KUISHINDA DHAMBI
KUISHINDA DHAMBI
*Mwanzo 4:7*
[7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Bwana Mungu akiliwa anazungumza na Kaini mzaliwa wa kwanza wa Adamu na Hawa, kwa habari ya ndugu yake Habili.
Kaini alikuwa mkulima, na Habili alikuwa Mfugaji ,Basi wakati wa kumtolea Mungu kila mtu akatoa kulingana na kile anachomiliki, Habili akatoa wanyama walionona mbele za Bwana Kama sadaka yenye utukufu.
Lakini Kaini alitoa mazao ambayo hayakumridhisha Mungu, Mungu akaona Kaini amepungua katika Utoaji wake( alitoa sadaka isiyo faa) .Hivyo Mungu akambariki Sana Habili kuliko Kaini. Kaini akamuonea wivu mwenzake kwa kuwa amebarikiwa, akaghathibika na kupanga kumuua ndugu yake,
Ndipo Mungu anamuuliza Kaini Kama ungetenda mema usingepata kibali??? Usipotenda mema lazima utaingia kwenye mtego wa dhambi, dhambi ikikufuatia hakikisha unaishinda.
Ukitenda vema utapata kibali Kama ni Baraka zote zitakufuata
Soma Kumbukumbu la Torati 28.
Lengo la somo hili natamani tujue kuishinda dhambi,
Ukiendelea kusoma hicho kitabu Cha mwanzo 4 Utaona Kaini hakuweza kuishinda dhambi iliyokuwa imemfuatia, Laana ya kutoa sadaka isiyofaa kwa Mungu , Wivu ,Hasira, na Ghadhabu vikamfanya akaamuua ndugu yake (Habili). Hatimaye Mungu alikuja kumuua Kaini pia kwasababu ya machukizo aliyoyafanya.
*Warumi 6:23*
[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Wengine hudharau kutoa sadaka, akidhani anawapa watu fulani wale, wakati sadaka ni agizo la Mungu mwenyewe tangu zamani ilikuwa ikitolewa, na Mungu anaitakabali.
Heri wewe unayetoa sadaka kwa moyo safi.
Usipotoa sadaka unalaaniwa na Mungu mwenyewe Wala si mchungaji wako.
*Ni Mara ngapi umeishinda dhambi? au dhambi ndo inakushinda!!?*
Mali unazo / fedha unazo lakini kutoa sadaka ni mtihani mgumu kwako, hujui hizo fedha ulizonazo ni Mungu alikupa, hivyo anauwezo wa kuziondoa muda wowote ukabaki Kama ulivyo au akakuondoa wewe na Mali zako wakala wengine!, na hiyo ndiyo Laana yenyewe. Niwekee hazina yako mbinguni
Ni Mara ngapi umeona wivu kwa mwenzako kisa amefanikiwa kuliko wewe, tenda wema nawe utabarikiwa acha kuwa na wivu wa hasara usio na faida
Mwenzio /Rafiki yako amepata kazi unampa hongera kumbe moyoni unaumia,
Mwenzio ameoa / Ameolewa unamuonea wivu, hujui kwamba ukimwombea mema nawewe Bwana atakubariki!, na utapata wa kufanana na wewe.
Ni Mara ngapi umekwazwa na ukapata hasira ikakupelekea kuwatukana watu /ukawajibu watu vibaya. Mwingine akipata hasira hata chakula Hali siku hiyo😃🙌
Na mwingine kwa sababu ya hasira wamewauwa ndugu zao na rafiki zao.
*Je ukiwa na hasira huwa unafanya nini?*
*Waefeso 4:26*
[26]Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;
😃Kuna mtu akikasirishwa na mtu mmoja anamchukia kila anayekuja mbele yake, usiwe mtu wa kukasirika kupita kiasi itakuletea madhara yasiyopona.
Ni mara ngapi umeenda mahali umekuta wanamsengenya mtu nawe ukaanza kuchangia point😃
Mfano pale kazini kwako Kuna boss hatendi haki au shuleni / chuoni Kuna mwalimu hafundishi vizuri ( yaaani haeleweki) huwa unafanyajee ukikutana na hali Kama hizo na unakuta wanaozungumzia hayo ni marafiki zako mlioshibana Sana.??
Una heri wewe ambaye ukikutana na hali hiyo huwa unachukua jukumu la kuondoka eneo hilo ili ikiwezekana usisikie kabisa mazungimzo yao.
Kijana ni Mara ngapi umeingia kwenye mtego wa Uzinzi na ukatoka salama? Au ndo ulijilegeza ukashituka umeshazini🤔?
*Mithali 6:32*
[32]Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Watu wengi hushindwa kujilinda nafsi zao wanapokutana na hali Kama hizi hata waliookoka🤔, sababu ya haya kutokea ni kukosa nguvu ya Mungu ya kuishinda dhambi, ( nguvu ya Roho Mtakatifu)
Tafuta nguvu ya Mungu ikusaidie kushinda dhambi, Soma Neno la Mungu , Funga na Uombe sana, Ishi kwa utulivu na hekima.
Shinda dhambi ya Ulevi,
Shinda dhambi ya uzinzi
Shinda dhambi ya Uongo na masengenyo
Shinda Roho ya Wivu mbaya na Uchonganishi.
Shinda Roho ya hasira kupitiliza
Shinda Roho ya kiburi na kuwadharau wengine.
Je ukitenda vema hutapata kibali!??
Mungu atusaidie, tukiishi kwa kuishinda dhambi tutakuwa ni watu ambao tunamfanya Mungu ajivunie sisi Kama alivyojivunia kwa mtumishi wake Ayubu💪.
*TUOMBE*
Ee Bwana Mungu Mwenye nguvu na uweza ,tunakila sababu ya kukushukuru kwa ukarimu wote uliotutendea.
Umekuwa mwema kwetu kila wakati Wala hujawahi kutuacha Yesu🙏
Umetulinda dhidi ya hila za Shetani, Ajali, Mauti na Magonjwa, umetuweka kuwa salama kwa Neema yako Kristo.
Si kwasababu hatuna dhambi hapana.
1 Yohana 1:8
[8]Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
Tunaomba Rehema zako Yesu uturehemu kwa sababu ya makosa yetu yote tuliyokukosea Mungu, uyafute kwa damu yaako takatifu na utujalie kuishi kwa Utakatifu.
Zaidi Sana tunajikabidhi kwako Mungu hatuna Baba mwingine ila wewe tu, Tunaomba nguvu yako ya kushinda dhambi ili tusiwe watumwa wa dhambi.
Bariki kazi za mikono yetu, wanafunzi mashuleni ukawape kufanikiwa kwenye masomo yao katika Jina la Yesu.
Wewe ni Mungu unastahili sifa Heshima na utukufu Amina.
Mungu akubariki Sana👏
Taifa Teule Ministry🙌.
Maoni
Chapisha Maoni