MOYO NI NINI KIBIBLIA


                                MOYO NI NINI KIBIBLIA

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, nimeona watu mbalimbali wamejaribu kutoa maana na uelewa wao juu ya kile wanachokiita moyo.

     Mungu awabariki sana kwa michango yote mliyotoa

       Hebu tuanze hivi👇

     👉 Wanadamu tuna moyo ambao ni tofauti na kiungo cha mwili kinachosukuma damu kupitia miili yetu. 

👉Tunauchukulia moyo huo kuwa chanzo cha hisia zetu kama vile upendo, huruma, uaminifu, au huzuni.

Swali

Je Biblia inasema mioyo yetu ni nini?

Biblia inafafanua mioyo yetu katika mistari mingi, sio tu katika mstari mmoja na tukitumia mstari mmoja basi ni rahisi sana kukosa maana sahihi ya moyo ndani ya Biblia. 

🙏Nadhani wote tunajua kuwa Mungu alituumba na sehemu tatu, yaani 

1:roho,

2: nafsi na 

3: mwili. 

👉Kwahiyo ni lazima tujue moyo upo katika sehemu gani? 

Biblia inapozungumzia moyo inahusisha vitu vyote vitatu ambazo ndizo zinajenga utu wa mtu. 

👉unaposikia neno moyo wakati mwingine inabeba maana ya kiini cha kitu, 

Kwamfano 

Moyo wa bahari= kiini cha bahari

Moyo wa mtu = kiini yaani pale katikati

 Hivyo basi, mioyo yetu ni muundo wa vitu vyote vitatu yaani 👇

 1: Akili zetu( fikra),( Mind) 
2:  Hisia, ( Emotion) 
3: Mapenzi( utashi) au WILL, katika lugha ya kiingereza- 
pamoja na sehemu muhimu zaidi ya roho yetu - yaani
dhamiri yetu.

👉 Hebu tuangalie baadhi ya mistari muhimu inayofunua hili.

1. Mathayo 9:4

Naye Yesu, akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza mabaya mioyoni mwenu?

Kufikiri ni shughuli ya akili( fikra) , lakini Bwana Yesu aliwauliza waandishi kwa nini walikuwa wanawaza mioyoni mwao. Hii inaonyesha kwamba akili ni sehemu ya moyo wetu.

2. Matendo ya Mitume 11:23

[23]Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.

Kusudi ni kuamua kwa dhati kufanya jambo, ambalo ni utekelezaji wa mapenzi yetu. Kwa hivyo mstari huu unaonyesha kuwa mapenzi yetu ni sehemu ya moyo wetu.

3. : Yohana 16:22

[22]Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.

Kushangilia kunahusiana na hisia zetu, lakini hapa tunaona kwamba moyo wetu unashangilia. Hii inatuonyesha kuwa hisia yetu pia ni sehemu ya moyo wetu.

4. Waebrania 10:22

[22]na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.

Kunyunyiziwa mioyo yetu kutoka kwa dhamiri mbaya kunaonyesha kwamba dhamiri yetu pia ni sehemu ya moyo wetu.

Hili linathibitishwa zaidi kwa maneno haya

👉 “1 Yohana 3:20-21

[20]ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.[21]Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;

 mstari huu pia unaonyesha wazi kwamba dhamiri yetu ni sehemu ya moyo wetu.

Mungu akubariki sana


Taifa Teule Ministry 
Mwl / Ev Mathayo Sudai 
0744474230 /0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI