TUNZA UAMINIFU WAKO KWA MUNGU
TUNZA UAMINIFU WAKO KWA MUNGU
Karibu tujifunze kwa ufupi somo hili na Mungu akusaidie kuelewa.
Tunaposema Uaminifu( kuwa mwaminifu), ni Hali ya kuweka nia moyoni mwakona kuzingatia kufanya yote uliyoagizwa na Mungu au mtu yeyote mtu wa namna hii tutamwita ni mwaminifu.
Yeremia 7:28
Nawe utawaambia, Taifa hili ndilo lisilosikiliza sauti ya BWANA, Mungu wao, wala kupokea mafundisho; uaminifu umepotea, umekatiliwa mbali na vinywa vyao.
Lakini nyakati za sasa na kizazi hiki wengi wamekosa uaminifu kwa asilimia kubwa mpaka inafikia watu kuogopana wenyewe kwa wenyewe. uongo kwenye vinywa vya watu imekuwa kawaida.
Mungu ameagiza tupendane Lakini ndugu haohao ndio wanao uwa ndugu zao, ndugu haohao wanabaka na kulawiti watoto kwenye jamii zetu,
ndugu huyo huyo unamwamini unamuweka kwenye duka lako ndo huyo anakufilisi, uaminifu umepungua baina ya watu na kuleta changamoto kwenye jamii zetu mtu anajiuliza nitamwamini nani sasa🤔.
kwa mabinti na vijana uaminifu umepotea kabisa unapotamani kuolewa au kuoa unaanza kuwaza nitamuoa nani au nitaolewa na nani ambaye atakuwa mwaminifu kwangu. imekuwa changamoto. Mungu akusaidie
Mpaka ndani ya ndoa uaminifu haupo wanandoa wanaishi kwa wasiwasi bila kuwa na imani baina yao, unadhani ni kwanini uaminifu umepotea? Nikwasababu maovu yamezidi juu ya uso wa nchi na wengi wamemuweka Mungu mbali nao.
*Yapo Mambo yanayoweza kukusaidia kutunza UAMINIFU ndani yako kwa Mungu na kwa watu wengine pia.*
1. Weka akiba ya NENO la MUNGU, ndani yako.
zaburi 119:11
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
wewe kama mkristo aliye hai hakikisha siku isipite bila kusoma Neno la Mungu maana Mungu atakukumbusha kutenda haki kupitia kwenye Neno lake, Tenga masaa yako ya kusoma Neno na kuomba utakuwa na hekima, na hekima ya Mungu humpa mtu maarifa ya kutenda haki, kuwa mwaminifu.
2. Tunza agano/ kusudi la Mungu ndani yako( maono yako) ili kuigikia hatima yako
ukisoma;
Mwanzo 49:1_23
hapo tunajifunza habari za Yusufu mtumishi wa Mungu alitunza uaminifu wake kwa Mungu kukataa kulala na mke wa boss wake yaani mke wa Potifa.
mke wa boss wako, au boss wako asikushawishi kutenda mabaya eti kwasababu anakulipa msharaha au kwa kigezo kwamba atakupandisha cheo au kukuongeza mshahara, au kukupa kipaombele acha kabisa mara moja kama unaona no ngumu ukiweza kimbia kabisa dhambi inakimbiwa si kwa kukemea kwa maombi tu. Yusufu asingekimbia angelala na Yule mwanamke maono yake ya kuwa mtu mkubwa ndo yangekufa pale, wewe ni wathamani sana kuwa mwaninifu utauona ukuu wa Mungu kwenye maisha yako.
3. Simamia misingi yako ya IMANI.
Usikubali kudanganywa nabkuyumbishwa imani na watu wasio na mafundisho ya ukweli, utajikuta unapoteza uaminifu wako, badala ya kuamini Jina la Yesu kwamba linaweza kukuponya unaanza kuamini majina ya watu fulani maarufu, unaanza kuamini vitambaa, chumvi ,Maji ya upako ,mara mafuta ya upako mara sabuni, kama siyo uganga ni nini
wagalatia 3:1-3
1. Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?
[2]Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
3. Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?
🔥Hakuna aliye kuloga umejiloga mwenyewe kwa kupoteza uaminifu wa Imani ya kweli.
4. kuwa na ushirika mzuri na Mungu na wanadamu pia
Luka 2:52
Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
tamani kuwa karibu na Mungu Kila wakati weka ushirika naye kwa Maombi na IBADA itakusaidia kutunza UAMINIFU kwa Mungu wako.
5. Ondoa Roho za Visasi (Malipizi), na Uchungu ndani yako.
Hii inaweza kukupelekea ukakosa uaminifu hata kwa watu wengine.
Mfano umebebelea watu fulani moyoni waliokutendea ubaya ,una uchungu wa kuumizwa na watu wengine, hii itakufanya ulipize kisasi hata kwa watu wengine
hata kwenye ndoa pia siyo afya, futa watu waliokukosea na uwasamehe Jenga uaminifu upya kwa watu na kwa Mungu utafurahia maisha.
6. Hakikisha unaishi maisha yenye USHUHUDA MZURI, ili kutunza UAMINIFU wako kwa Mungu na mbele za wanadamu pia
utaaminika Kila mahali, kwanza Mungu atakuamini kwasababu uaminifu wako unamtambulisha yeye ndani yako
utaaminika kazini,
utaaminika na familia yako
utaaminika kwa Mume / mke wako
uaminifu no kitu Cha Thamani Sana pia huleta Heshima.
kama unataka kuheshimika Mpende Mungu halafu kuwa mwaminifu Kila mtu atakupenda🥰 japo so wote watakupenda, wale wanaowaza mabaya juu yako ndo hawatakuelewa 😄
7. Toa zaka na sadaka zako za dhabihu mbele za Mungu.
Soma Malaki 6:1_...... mjaribu Mungu kwa kumtolea uone kama hayo Mambo yako yaliyoshindikana yanavyofunguka na kwenda sawa😄
Acha kuona kila siku wewe ndo unamajukumu mengi na Mambo mengi wewe Kila siku bajeti inakubana mpaka unakosa pesa ya kutoa zaka ( unakula zaka🤔)nihatari Sana, Huwezi kuwasaidia wahitaji, Huwezi kuwalisha watumishi wa Mungu.umepoteza uaminifuwako kwa Mungu,kumbuka sadaka humpatanisha mtu na Mungu
kumbuka ni mara ngapi umemuahidi Mungu kwamba utachangia ujenzi wa kanisa au Nyumba ya mchungaji na haujatimiza🤔, umeweka nadhiri nyingi na haujatimiza hata moja mpaka sasa
ulimuomba Mungu akupe kazi utamtolea zaka kwa uaminifu ,sasa mbona unamuibia Mungu?
Penda ibada, wewe Kila siku za IBADA ndo unapata safari ya biashara , au kusalimia ndugu.
mwingine siku ya IBADA ndo anapumzika nyumbani na kufua nguo😄 mwingine ndo siku ya kula bata. uaminifu wako uko wapi?. Mwanzo ulikuwa ukikosa IBADA unaumia moyo, Leo hii hata hishituki umesongwa na na Mambo mengi ya ulimwengu huu.utakufa vibaya na watu watakuzika, ukifika mahali panapokustahili ndo utatamani urudi duniani angalau utemgeneze na Mungu na haitawezekana. na ndo kilio na kusaga meno milele. Geuka leo Amua kurejea kwa Mungu naye kwa upole atakupokea
kwa watumishi mnaotumiwa na Mungu uliomba kuinuliwa kwenye viwango vizuri vya kiroho ili umtumikie Mungu kwa ukubwa zaidi , lakini kiburi kinatoka wapi, Jeuri inatoka wapi, kujiinua na kujitangaza jina kwa umaarufu wako binafsi inatoka wapi hii, Umeinuliwa sawa ,wewe mwinue Mungu kwenye utumishi wako.
Wale waimbaji, umepewa saauti mzuri ukiimba unawabariki watu wengi na wengi wanafunguliwa kupitia huduma yako lakini kujiinua kunatok wapi na kujiona hapo kanisaniusipo kuwepo Basi watu hawataimba ,usipomtumikiaungu kwa unyenyekevu na kumwinua Mungu tu yeye ataondoa hicho kilichopo ndani yako, ndipo mtu anabaki kusema nilikuwaga nahubiri Mimi, nilikuwaga naomba Mimi? kabla hatari mbaya hazijaja kwako acha tabia hizo na Mungu atakuamini zaidi utakuwa kila siku unajiona unakuwa na kuongezeka kiviwango🙌
🔥oooh kwako wewe kijana au Binti, ni mara ngapi au ni wangapi umewaahidi utawaoa au utaolewa nao kumbe unawadanganya,umekuwa muongo kila mahali huaminiki tena, Binti wa watu au kijana anakusubiria wakati mwingine anakuombea kabisa akiwa na matarajio mazuri kumbe wewe ulishaamua kumwacha kisirisiri. Uaminifu wako uko wapi?🤔 Binti wawatu au kijana anashitukia unatangaza uchumba tu na mtu mwingine😭
Na wewe uliyepo kwenye ndoa tayari, wakati mnachumbiana mpaka mnafunga ndoa mliwekeana ahadi kwamba mtapendana na kushirikiana katika furaha na huzuni ( yaani katika Mambo yote mbona wewe umemsaliti mwenzako na kutafuta ndoa ya nje? mbona nyumbani wakila dagaa wewe unaenda hotelini kula vizuri upendo wako wa mwanzo uko wapi 🤔 mmmmmm najaribia kutafakari naogopa Sana Maana niwengi Sana watachomwa moto siku ya mwisho kwa kupoteza uaminifu.
🎤Nikukumbushe kitu kingine tena cha Muhimu Sana,
Ukikosa Uaminifu Kuna vitu Utaavikosa ukiwa hapa duniani na hata maisha yako baada ya kufa, yaani maisha ya milele uliyojichagulia
_kwanza kabisa Utaukosa uzima wa milele kwa kupoteza uaminifu wako
_pia unaweza kupoteza kazi yako mzuri, kwa kukosa uaminifu, unapenda rushwa , unapendelea watu kwasababu ya cheo chako. utapoteza CV yako mzuri uliyonavo sasa.wakati unajaza mkataba ulikubali kuwa mwaminifu Leo hii umepoteza uaminifu kazini, utapotezaa cheo , nafasi ya uongozi au kazi kabisa.
_unaweza kumpoteza Rafiki mzuri,mchumba, Mke au Mume wako kwasababu ya kukosa uaminifu kwa mwenzako
_Pia unaweza kukosa Heshima na kibali Cha kusikilizwa, kuwekewa Dhamana, kukosa kushirikishwa kwenye baadhi ya Mambo ya kifamilia na jamii kwa ujumla na itakupelekea kutouyafikia maono yako nabaadhi ya mazingira kwasababu ya kukosa uaminifu.
👏Nakushauri amua Leo na utoke huko uliko, wewe unajua ni wapi umepoteza uaminifu wako kwa Mungu na hata kwa jamii yako. Mwambie Mungu natoka huku niliko jisafishe ,jioshe uwe mwaminifu tena uaminike tena na Mungu ili akuamini kwa Mambo makubwa zaidi.
Ulimwengu na mazingira fulani, Au Mafanikio fulani, au watu fulani visikutoe kwenye uaminifu uliokuwa nao mwanzo au ulionao sasa.
Ukiwa mwaminifu Mungu anakuinua kuliko ulivyotarajia kwa akili zako.
Soma kitabu Cha ;
Danieli 6:4
Waebrania 3:5
Mungu akupe neema hiyo uwe mwaminifu na uutunze UAMINIFU wako kwa Mungu na wanadamu pia.
wewe ni wa Thamani Sana .Ubarikiwe Sana na Mungu aliye hai🙏
Taifa Teule Ministry
Mwl. Beata Silwimba
0742442164 / 0620507212
Maoni
Chapisha Maoni