KUHESHIMIWA NA MUNGU



KUHESHIMIWA NA MUNGU

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, 

Ne siku nyingine, naomba jifunze jambo ambalo linamfanya mtu aheshimiwe na Mungu. 

Zaburi 8:4-6

Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.”

👉 Inawezekana unajiuliza ni kwa namna gani Mungu anaweza kuniheshimu mimi mwanadamu niliye mtu tu, lakini ni vizuri sana ujue ya kwamba Mungu anaweza kukuheshimu na kukupandisha juu ijapokuwa wanadamu wamekushusha na kukudharau. 

👉Yapo mambo ambayo ukiyafanya yanapelekea Mungu akuheshimu na kukupandisha juu zaidi ya unavyodhani.

Neno ‘heshima’ lina tafsiriwa kama tetemekea au ogopewa au hofiwa, au kupewa kipaumbele. 

👏Sasa Ukiheshimiwa unatetemekewa; 

👏Ukiheshimiwa unapendelewa, unasemeshwa kwa adabu. 

👏Ukiheshimiwa unaogopwa na kuhofiwa na watu duniani.

Kulingana na tafsiri ya neno hili, tuangalie maana ya heshima ya kidunia au heshima inayo tolewa na dunia.

👉 Ili mtu aheshimiwe na dunia lazima awe na vitu fulani fulani hivi. 

Vitu hivyo ni Elimu, Kazi, Mali, Utajiri, Fedha na nafasi aliyonayo katika jamii. 


Watu wanamuheshimu Msomi, Profesa, au mwenye degree kwa sababu amesoma. 

Mbunge anaitwa mheshimiwa kwa sababu ya nafasi yake katika jamii. Wewe kwa sababu sio mkurugenzi huwezi kuitwa mheshimiwa, watu watakuheshimu kwa sababu ya nafasi yako katika jamii, au mali zako. Ndio maana wakati mwingine unaweza kumwona mtoto mdogo anaitwa muheshimiwa au bosi kwa sababu ya fedha au mali aliyokuwa nayo. 

Sababu nyingine inayosababishwa mtu aheshimike katika jamii ni kujitoa kwake kwa ajili ya watu wengine, kujitoa kwa ajili ya wengine katika shida na mahitaji yao, labda chakula maji n.k. Mtu mwenye moyo wa kusaidia watu anaheshimika katika jamii husika. 

Heshima ya dunia inaambatana na jinsi unavyoonekana machoni pa watu; unavaa nini, unakula nini, unaendesha nini.

 Mahali unapolala je, ni nyumba ya ghorofa, au ya udongo, pia unacho kula je unakula maharage kila siku, au anaishi morogoro lakini chakula cha mchana (lunch) unakula America na chakula chako ni mlo kamili? Wanaangalia unava nini, je mavazi ya kizamani na yaliyochakaa au mapya? Wakiona ulivyovaa wanakuheshimu.

Dunia inaweza kukuheshimu lakini Mungu hajakuheshimu, dunia inaweza kukutukuza kwa ajili ya mali, utajiri na mambo yako katika jamii lakini bado Mungu akawa hajakuheshimu. Mungu humweshimu mwanadamu si kwa sababu ya mambo wanayodhani wanadamu, si kwa ajili ya fedha, mali au utajiri. Mungu anaweza kukuheshimu hata kama hujawahi kuwa kiongozi, huna fedha au elimu n.k

Inawezekana huna fedha wala mali na utajiri, wala hujasaidia jamii, huna lolote lile. Kwa sababu hiyo umekosa heshima kwenye jamii na kwenye macho ya watu. Kwa sababu ya hayo kulala kwako, kula yako, na mavazi yako ni duni sana kiasi kwamba umekuwa kicheko kwa jamii. Unavaa nguo moja na kiatu kimoja.

😦Umekata tamaa na umewaza kuwa mimi sasa siheshimiki na mtu huku, ukiyataja mambo ambayo huna, labda siitwi kwenye kikao kwa sababu ya elimu yangu, hawaniambii habari za sherehe kwa kuwa sina fedha. 

🙏Nakuambia leo usiogope kwa maana Mungu anavyo mweshimu mtu ni tofauti kabisa na wanadamu wanavyo heshimu.

👉Kuna heshima ya kimungu ambayo Bwana anataka kukupa wewe na kupitia hiyo analenga uheshimike kwenye jamii. Kuna watu waliwahi kusema wamekosa heshima kwa kuwa hawana fedha, mali na utajiri, na kwa sababu hiyo wakakata tamaa na mwisho wakasema kumtumikia Bwana hakuna faida.

👉Duniani hapa kuna vitu vinavyokupa heshima ambazo ni fedha, mali, utajiri. 

