USIYAKATAE MAFUNDISHO YENYE UZIMA
USIYAKATAE MAFUNDISHO YENYE UZIMA
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, ni saa nyingine naomba kukujulisha ujumbe huu kuhusu kanisa la nyakati za mwisho yaani mimi na wewe.
Hebu soma hapa maana ndipo penye msingi wetu wa leo👇
2 Timotheo 4:3-4
[3]Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
[4]nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
Karibu sana......
Biblia inatuambia kwamba, katika nyakati fulani kutatokea jambo la ajabu sana si kwa wapagani bali kwa wale wale waliyopo ndani ya kanisa na jambo lenyewe ni hili👇
"Kukataliwa kwa mafundisho yenye uzima"
Haya mafundisho yenye uzima ni yepi?
Hebu soma hapa👇
Yohana 3:16
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
Biblia inasema Kristo alitolewa ili kila AMWAMINIYE asipotee bali awe na UZIMA wa milele
👉Sasa kumbuka Yesu alipokuja duniani alianza kuwafundisha watu habari za ufalme wa Mungu ambapo kuna watu walimkubali na wengine kumkataa. Lakini Biblia inakiri kuwa alifanya ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
Kwa lugha nyingine ni kwamba yale mafundisho aliyokuwa anayatoa ndiyo yaliyokuwa yanampa mtu nuru na uzima pale tu anapoamini. Yeye mwenyewe alisema hivi👇
Yohana 8:12
[12]Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Sasa kumfuata Kristo ni kuyashika mafundisho yake na kuyaishi jambo ambalo litakufanya uwe katika nuru ya Kristo, na ndiyo maana mtu asiyefuata maagizo ya Yesu hana tofauti na mpagani wote wapo gizani.
Soma hapa👇
1 Yohana 1:6
[6]Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;
Sasa baada ya Kristo kumaliza muda wa yeye kuwepo duniani, alituachia maagizo kwamba na sisi tuhubiri kama alivyohubiri yeye, yaani tuhubiri mafundisho yanayompa uzima kila atakayisikia na kuamini.
Na ndiyo maana mitume walianza kuhubiri injili ya Yesu kwa nguvu na ushindi na hata kanisa la Mungu likaongezeka kwa kasi sana kwasababu yale mafundisho yalikuwr ni mafundisho ya uzima., yaliyojaa kukemea dhambi, kulinda utakatifu, kuonya na mengine kama hayo, ambayo watu waliyoyakubali walifanyika wa thamani sana na yanamfanya mtu kumuona Mungu kwenye maishr yake, na kumpa uhakika wa kuingia katika ufalme wa Mungu.
Lakini Biblia inatupa ishara ya hatari katika nyakati za mwisho kwamba wengi ambao zamani walikuwa wanafuatisha njia ya Mungu na kuyashika mafundisho ya uzima, lakini watajitenga na mafundisho hayo na kuyakataa.
Biblia inaposema KUKATAA maana yake kuna watumishi wa Mungu ambao watakuwa wakiyatoa mafundisho kama hayo yaliyojaa maonyo, na mambo ya utakatifu, lakini wasikilizaji ndiyo hawatahitaji mafundisho ya namna hiyo.
👉Kitakachofuata ni makanisa ya watumishi wa namna hiyo yatapungukiwa na waumini waliokuwepo awali,
👉Na watu kipindi hicho, Biblia inatabiri kwa kusema kwamba WATAJITAFUTIA WALIMU MAKUNDI MAKUNDI
Ikiwa na maana kuwa kila mtu atanya udadisi wa kuona ni mwalimu gani au muhubiri gani anayemfaa kulingana na kile anachokifundisha muhubiri au mwalimu huyo.
Kama ni watu wasiopenda kukemewa basi watawatafuta walimu ambao wao hawajui kukemea dhambi, yaani wao kila siku ni mafundisho ya kuinuliwa tu bila kujali waumini wao wapo rohoni au mwilini.
Wengine watakuwa na mafundisho kuhusu kutokula vyakula vya aina fulani.
Wengine watakuwa wanatoa mafundisho ya kuwazuia watu wasioe.
Yani mafundisho yatakuwa ni tofauti na yale ya Yesu ambayo kimsingi ndiyo mafundisho yaletayo uzima.
Na huko ndiko kujitenga na imani.
Hebu soma hapa👇
1 Timotheo 4:1-3
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
[2]kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
[3]wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
😯Sasa kama ni mtu uliyeokokr ni lazima usiishi kihasara bila kuwr na utambuzi wa majira na nyakati.
Hata sasa, unaweza kufumba macho yako japo kwa dakika moja tu, halafu anza kutafakari juu ya mafundisho unayoyasikia kila siku kutoka kwa watumishi mbalimbali na kisha ujipe jibu mwenyewe kwamba kanisa limefika kwenye nyakati za hatari au bado.
👉Tafakari kuhusu mafundisho ya Kristo na mitume wake, halafu fananisha na mafundisho ya siku hizi za leo.
👉Tafakari kuhusu nafasi yako, je ni mafundisho gani unapenda kuyasikia? Je yanakupa tumaini gani?
👉Tafakari je hujayakataa mafundisho ya uzima na kujitenga na imani?
Chukua muda kidogo tafakari kuhusu mafundisho yanayotolewa kanisani kwenu na walimu wenu, je ni mafundisho yenye uzima au yasiyo ea uzima?
KUMBUKA
Aina ya mwalimu unayemfuata imebeba hatima ya mavuno yako ya baade yaani kile anachokulisha ndicho hichohicho ambacho utakuwa nacho.
Kama Mwalimu wako ni dhaifu basi ni lazima utumie jitihada zako ili uwe imara mbali na hapo unakuwa dhaifu kama alivyo yeye.
Ambapo ni jambo la hatari sana katika nyakati za mwisho kwa hali ilivyo na itakavyoendelea kuwa, yaani inawahitaji watu wenye nguvu na uelewa wa kutosha ili kushinda.
Soma hapa👇
Mathayo 11:12
[12]Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Na kama Mwalimu wako ni mzuri basi na wewe utakuwa mzuri sana kwa msaada wa Mungu na ndiyo mapenzi ya Mungu kwamba wote tuwe vizuri kwa kuyashika mafundisho ya uzima, kujua kweli halisi na kuwa huru kweli kweli hata kuuteka ufalme wa Mungu na kumweka chini shetani.
Lakini hii wakati mwingine hutegemea na nani anayekulisha chakula au ni nani anaye kuongoza.
Soma hapa👇
Mithali 27:17
[17]Chuma hunoa chuma;
Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
Kama wewe ni chuma basi lazima unolewe na chuma, au kama unahitaji kuwa chuma basi mwalimu wako anatakiwa kuwa chuma.
Lakini katika nyakati za mwisho wengi watapotea na kibaya zaidi hawatajua kwamba wanapotea.
Watahisi kwamba wamepata walimu ambao hawawaonyi, hawawakemei, wala kuwaonya, kila siku ni kufarijiana tu, kutiana moyo tu bila kujua kuna upande wa pili wenye tiketi ya kumuona Mungu mbali na hizo faraja wanazopewa na walimu wao.
Soma hapa👇
Waebrania 12:14
[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Katika kipindi ambacho kanisa linatakiwa kuyapenda maonyo na masomo kuhusu utakatifu basi hiki ni kipindi pekee kwasababu ndicho kipindi ambacho ajenda ya watu kuanza kujitenga na imani nr kutokutaka mafundisho yenye uzima ya Kristo inaingizwa duniani na ndani ya kanisa na mwovu shetani.
✋Penda kusikiliza mafundisho yenye uzima hata kama yanakuumiza, lakini baada ya hapo unayafanyia kazi na unaendelea kuwa mkamilifu
Maana ukiyafanyia kazi kwa kurekebisha pale ulipokuwa unakosea, basi jua hata siku nyingine hayatakuumiza tena maana hayakudai kitu.
✋Lakini wengi leo hii wakiinywa kwa madhambi yao, wanafikiri muhubiri anawahukumu,
👉Kijana akionywa kidogo tu, hata kama alikuwa anaimba kwaya utashangaa ameacha. Eti amezila...
👉Binti alikuwa anaimba praise ukimuonya tu, hataki tena kuimba anataka mumbembeleze, ananuna.
Mimi nakuambia wewe, wewe nhe, hujui tu unachokifanya kwr kutokujua majira uliyopo.
👉Kipindi hiki unatakiwa ukionywa basi upige magoti mbele za Mungu, uimbe toba kwa dhambi uliyokuwa unaifanya bila kujua.
Usionyeshe kiburi unapoonywa
Usionyeshe dharau unapofundishwa mafundisho yenye uzima
Usijaribu kuyakataa mafundisho ya Kristo.
Na ukiona una tabia ya kukataa mafundisho ya uzima basi jua hata Roho mtakatifu umemzimisha na unaongozwa na roho nyingine ya shetani kwasababu hata Roho mtakatifu hafanyi vitu kwa mapenzi yake bali kwa mapenzi na mwongozo wa Yesu Kristo.
Soma hapa👇
Yohana 16:13
[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Kwahiyo ukikataa mafundisho ya uzima basi jua umempinga Roho mtakatifu hadharani kabisa.
Tena Yesu akaongezea kwa kusema
Yohana 16:14-15
[14]Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
[15]Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.
Chochote anachokwambia Roho mtakatifu amekichukua kwa Kristo na hata wale watumishi wanaofundisha mafundisho yenye uzima, pia nao wanaongozwa na Roho mtakatifu kwasababu wanachokifundisha ni cha Yesu mwenyewe na ndicho hata yeye alikifundisha.
Je umeokoka? Kama bado, je unahitaji kumpokea Yesu leo?
Kama upo tayari bila kulazimishwa basi piga simu kwa namba hiyo hapo chini ili nikusaidie kwa jina la YESU.
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl/ Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni