Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2023

SHIDA YA MIAKA 17 HADI 27 KWA MABINTI

Picha
  SHIDA YA MIAKA 17 HADI 27 KWA MABINTI Binti nakusalimu kwa jina la Yesu.   Kuna Kitu kidogo chenye ukubwa ambacho mabinti wengi hawakifahamu mwisho wa siku wanaambulia machozi mengi pale wanapofika kwenye kipindi cha kuolewa. Kama binti unayejitambua na una mpango wa kuwa na ndoa yako takatifu na maisha ya amani. Basi naomba nikufundishe kitu ambacho ni kigumu kukimeza lakini ndivyo kilivyo.  Ni hivi🤔 Mabinti wengi wenye umri kuanzia miaka 17,18, 19,20,21,22,23 hadi 27 huwa 👉 wanakuwa katika kipindi ambacho miili yao inazungumza kwa sauti kubwa sana 👉Wanatumia muda mwingi sana kukaa kwenye kioo kujilemba na kujipamba kwa mapambo mengi 👉Na pia katika umri huu ndipo mabinti wengi hujitazama na kujiona kuwa wao ni wazuri kuliko wanawake wote duniani 👉Ni kipindi ambacho binti anajiona sana na kujikubali sana. 👉Ni kipindi ambacho mabinti wengi wanatumia akili zao na huona kuwa wana uwezo wa kufanya kila wanachokifikiri kuhusu ndoa.  Anakuwa kama mke wa potifa ambaye alipojiona ana k

NAFASI YA MKE KATIKA KUHARIBU NDOA YAKE

Picha
  NAFASI YA MKE KATIKA KUHARIBU NDOA YAKE Bwana Yesu asifiwe mabinti wa Kristo leo naomba kukujulisha kuhusu jambo fupi sana ambalo limekuwa ni tatizo kwenye ndoa nyingi, bila kujua kwamba Biblia imetoa mwongozo mzuri tu kwa namna ya kuishi baina ya mke na mume. Tusome hapa👇 Waefeso 5:25-26 [25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; [26]ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; Ukisoma vizuri Biblia utagundua mbali na mambo yote ndani ya ndoa, mwanaume ameambiwa jambo moja la msingi ambalo Mungu alimaanisha kitu fulani ndani yake. Jambo lenyewe ni WAPENDENI WAKE ZENU. sasa unaweza usielewe kwanini Mungu alimwambia hivi mwanaume. Kwa asili Mungu alipomuumba mwanamke, alimpa asili ya kitu kinachoitwa MWITIKIO. Sasa huu mwitikio unategemea sana kutoka kwa mume wake, yaani ni kwamba mwanamke ameumbwa kama mtu mwenye sifa ya👇 👉Kuitikia maono yanayotoka kwa mume 👉Kuitikia upendo kutokana na upendo wa mume 👉Kuiti

TUNZA UAMINIFU WAKO KWA MUNGU

Picha
  TUNZA UAMINIFU WAKO KWA MUNGU Karibu tujifunze kwa ufupi somo hili na Mungu akusaidie kuelewa. Tunaposema Uaminifu( kuwa mwaminifu), ni Hali ya kuweka nia moyoni mwakona kuzingatia kufanya yote uliyoagizwa na Mungu au mtu yeyote mtu wa namna hii tutamwita ni mwaminifu. Yeremia 7:28 Nawe utawaambia, Taifa hili ndilo lisilosikiliza sauti ya BWANA, Mungu wao, wala kupokea mafundisho; uaminifu umepotea, umekatiliwa mbali na vinywa vyao. Lakini nyakati za sasa na kizazi hiki wengi wamekosa uaminifu kwa asilimia kubwa  mpaka inafikia watu kuogopana wenyewe kwa wenyewe. uongo kwenye vinywa vya watu imekuwa kawaida. Mungu ameagiza tupendane Lakini ndugu haohao ndio wanao uwa ndugu zao, ndugu haohao wanabaka na kulawiti watoto kwenye jamii zetu, ndugu huyo huyo unamwamini unamuweka kwenye duka lako ndo huyo anakufilisi, uaminifu umepungua baina ya watu na kuleta changamoto kwenye jamii zetu mtu anajiuliza nitamwamini nani sasa🤔. kwa mabinti na vijana uaminifu umepotea kabisa unapotamani kuol

UWE MWAMINIFU HATA KUFA

Picha
  UWE MWAMINIFU HATA KUFA  Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.    Karibu katika wakati mwingine wa kujifunza maneno ya Mungu na leo tutatazama kifungu cha Ufunuo 2:9-10 Karibu sana...... Soma hapa👇 Ufunuo wa Yohana 2:9-10 [ 9]Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. [10]Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. Leo naomba tutazame kifungu hiki cha Biblia ambacho kanisa la pili liliambiwa. 👉Kipindi hiki ni kipindi ambacho kanisa la Mungu(waliookoka) walikuwa wakipitia kipindi kigumu cha mateso mengi chini ya wafalme kumi   👉Ni kipindi ambacho watu waliabudu kwa taabu sana na ilikuwa si ruhusa kumuabudu Mungu aliye hai bali Rumi walikuwa na miungu yao ambayo waliwataka watu wote waiabudu hiyo na wafalme wengine walitaka kuabudiwa wao. 👉Kani

USIYAKATAE MAFUNDISHO YENYE UZIMA

Picha
USIYAKATAE MAFUNDISHO YENYE UZIMA Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, ni saa nyingine naomba kukujulisha ujumbe huu kuhusu kanisa la nyakati za mwisho yaani mimi na wewe. Hebu soma hapa maana ndipo penye msingi wetu wa leo👇 2 Timotheo 4:3-4 [ 3]Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; [4]nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Karibu sana......  Biblia inatuambia kwamba, katika nyakati fulani kutatokea jambo la ajabu sana si kwa wapagani bali kwa wale wale waliyopo ndani ya kanisa na jambo lenyewe ni hili👇 "Kukataliwa kwa mafundisho yenye uzima"   Haya mafundisho yenye uzima ni yepi?  Hebu soma hapa👇 Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."  Biblia inasema Kristo alitolewa ili kila AMWAMINIYE asipote

KUHESHIMIWA NA MUNGU

Picha
KUHESHIMIWA NA MUNGU Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu,  Ne siku nyingine, naomba jifunze jambo ambalo linamfanya mtu aheshimiwe na Mungu.  Zaburi 8:4-6 “ Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.” 👉 Inawezekana unajiuliza ni kwa namna gani Mungu anaweza kuniheshimu mimi mwanadamu niliye mtu tu, lakini ni vizuri sana ujue ya kwamba Mungu anaweza kukuheshimu na kukupandisha juu ijapokuwa wanadamu wamekushusha na kukudharau.  👉Yapo mambo ambayo ukiyafanya yanapelekea Mungu akuheshimu na kukupandisha juu zaidi ya unavyodhani. Neno ‘heshima’ lina tafsiriwa kama tetemekea au ogopewa au hofiwa, au kupewa kipaumbele.  đź‘ŹSasa Ukiheshimiwa unatetemekewa;  đź‘ŹUkiheshimiwa unapendelewa, unasemeshwa kwa adabu.  đź‘ŹUkiheshimiwa unaogopwa na kuhofiwa na watu duniani. Kulingana na tafsiri ya neno hili, tuangalie maana ya heshima ya