Lakini Bwana Yesu alikuja ili wewe upate heshima, si heshima ya kidunia. Kuheshimiwa na Mungu ni tofauti sana na kuheshimiwa na mwanadamu na ukiheshimiwa na Bwana utashangaa utaheshimiwa na wale wanadamu walio kudharau kwa maana umepita vigezo.

Sababu pekee inayokufanya wewe uheshimiwe na Bwana ni moja tu, na hiyo ni kumtumikia Bwana.

👉 Watu wanaweza kukuacha kwa sababu huna vitu vya kidunia, lakini kwa kuwa umeamua kumtumikia Bwana, yeye anasema ukitaka nikuheshimu lazima unitumikie. Mawazo ya Mungu ni tofauti na ya wanadamu, sababu pekee itakayo kufanya utetemekewe na uogopwe na watu, uitwe kwa heshima ni lazima umtumikie Bwana.

Usiwaze kuwa Mungu anakuheshimu sababu wewe ni Profesa, ua mwenye fedha na mali, Mungu anakuheshimu kwa sababu moja tu nayo ni kumtumikia yeye. Ukimtumikia yeye anakuheshimu. Mungu haangalii cheo chako, mali, nafasi ya kazi yako bali anaangalia utumishi ulio ndani yako.

🙂Huenda hujuhi maana ya kumtumikia Bwana;

👉 Kumtumikia Bwana ni kuifanya kazi ya Mungu, kumwabudu, kumtii na kumtegemea yeye. Kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, kuenenda katika njia ya Bwana, kuzishika amri zake na yote aliyo kuagiza. Ni kushikamana na Mungu kwa mali yako na kila kitu ulicho nacho. 

Soma hapa👇

Yohana 12:26

Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.” 

Ukimtumikia Bwana atakuheshimu, Yesu anasema ukimtumikia Mungu pale atakapokuwepo yeye na wewe utakuwepo. Kwa maana nyingine pale utakapokuwapo wewe na yeye atakuwepo, kwenye kazi yako, biashara, n.k, yaani ukimtumikia Mungu ukikaa mahali unakunywa chani naye anakuepo, ukiwa umelala naye anakuwepo, ukiwa ofisini naye yupo. Mungu yupo kila mahali utakapo kuwepo naye atakuwepo lakini kwa sharti moja, ukimtumikia.


Soma hapa👇

Yohana 14:1-3

Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.” 

👉Mungu umweshimu mwadamu si kwa ajili ya mambo ya kidunia, si kwa ajili ya mali au cheo chako katika jamii, anasema ukimtumikia yeye atakuheshimu. Ni kutumika tu, kunakofanya uheshimike mbele za Mungu na mbele za wanadamu wote.

👉Uthamani wako kwa Mungu hautokani na fedha au mali wala cheo chako, unatokana na kumtumikia Bwana. Ukimtumikia Mungu yeye anakupenda na anakuthamini, na kwasabau hiyo anatoa watu kwa ajili yako na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. 

Soma hapa👇

Isaya 43:4

Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.” 

👉Mtu anayemtumikia Mungu anaweza kuonekana si kitu mbele za watu, hana mali, fedha na kila kitu lakini Mungu anamheshimu na akaisha kumheshimu yeye anafanya jambo linalo sababishia kuheshimika kwenye maisha ya watu. Na zaidi anatafuta watu watakao kusimamaisha, kwahiyo usikate tamaa, kwa maana Bwana atakuheshimisha na atatoa watu kwa ajili yako.

👉Ingawa ukijitazama ulivyo, wewe mwenyewe umejishushia heshima. Ukitazama ukoo wenu hakuna aliye soma, hakuna tajiri wala mfanya biashara mwisho unajitamkia ‘mimi si heshimiki,’. Lakini ukiamua kumtumikia Bwana yeye anakuheshimu kwa namna ya tofauti, ukiheshimiwa na Mungu hakuna mwanadamu asiweza kukuheshimu, yeye atawalazimisha watu wakuheshimu. 

Kinacho kufanya usiheshimiwe na hata sasa hujaheshimiwa ni kwakuwa ujachagua kumtumikia Bwana, umejaribu kazi umekosa, huna elimu, huna mali, kimsingi umekosa sifa za kuheshimiwa na mwandamu kwa sababu hiyo hata watu wamtaani wanakuona hufai. Lakini ukimtumikia Bwana unaheshimiwa na Mungu naye anatoa watu wakuheshimu wewe kwa jina la Yesu. 

Unaweza kuwa na sifa ya kidunia lakini usiheshimike, una kazi, biashara, elimu lakini huheshimiki, kwakuwa shetani anaweza kufunika heshima yako. Ukiamaua leo kumtumikia Bwana, yeye anakuletea watu kwa ajili yako, anakuheshimu nawe unaheshimika tena.

