WENYE DHAMBI WAKIKUSHAWISHI, KATAA
WENYE DHAMBI WAKIKUSHAWISHI, KATAA
Mithali 1:10-15
Wewe usikubali.
[11]Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi,
Na tuvizie ili kumwaga damu;
Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;
[12]Tuwameze hai kama kuzimu,
Na wazima, kama wao washukao shimoni.
[13]Tutapata mali yote ya thamani,
Tutazijaza nyumba zetu mateka.
[14]Wewe utashirikiana nasi;
[15]Mwanangu, usiende njiani pamoja nao;
Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
Bwana Yesu asifiwe. ni Jumapili njema kabisa, na leo ninaiita Jumapili ya kujitenga, kama tunavyoona hapo kwenye vifungu vyetu vya maandiko.
Biblia inatuambia wenye dhambi WAKIKUSHAWISHI kwa ajili ya kuambatana nao ili kufanya uovu fulani basi usikubali
👉wakikushawishi ili kuvunja nyumba ya mtu, KATAA
👉wakikushawishi ili kuua na kujipatia mali, KATAA
wakikushawishi ili kufanya uzinzi, KATAA
wakikushawishi ili kwenda kulewa pombe, KATAA.
Kwasababu hizo ni njia za hao waendao katika uovu na miguu yao vinafanya haraka kupata mali zisizo halali.
na sisi leo tunakumbushwa ni lazima tujitenge na vishawishi na uovu kama huo, jitenge na wale wayatendayo mambo kama hayo maana ni udhalimu mbele za Mungu.
👉sikuhizi wengi huwa wanaanguka kwenye dhambi kwasababu walikubali kuwafuata rafiki zao pale walipowashawishi kufanya dhambi.
Mimi na wewe leo tukatae kushawishika ili kumkosea Mungu wetu.
tuwe watu wa haki mbele za Mungu na ndipo baraka za Mungu zitakapotujilia siyo kama wale waendao katika uovu.
Zaburi 1:1-4
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
[2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
[3]Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
[4]Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
* TUOMBE *
Mwenyezi Mungu muweza wa yote, asubuhi hii ya leo mbele zako tunasogea watoto wako Tunaomba neema yako na nguvu yako iwe pamoja nasi ili tukupendeze katika njia zetu zote. utupe nguvu ya kushinda vishawishi kutoka kwa mwovu shetani na kwa waendao katika uovu.
Asante Bwana kwa ukuu wako nasi katika jina la YESU tunajitenga na uovu wote na vishawishi vyake vyote kwa mamlaka ya jina la Yesu. AMINA
Taifa Teule Ministry
Mwl Beata Silwimba
0742442164 / 0620507212
Maoni
Chapisha Maoni