MWANAMKE NI JESHI KUBWA
MWANAMKE NI JESHI KUBWA
🩸Jeshi kubwa, ni jeshi lenye nguvu kuliko majeshi mengine.kiutendaji, ki-msimamo, hata kimbinu pia, Tena Ni jeshi linalotegemewa Sana , ndilo jeshi kubwa.
🩸kwanini tunasema mwanamke Ni jeshi kubwa soma hapa,👇
Yeremia 9:20
[20]Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake,
Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake;
Mkawafundishe binti zenu kuomboleza,
Na kila mmoja jirani yake kulia.
🩸Mwanamke ametajwa kama shujaa wa kuomboleza mbele za Mungu.
na moja kwa moja maombi ndio jiko kuu la mkristo halisi , Ni sawa na Nyumba lazima iwe na jiko, huko jikoni kunatoka chakula,
huko jikoni Kuna Moto,
huko jikoni Kuna vifaa vyote vinavosababisha chakula kikamilike na kuliwa😋.
🩸Mwanamke anafananishwa na jiko ndani ya Nyumba
Na wakati mwingine ulishawahi kusikia watu wakimwita mwanamke Kama JIKO😃.
😇Mfano mwanamume anapo Oa utasikia Amepata Jiko.
kwanini mwanamke anafananishwa na jiko tumeona hapo juu👆
🩸Sasa tutoke mwilini tuje Rohoni
Mwanamke anafananishwa na jiko kuu la mkristo hai ambalo ni MAOMBI, Tena maombi ya kuomboleza🙇 mwanamke ni shujaa sana katika sector hii ya maombi akijitambua.
Mwanamke mwombaji hata mumewe humsifu😃
Ni MTU anayeweza kubadilisha mfumo wa maisha fulani usiofaa, Ni MTU anayeweza kuyageuza mambo mbaya yakawa mazuri
kasome kitabu cha ESTA utaona hayo🙏
🩸Mwanamke anauwezo mkubwa sana wa kuijenga Nyumba yake mwenyewe (yaani familia). Ni mwanaamke muombaji. katika maombi hupata hekima naa busara ya kujiendesha Nyumba yake hata Kama Mumewe hajamjua Mungu bado
Mithali 14:1
[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Sasa itakuwa ni ajabu sana Kama mwanamke asipojitambua kuwa yeye ni nani
🩸Katika kanisa
🩸Katika familia
🩸Katika malezi ya watoto wake na waa wengine pia
🩸 Katika Taifa na Jamii kwa ujumla.
*Mwanamke Anayejitambua na kuitwa Jeshi kubwa lazima awe na sifa zifuatazo*
*📍Anapaswa kulishika Neno la Mungu na kuliishi ndipo ataitwa jeshi kubwa.*
Naweza nikasema mwanamke ambaye hajokoka, halijui neno la Mungu , Wala hajui nafasi yake kwa Mungu asijiite Jeshi kubwa😃.
Kiroho jeshi kubwa haliko hivyo, lipo hivi
Waefeso 6:12-13
[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
[13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Hapo kuna vitu vya msingi sana unapaswa kuwa navyo.;
Dirii ya haki
Ngao ya Imani
Chepeo ya wokovu
Upanga wa Roho Mtakatifu ambao ni Neno la Mungu.
Mwanamke ambaye ni jeshi kubwa amekomaa katika mambo hayo.
*📍Kuukomboa wakati*
Waefeso 5:15-17
[15]Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
[16]mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
[17]Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Mwanamke Anayejitambua lazima awe na ratiba yake Binafsi yenye manufaa Rohoni na mwilini , namaanisha uaminifu katika kuutumia Muda wake vizuri bila kupoteza Muda katika mambo yasiyo na umuhimu.
Kama Mungu anavyoshika maagano na kuyatimiza Basi na wewe mwanamke uwe na hekima katika Kuukomboa wakati katika mambo yako itakuwa afya kwa Mungu, familia hata katika ukuaji waa mafanikio yako.
*📍Kuwa kielelezo kwa kizuri kwa Jamii*
Mwanamke amchaye Bwana ndiye husifiwa Sana
Mithali 31:30
[30]Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
Soma
Yakobo 4 :1 - 4.
🩸Pia Mwanamke jeshi kubwa anajua kuvaa vizuri ( Smart )
🩸Anavaa Nguo za Heshima .
🩸Hujiweka katika namna iliyo mzuri 💃
🩸Ana hekima katika usemi wake , mwenye busara😇.
🩸 Siyo mgomvi anajua kuji -control
🩸Si mtu wa hasira ni mtu anayeleta tabasamu mbele ya familia yake.
Mweee mwanamke akiwa na sifa njema ni raha sana🥳🥳🥰
*📍Kuongoza Nyumba yake ipasavyo( familia)*
mwanamke jeshi kubwa kuhakikisha ustawi mzuri waNdoa yake kiroho na kimwili*
Mithali 14:1-3
[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
[2]Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA;
Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.
[3]Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi,
Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.
*📍Kuwa na Juhudi*
Mwanamke Jeshi kubwa siyo mvivu,
- Anajua kujishughulisha na shughuli za uzalishaji na kukuingizia kipato chake ( hufanya kazi siyo mama wa nyumbani tu.)
-Anajua kuilisha familia yake bila uvivu.
-Anajua kuisafisha Nyumba yake na kuiweka katika hali ya usafi muda wote,
-bila kusahau chumbani kwake ,jikoni na msalani😁 wanawake wengi wavivu maeneo haya huwashinda katika ku-maintain usafi vizuri
- Mwanamke ni msafi wa mwili pamoja na mavazi yake , ya watoto wake na Mumewe,
📍Mwanamke, Nguo za Mume wako fua mwenyewe usimwachie dada wa kazi 📌
Soma : Mithali 31 : 10,15, 30.
*📍Kuwa Muombaji*
Mwanamke anayependa maombi huyo ni jeshi kubwa ambalo hata Mungu analitegemea Sana .
Mwana Mume Anayejitambua hupenda mwanamke mwombaji , anayemcha Mungu, na Mwenye hekima ya Mungu, msikivu, anayejua kunyenyekea kwake na kwa Mungu.🙏
Yeremia 9:17-18
[17]BWANA wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje;
[18]na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
MATHAYO 21:28-31.
🔥📌Mwanamke Kama huna sifa hizi hata moja usijiite Jeshi kubwa. Jiulize kwanza kwanini mwanamke ndiye anaitwaa jeshi kubwa na so mwanamume iko namna hapo, yeye Mwanaamume anaitwa Kichwa Cha familia, Kama Kristo ndani ya kanisa na anahakikisha anafanya majukumu yake ya kuitwa Kichwa.
*Note;✍️*
Sijasema mwanamume asiwe Muombaji , Mwenye juhudi, Mwenye Kuukomboa wakati , Mwenye Kumcha Mungu na mengine hapana, Bali kila mmoja Mwanamke / Mwanamume asimame kwa nafasi yake kama kiungo ndani ya mwili/ kanisa ili kuukamilisha mwili wa Kristo.
Tafakari na uchukue hatua itakayokuletea mabadiliko mazuri kimwili naa kiroho.
*SEMA MIMI NI JESHI KUBWA🙌😁*
*MUNGU AKUBARIKI SANA🙏*
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl. Beata Silwimba
0620507212
Maoni
Chapisha Maoni