Mungu ana majina mengi; wakati anamtuma Musa kuwaokoa wana wa Israeli, Musa alimuuliza Mungu ‘nikawatambulishe watu wako kuwa wewe ni nani?’ Mungu akasema kawaambie kuwa ‘Niko ambaye Niko’ amenituma kwenu, yaani Mungu huwa chochote wakati wote, maji wakati wa kiu, chakula wakati wa njaa, tiba wakati wa magonjwa

Unajua🙂

Mungu anakutafsiri na kukulinganisha na yeye, kiasi kidogo kuliko Mungu. Ukimtumikia Mungu binadamu mwingine anakuona katika nafasi ya juu, yani Bwana anakupa heshima na kukuinua hata unaheshimiwa na wengine kwa maana anakuvika taji ya heshima na utukufu. Ukimtumikia Mungu anakutwadha ili umiliki, utawale na kutiisha na anaweka vitu chini ya miguu yako, 

Usipo mtumikia Mungu upo katika hali ya hatari, kuna dakika inaweza ikatokea ukabadilishwa toka katika nafasi uliyo nayo hata kutupwa chini. Lakini ukimtumikia Bwana vitu vyote vinatiwa chini ya miguu yako, ukiamua umiliki au uache ni wewe tu kwa maana umemtumikia Bwana, ukiamua unachotaka kiwe kina kuwa kuwa kwa jina la Yesu.

Watu wemetumikia elimu, mume, cheo, mchumba lakini hivyo vyote vimeondoka. Ukimtumikia Bwana mambo yote yanaweza yakaisha lakini Bwana anakuvalisha taji, na anakuheshimisha na kukupandisha tena kwa jina la Yesu.


MIFANO YA KIBIBLIA WALIO HESHIMIWA PASIPO VIGEZO VYA KIDUNIA

1.PETRO NA YOHANA

Walimtumikia Mungu kwa moyo na watu wakawa wanawaogopa na kuwatetemekea. Hawakuwa na kitu, mali, elimu, wala fedha lakini walimtumikia Mungu naye akawavalisha taji ya utukufu na heshima kiasi kwamba watu wakawaheshimu kwa namna ya ajabu watu waliona kuwa kama wapo na Yesu, wakafanya ishara na mambo makuu kupitia hayo wakaheshimiwe na watu na kuwatafuta popote walipoenda.

Soma hapa👇

“Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao, wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana.” (Matendo 4:13-16)

Soma hapa👇

Matendo 3:6

Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.” 

Kitu cha Bwana kikionekana ndani yako unaheshimika, haijarishi hauna fedha au mali, kupitia hicho ulichopewa na Bwana unaheshimika. Kupitia huduma yako Bwana atakupatia fedha, mali, utajiri na utaheshimika. 


2.YOHANA MBATIZAJI

Yohana mbatizaji alimtumikia Mungu na kuifanya kazi yake, kupitia hiyo Bwana akamheshimisha, akaheshimiwa na watu wote na kila mtu akamhofia na kumtetemekea kwakuwa alikuwa na roho ya Mungu. Ijapokuwa Yohana hakuwa na mali, wala fedha na alivaa mavazi duni, alimtumikia Mungu na Bwana akamheshimisha. 

Soma hapa👇

Luka 3:3-7

wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani. Akafika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi, kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa; Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu. Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?

Heshima ya kiduna inategemea unakula nini, unavaa nini au unalala wapi, lakini kati ya hayo halikuwapo hata moja kwa Yohana. 

👉Yesu anasema Yohana alivaa mavazi duni na kuishi jangwani lakini alifuata na watu hivyo nawe ukimtumikia Bwana watu wote watakufuata na kukuheshimu. 

3.YUSUFU

Yusufu kwa ajili ya ndoto zake nduguze wakakusudia afe. Kwakuwa waliona ni ndugu yao wakakusudia kumuuza, wakamuuza Misri kwa potifa na akiwa huko alitumika kama mfanya kazi wa ndani. Akapata kibali kwenye nyumba ya Potifa, chakushangaza mke wa potifa akamtaka kimapenzi na kwakuwa Yusufu alikuwa mwaminifu akakataa. Alipo kataa akasingiziwa mwisho akafungwa gerezani.

👉Akiwa gerezani aliwakuta watu wenye shida kama yeye na taabu kama yeye, wafanyakazi wa Farao mnyweshaji na mwokaji, wakaota ndoto naye Yusufu akawatafsiria ndoto zao kisha wakatolewa gerezani, mmoja akarudishwa kazini na mwingine akanyongwa. Siku moja Farao naye akaota ndoto na akakosa mtafsiri, lakini yule aliyetoka gerezani akamwambia mfalme yupo aliye tutafsiria ndoto yetu tulipokuwa gerezani na ikawa hivyo hivyo. Mfalme akaagiza Yusufu aitwe atafsiri ndoto.

Kwakuwa alikuwa na kitu chenye ufumbuzi kwenye jamii akatolewa gerezani, akanyolewa nywele, akabadilishwa mavazi na kumpandisha kwenye gari la mfalme na kumpeleka mbele ya Mfalme. Yusufu akatolewa gerezani hadi kwenye kiti cha Farao.

👉Yusufu akamwambia mfalme mimi sina uwezo wa kutafsiri ndoto bali ile roho ya Mungu ikaayo ndani yangu.

✋ Sisi tunaye mtumikia Bwana ni mawakili wa siri za mbinguni, ukimtumikia Bwana anakujulisha mambo ya siri ya mbinguni ambayo wengine hawana.

Yusufu akaitafsiri ndoto ya mfalme kama ilivyo na akatoa ushauri, akamwambia mfalme atafute mtu mwenye akili na hekima ataye kusanya chakula katika kipindi chote cha chakula kifae wakati wa njaa. Na mimi leo nakushauri mtumikie Bwana na ukimtumikia Bwana utapata heri. 

👉Mfalme akaangali kote asione mtu wa kuifanya kazi hiyo, akamwambia Yusufu ‘tupate wapi mtu mwenye akili na hekima na mwenye roho ya Bwana kama wewe, kwakuwa wewe Mungu amekufahamisha mambo haya, wewe ndio utakaye kuwa mkuu kuwa mtawala wa haya’. 

😁Ukimtumikia Bwana anakuheshimisha na kukuweka mashauri ndani yako kupitia hayo unaheshimika na kupewa mamlaka. 

Ndipo Farao akamweka Yusufu juu ya misri yote, akamwambia watu wangu wote wa Misri watataliwa na kwa neno lako. 

   👉Bwana alimtoa Yusufu gerezani hadi kumfanya kuwa mkuu juu ya misri, akatukuzwa, akaogopwa na akaheshimika.

✋Ukimtumikia Mungu haitoshi wewe kuitwa mheshimiwa, kiwango chako ni kikubwa na cheo chako ni zaidi ya raisi mbele za Mungu. Anaye mtumikia Mungu anakuwa na akili na hekima kuliko watu wote. Yusufu kama angefanya dhambi asingeweza kuwa juu ya Misri, nakushauri wewe usitende dhambi, usipo tenda dhambi utatolewa kotaka gerezani hadi kuwa mkuu.

Kuna mambo fulani ambayo Mungu anaruhusu uyapitie ili akupandishe, ili mlazimu Mungu mtu huyu ‘Yusufu’ kuingia gerezani ili anapatoka asirudi tena kwa Potifa bali awe mkuu mbele ya nchi yote ya Misri. Shida unayopitia isikufanye umtende dhambi Mungu, ijapokuwa upo katika shida Bwana ameruhusu hiyo ili kupitia hiyo akuinue na akuketishe na wakuu. 

👉Historia yako si muamuzi wa maisha yako, bali muamuzi wa maisha yako ni utumishi wa Mungu ulio ndani yako. 

👉Ukimtumikia Mungu anabadirisha maisha yako, ukimtumikia Bwana anakuletea kesho yako mpya haraka kama Yusufu.

👉Yesu anaweza kukubadirisha jina, ulikuwa umepotea sasa umeonekana, Mungu alimbadirisha Yusufu jina kutoka mfungwa hadi mkuu. Yamkini umesha teseka mno wamekuzomea, wamekucheka lakini ukimtumikia Bwana yeye atabadiri historia yako kutoka maskini hadi tajiri. 

Ili uweze kuheshimiwa na Mungu jambo la kwanza umpokee Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Ukisha mpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako unafanyikiwa kuwa mtoto wa Mungu na unapewa haki za kifalme. Unapata nguvu ya kumtumika na ukimtumika yeye anakuheshimisha.

Mashetani wakiona una Mungu ndani yako wanatetemeka, Yesu na wanafunzi wake walipoenda katika mji wa wagerasi walikutana na mtu mmoja mwenye pepo, alipo mwona Yesu, akaogopa akatetemeka. Kwahiyo ukimtumikia Bwana unakuwa mtu wa tofauti hata mapepo wanakuheshimu na kukuogopa kwa jina la Yesu.

 Mungu akubariki sana 


Taifa Teule Ministry

Mwl/Ev Mathayo Sudai

0744474230 /0628187291 

Maoni

  1. SoMo zuri Sana nimejifunza kitu kikubwa Sana hapa Mungu akubariki na azidi kukutumia kwa kazi za Ufalme wake.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI