BWANA ATAKUTHIBITISHA
BWANA ATAKUTHIBITISHA
Yeremia 33:2-3
[3]Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
Mungu anasema tusipozimia mioyo katika kutenda mema tutaipokea Taji ya uzima wa milele. Na kabla ya Taji tutapokea mema mara mia duniani Kisha uzima wa milele Mathayo 19:29
Kumbe Kama tunapokea duniani mara Mia ni wazi kwamba yapo mambo mengi Sana mazuri ambayo ni haki yetu kupokea.
😃Nataka nikuambie Jambo moja zuri Sana mpendwa wangu, ikiwa umekaa katika Msatari wa Mungu na kuendelea kumpenda Mungu na kumtegemea yeye uwe na uhakika kwamba baraka zote tunazozihitaji kwenye maisha yetu lazima tuzimiliki kwasababu zimewekwa kwaaajili yetu haleluya🙌 Kuna watu wananielewa hapa wanaweza wakamshuhudia Mungu🙌
Lile unaloona kwamba ni zito unajiuliza sijui itakuwaje, sijui utafanyaaje?. Umekuwa na maswali mengi kichwani mwako mpaka unahisi Mungu hakusikii, Ooooh Sikio la Mungu ni jepesi Sana kusikia sauti ya kila aombaye kwa haki na kwa imani.
maana aombaye kwa haki( katika utakatifu) hupokea, hivyo kwanza tafuta haki / Imani, utapokea.
Mungu wetu ni Mungu aliyeviumba vitu vyote na ndiye Mungu anayetenda vyote. Hivyo anajua kila kitu kinachokuhusu wewe.
Anajua kuwa unahitaji Mume mzuri ambaye ni baba Bora
Anakujua kuwa unahitaji Mke mwema wa mithali 31 ( A virtuous lady) who can find, but God into you🙌
yeye aliyewaumba watu wote anajua ni yupi anayeweza kuja kukukamilisha pale ulipopungua/ kwenye hitaji lako.
Wewe uliyepoteza afya kwenye mwili wako Bwana akajitukuze ndani yako uwe mzima kwa Jina la Yesu
Wewe unayehitaji mtoto, Bwana anakwenda kukufanyia kicheko kwenye ndoa yako.
Pia Mungu anakujua kwamba unahitaji Amani ya moyo, unahitaji faraja, unahitaji uchumi mzuri.
Mungu anakujua Nia ya moyo wako na pengine ukiingia kuomba unalia kweli unahitaji Mungu akutumie kwa viwango vikubwa katika huduma yako/ unalia Mungu ajibu hitaji lako, yes God is on control just pray and relax, unakwenda kupokea hitaji lako maana aliyesema ni Mungu mwenyewe aliye ASILI ya vitu vyote, na aliye ASILI ya mema yote.
Mungu anakwenda kukudhibitisha kuwa wewe ni Mwana wake🙌
Na kwasababu hiyo hata laana na mabaya yote si sehemu ya maisha yetu,
Kuna namna huoni kubarikiwa kwenye mambo yako angalia kwanza njia zako usikae kumlaumu Mungu au mtu kwamba yamkini ndiye amezuwia baraka zako no.
Mungu anawapenda watu wote wanaopenda yeye.
Mithali 8:17-21
Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
[18]Utajiri na heshima ziko kwangu,
Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
[19]Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi,
Na faida yangu hupita fedha iliyo teule.
[20]Natembea katika njia ya haki,
Katikati ya mapito ya hukumu.
[21]Niwarithishe mali wale wanipendao,
Tena nipate kuzijaza hazina zao.
Huo wote ni urithi wa watu wanaopenda Mungu.
*Wewe umerithi nini kutoka kwa Bwana??🤔😁*
Usiogope, usiwe na mashaka, Usikate tamaa ,usiangalie ukubwa wa hitaji lako, usipime mazingira ya kile unachohitaji ukafikiri Huwezi kufika unakotarajia kwenda, utafika kwa msaada wa Mungu.
Ninakuambia hivo kwasababu yamkini na Mimi nilikuwa Kama wewe Leo yapo Mambo nilikuwa namuuliza Mungu itakuwaje, sasaa nafanyaje, Mungu natokaje hapa, Ila Mungu alionekana pale niliposimama kumwita Yesremia 33:3. Hakika nimeona Mungu kwa ukubwa Sana na nitazidi kumuona katika makubwa zaidi.
Yesu ni mzuri Sana ukimuelewa,🙏
Mungu akubariki Sana.
*TUOMBE*
JEHOVA SHAMA ,KIMBILIO LETU, MSAADA WETU UTAKAOONEKANA WAKATI WA MATESO, WEWE NI BABA YETU PEKEYEKO WEWE NDIWE MUNGU WA KWELI TENA NI NGOME YETU POKEA SIFA NA UTUKUFU YESU MAANA UMEKUWA MWEMA KWETU ZAIDI YA TARAJIO YESU.
Zaburi 46:1-2,7
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
[2]Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
[7]BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
KAA NASI MUNGU ILI TUZIDI KUSHUHUDIA NA KUUTANGAZA WEMA WAKO KWA MATAIFA YOTE,
TUPE MIOYO YA UTULIVU NA USTAHIMILIVU TUNAPOKUTANA NA CHANGAMOTO KUBWA, YESU UKAHUSIKE MWENYEWE KWENYE MAISHA YETU YOTE.
BARIKI MADHABAHU HII BWANA KWA UTUKUFU WA JINA LAKO YESU ILI IKANENE MEMA KWA KILA MMOJA WETU AKAONE FAIDA YA KUWA HAPA.
FAMILIA, KAZI, BIASHARA HUDUMA ZETU NA WATOTO WETU BWANA UKATUTHIBITISHE WEWE KWA UTUKUFU WAKO . BARIKI KAZI ZA MIKONO YETU UKAZILINDE ZISIHARIBIWE NA MWOVU KATIKA JINA LA YESU.
BABA TUNAKUSHUKURU ,TUNAKUSIFU, TUNAKUABUDU ,TUNAKUTUKUZA NA KUKUINUA JINABLAKO KWAKUWA WEWE NI MWEMA KWA MAANA FADHILI ZAKO NI ZA MILELE AMEN.
Mwl Beata
0742442164.
Maoni
Chapisha Maoni