi kutoka kwa mtu. 

Lakini Yesu hakutuacha nw maswali ya kwanini wanatuchukia😁

Yohana 15:21

[21]Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.

Akasema na hapa tena👇

Yohana 16:1-3

[1]Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.

[2]Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.

[3]Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.

KUCHUKIA NA DUNIA KUNATENGENEZA UZIMA KWETU, maana hata Baba yetu alidharauliwa na watu wenye mwili japo alifanya mema na alikuwa na lengo la kuwakomboa wenye mwili haohao

Soma hapa👇

Isaya 53:3

[3]Alidharauliwa na kukataliwa na watu; 

Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; 

Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, 

Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.


SIRI NI HII, ili usisumbuke

Idadi kubwa ya wale watakao kufanyia hayo ni WALE AMBAO WANAINGIA KANISANI NA KUTOKA HUKU WAKIJIITA WAKRISTO HUKU WAKILEA DHAMBI. 

Wale watu wa dini ndiyo wanaojenga idadi kubwa ya maadui kuliko hata, wasiomjua Kristo kabisa.

👏👏👏Mama., Baba, na wewe kijana unayesoma ujumbe huu, nakujulisha siku hii kuwa, 

Mungu anaandaa watu wake saa hii, watu watakaoweza kusimama na jina la YESU bila kuogopa, watu ambao wanajikana wenyewe, watu ambao hawapendi mifumo na starehe za kidunia, wanajeshi katika ulimwengu wa roho.

Lakini ukishindwa kusimama kwenye nafasi yako basi jua UTAIPOTEZA na utakataliwa.



Taifa Teule Ministry 

Mwl/Ev Mathayo Sudai

0744474230 / 0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI