UHUSIANO WA JARIBU NA KUSUDI LA MUNGU MAISHANI MWAKO
UHUSIANO WA JARIBU NA KUSUDI LA MUNGU MAISHANI MWAKO
*Waamuzi 16:15*
[15]Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi.
Hayo yalikuwa ni maneno ya mwanamke Delila yaliyojaa ushawishi mkubwa / mbaya sana kwa Mtumishi wa Mungu Samsoni Ambao ulikuja kumfanya Samsoni kupoteza nguvu zake na mwisho wake haukuwa mzuri
Kama tunavyojua Samsoni alizaliwa katika familia ya Mzee Manoa.
Kabla ya kuzaliwa kwake Mungu alimkusudia aje azaliwe kwa kusudi la kuwapigania Wana wa Israeli dhidi ya Wale wafilisti / watu wabaya waliokuwa wanaitesa Israeli kwa muda mrefu na kuwauwa watu wa Mungu wengi.
Hivyo Samsoni alizaliwa kwa kusudi maalumu kabisa Kama tunavyoona Yohana mbatizaji alivyo zaliwa kwa kusudi maalumu la kuja kuitengeneza njia ya Kristo na kuyanyosha mapito yake.
Samsoni alizaliwa Kama mnadhiri wa Bwana yaani mtu aliyetengwa na kuwekwa wakfu kwaajili ya kazi ya Mungu.
Mama yake Samsoni alipobeba mimba Mungu alimzuwia hata kutumia vitu vyenye chachu/ mvinyo kiasi kwamba vingeweza kumnajisi mtoto aliyepo tumboni maana alikuwa kwa kusudi maalumu la kuitimiza kazi ya Mungu aliyoumbwa kwayo.
Mungu akaweka nguvu ya ajabu Sana ndani ya Samsoni ambayo haikuwa ya kawaida kabisa.
Ndiyo ilikuja kumsaidia kuwapiga wafilisti na Simba wakali, kusudi kuwatetea Israeli watu wa Mungu
Mungu akampa miiko mama yake kwamba samsoni asinyolewe nywele zake kamwe, na afungwe vifundo Saba vya nywele zake ishara ya connection ya Samsoni na nguvu za Mungu ( yaaani nguvu za Roho Mtakatifu.)
Samsoni alifanyika Msaada mkubwa sana kwa Wana wa Israeli kwa muda wa miaka 20 akawauwa wafilisti wengi Sana na Bwana akajitukuza kwaajili yake.
Baadae Samweli akapata mwanamke Aitwaye Delila, ambaye alijua kwa huyo yamkini anaweza kuwa baba wa familia. Samsoni akampenda kweli huyo mwanamke, kumbe mwanamke alikuwa na ajenda zake za siri ambazo zilimfanya awe na Samsoni. Samsoni hakujua hapo awali yeye aliangalia upendo tu🤔 Delila alilenga kupata fedha alizoahidiwa na wakuu wa wafilisti kwamba akiweza kumshawishi mpaka kujua Siri ya nguvu zake Basi atapewa fedha nyingi Sana Kama Yuda alivyofanya kwa Yesu.
Tukirejea mstari wetu hapo juu kweli Delila alifanikiwa kumshawishi Samsoni mpaka kutoa Siri ya nguvu zake kwamba zipo kwenye nywele zake. hatima yake ilikuwa mbaya sana aliponyolewa zile nywele aliishiwa nguvu zake ndipo wafilisti. walipopata nafasi ya kumkamata na kumfunga gerezani ,huko wakamtoboa macho yake na hatma yake ikaishia huko mpaka alipo kufa.
*Nataka kusema nini kuhusu historia hii fupi ya Samsoni ni kwamba;*
*Usipuuzie watu wa karibu yako / wanaokuja kwenye maisha yako, kwa sababu KUSUDI na HATMA yako vinaweza kuathiriwa vibaya na watu wa karibu yako, Ambao unaona wanaweza kuwa watu wa maana kwako.*
Samsoni aliingia kwenye mtego wa jaribu bila kujua kuwa lile ni jaribu la hatma yake kwa Mungu, hatma yake ikawa mbaya sana.
Yamkini umezaliwa kwa kusudi fulani na Shetani akikutazama anakusudia kupoteza tu, Sasa zipo njia nyingi ambazo Shetani huzitumia kuwajaribu Wana wa Mungu.
Ishi kwa akili na watu wanaokuzunguka / Wapime kwa mizani ya Kiroho ili kujua watu sahihi wa kuambatana nao. Shetani hutumia vitu vya karibu yako kukujaribu ,lengo ili usishtuke kwamba hili ni jaribu, mpaka utakapoharibikiwa ndipo unakuja kujuta.
Angalia watu unaoshirikiana nao kazini , kanisani, kwenye jamii ya kawaida yamkini hata nyumbani mwako anaweza kuwa ni;
Rafiki, mchumba / Mke / Mume uliyempata wakafanyika jaribu kwako hata kuliuwa kusudi la Mungu ndani yako na hatma yako ikawa mbaya.
Unajikuta ghafla unapoa na kushuka kiroho kumbe ni Aina ya watu unaoambatana nao.
Kama hakuna ulazima wa wewe kuambatana na watu fulani waache maana watakupunguzia mwendo.
Ili kulinda usalama wa Roho yako na kusudi / Hatma yako mbele za Mungu
Si kila mtu unaweza kuambatana naye kila mtu ameumbwa kwa kusudi lake na kwaajili ya mtu fulani na si kila mtu, So kila mtu anapaswa kuzijua Siri zako wengine hawapaswi hata kujua unaishi wapi hata Kama ni wapendwa.
Siku yakikupata madhara hutawaona tena maana watakuwa wamekamilisha kusudi la Shetani alilolikusudia kwako kukuangusha.
Mungu anakutegemea wewe Linda hatma yako na kusudi la Mungu ndani yako lisiharibiwe na mwovu. kazi ya mwovu ni; kuiba hatma yako
kuharibu hatma yako na
kuchinja hatma yako.
*Yohana 10:10*
[10]Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Umepata Neema ya kumjua Kristo na unayohuduma ndani yako , Kuna mahali Mungu anatamani ufike hivyo tunza Sana hiyo Neema, Shetani asije akaitwaa taji yako bila kujua ukabaki kuishi tu kwa mazowea na usifikie kwenye hatma yako njema.
Mungu akubariki Sana
*TUOMBE🙏*
Ee Mungu Mwenye mamlaka na Enzi yote tunakushukuru kwa kuwa ni mwema kwa maana fadhiri zako ni za milele. Umetukirimia Neema ya ajabu nasi tunauona utukufu wako kila iitwapo leo.
Hata sasa Bwana tuko mbele zako tena tukiomba Rehema na nguvu zako viwe juu ya maisha yetu
Tusaidie Bwana tuishi kwa Akili Hekima na Maarifa yatokayo kwako ili tuweze kujipatia nguvu ya kushindana wakati wa uovu.
Baba Mungu tunalibariki jina lako maana wewe u mwaminifu siku zote.
Katika Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amen🙏.
Mungu akubariki
Taifa Teule Ministry
Mwl. Beata Silwimba
0742442164 /0620507212
Maoni
Chapisha Maoni