Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2023

MOYO NI NINI KIBIBLIA

Picha
                                MOYO NI NINI KIBIBLIA Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, nimeona watu mbalimbali wamejaribu kutoa maana na uelewa wao juu ya kile wanachokiita moyo.      Mungu awabariki sana kwa michango yote mliyotoa         Hebu tuanze hivi👇      👉 Wanadamu tuna moyo ambao ni tofauti na kiungo cha mwili kinachosukuma damu kupitia miili yetu.  👉Tunauchukulia moyo huo kuwa chanzo cha hisia zetu kama vile upendo, huruma, uaminifu, au huzuni. Swali Je Biblia inasema mioyo yetu ni nini? Biblia inafafanua mioyo yetu katika mistari mingi, sio tu katika mstari mmoja na tukitumia mstari mmoja basi ni rahisi sana kukosa maana sahihi ya moyo ndani ya Biblia.  🙏Nadhani wote tunajua kuwa Mungu alituumba na sehemu tatu, yaani  1:roho, 2: nafsi na  3: mwili.  👉Kwahiyo ni lazima tujue moyo upo katika sehemu gani?  Biblia in...

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA

Picha
          TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA DHAMBI  ni uasi wa sheria ya MUNGU. Ni matendo yote yaliyo chukizo kwa MUNGU. 1 Yohana 3:4  " Kila mtu afanyaye dhambi,afanya uasi maana dhambi ni uasi." UOVU Ni dhambi iliyokomaa na kuwa ya kujirudiarudia kwa mhusika 👉Hii ni pale ambapo mtu anakuwa ameifanya dhambi kuwa desturi yake, na hutenda mara kwa mara.  Isaya 59:2  " lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia." MAKOSA Hii inahusisha utendaji wa mambo mabaya/ yasiyofaa kwa kukusudia au kutokukusudia, kwa kujua au kwa kutokujua.   👉 Lakini kwenye maisha ya kawaida si kila kosa ni dhambi ila dhambi zote ni makosa  Maneno yote matatu yanabeba kile na yana uwezo wa kumfanya mtu kuwa mbali na Mungu.  na husamehewa kwa kutubu tu! wala si kutenda wema. ni lazima utubu ndipo uanze kufanya wema 👍Mtu akitubia DHAMBI zake na kuacha kabisa anasamehewa. 👍Mtu...

BWANA ATAKUTHIBITISHA

Picha
                              BWANA ATAKUTHIBITISHA Yeremia 33:2-3 [ 2]BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi, [3]Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Mungu anasema tusipozimia mioyo katika kutenda mema tutaipokea Taji ya uzima wa milele. Na kabla ya Taji tutapokea mema mara mia duniani Kisha uzima wa milele  Mathayo 19:29 Kumbe Kama tunapokea duniani mara Mia ni wazi kwamba yapo mambo mengi Sana mazuri ambayo ni haki yetu kupokea. 😃Nataka nikuambie Jambo moja zuri Sana mpendwa wangu, ikiwa umekaa katika Msatari wa Mungu na  kuendelea kumpenda Mungu na kumtegemea yeye uwe na uhakika kwamba baraka zote tunazozihitaji kwenye maisha yetu lazima tuzimiliki kwasababu zimewekwa kwaaajili yetu haleluya🙌 Kuna watu wananielewa hapa wanaweza wakamshuhudia Mungu🙌 Lile unaloona kwamba  ni zito  unajiuli...

WENYE DHAMBI WAKIKUSHAWISHI, KATAA

Picha
          WENYE DHAMBI WAKIKUSHAWISHI, KATAA Mithali 1:10-15 [ 10]Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi,  Wewe usikubali. [11]Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi,  Na tuvizie ili kumwaga damu;  Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; [12]Tuwameze hai kama kuzimu,  Na wazima, kama wao washukao shimoni. [13]Tutapata mali yote ya thamani,  Tutazijaza nyumba zetu mateka. [14]Wewe utashirikiana nasi;  [15]Mwanangu, usiende njiani pamoja nao;  Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao. Tutakuwa na vitu vyote shirika. Bwana Yesu asifiwe. ni Jumapili njema kabisa, na leo ninaiita Jumapili ya kujitenga, kama tunavyoona hapo kwenye vifungu vyetu vya maandiko.  Biblia inatuambia wenye dhambi WAKIKUSHAWISHI kwa ajili ya kuambatana nao ili kufanya uovu fulani basi usikubali  👉watakapokushawishi ili mmsengenye mtu fulani, KATAA 👉wakikushawishi ili kuvunja nyumba ya mtu, KATAA 👉wakikushawishi ili kuua na kujipatia mali, KATAA  wa...

UHUSIANO WA JARIBU NA KUSUDI LA MUNGU MAISHANI MWAKO

Picha
  UHUSIANO WA JARIBU NA KUSUDI LA MUNGU MAISHANI MWAKO *Waamuzi 16:15* [15]Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. Hayo yalikuwa ni maneno ya mwanamke Delila yaliyojaa ushawishi mkubwa / mbaya sana kwa Mtumishi wa Mungu Samsoni Ambao ulikuja kumfanya Samsoni kupoteza nguvu zake na mwisho wake haukuwa mzuri Kama tunavyojua Samsoni alizaliwa katika familia ya Mzee Manoa.  Kabla ya kuzaliwa kwake Mungu alimkusudia aje azaliwe kwa kusudi la kuwapigania Wana wa Israeli dhidi ya Wale wafilisti / watu wabaya waliokuwa wanaitesa Israeli kwa muda mrefu na kuwauwa watu wa Mungu wengi. Hivyo Samsoni alizaliwa kwa kusudi maalumu kabisa Kama tunavyoona Yohana mbatizaji alivyo zaliwa kwa kusudi maalumu la kuja kuitengeneza njia ya Kristo na kuyanyosha mapito yake. Samsoni alizaliwa Kama mnadhiri wa Bwana yaani mtu aliyetengwa na kuwekwa wakfu kwaajili ya kazi ya Mungu. Mama...

KUISHINDA DHAMBI

Picha
                                 KUISHINDA DHAMBI *Mwanzo 4:7* [7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Bwana Mungu akiliwa anazungumza na Kaini mzaliwa wa kwanza wa Adamu na Hawa, kwa habari ya ndugu yake Habili. Kaini alikuwa mkulima, na Habili alikuwa Mfugaji ,Basi wakati wa kumtolea Mungu kila mtu akatoa kulingana na kile anachomiliki, Habili akatoa wanyama walionona mbele za Bwana Kama sadaka yenye utukufu. Lakini Kaini alitoa mazao ambayo hayakumridhisha Mungu, Mungu akaona Kaini amepungua katika Utoaji wake( alitoa sadaka isiyo faa) .Hivyo Mungu akambariki Sana Habili kuliko Kaini. Kaini akamuonea wivu mwenzake kwa kuwa amebarikiwa, akaghathibika na kupanga kumuua ndugu yake, Ndipo Mungu anamuuliza Kaini Kama ungetenda mema usingepata kibali??? Usipotenda mema lazima utaingia kwenye mtego wa dhambi, ...