SHIDA YA MIAKA 17 HADI 27 KWA MABINTI
SHIDA YA MIAKA 17 HADI 27 KWA MABINTI
Binti nakusalimu kwa jina la Yesu.
Kuna Kitu kidogo chenye ukubwa ambacho mabinti wengi hawakifahamu mwisho wa siku wanaambulia machozi mengi pale wanapofika kwenye kipindi cha kuolewa.
Kama binti unayejitambua na una mpango wa kuwa na ndoa yako takatifu na maisha ya amani.
Basi naomba nikufundishe kitu ambacho ni kigumu kukimeza lakini ndivyo kilivyo.
Ni hivi🤔
Mabinti wengi wenye umri kuanzia miaka 17,18, 19,20,21,22,23 hadi 27 huwa
👉 wanakuwa katika kipindi ambacho miili yao inazungumza kwa sauti kubwa sana
👉Wanatumia muda mwingi sana kukaa kwenye kioo kujilemba na kujipamba kwa mapambo mengi
👉Na pia katika umri huu ndipo mabinti wengi hujitazama na kujiona kuwa wao ni wazuri kuliko wanawake wote duniani
👉Ni kipindi ambacho binti anajiona sana na kujikubali sana.
👉Ni kipindi ambacho mabinti wengi wanatumia akili zao na huona kuwa wana uwezo wa kufanya kila wanachokifikiri kuhusu ndoa.
Anakuwa kama mke wa potifa ambaye alipojiona ana kila kitu, basi akafikiri anaweza kuwa na Yusufu.
😦Na ndiyo maana Mabinti wengi wenye umri huu utawakuta wana mahusiano na wanaume ambao ni watu wazima kabisa
Unafikiri shida ni nini?
Shetani hufanya kazi kwa bidii sana ili kuuendesha mwili wa binti aliyepo kwenye rika hili akiwa na lengo la kumharibia maisha yake ya baadae
Kivipi?
Huyu binti mwenye mihemko kama hii kwenye umri huo, huwa akifikisha miaka 29 hada 32, anakuwa tayari
👉ameshaanza kufunguka akili,
👉Ameshaanza kuwa na uhitaji wa kupata ndoa
👉Ameshaanza kuwa na uhitaji wa kuwa na mwenza wake
👉Anaanza kujuta kwa ujinga wa ujanani ambao haujampa alichokuwa anakitaka.
Lakini bahati mbaya MUDA UNAKUWA UMEPITA wa kufanya maandalizi sahihi ya ndoa nzuri, na kinachofuata ni maumivu na kuona ubaya wa maisha.
👉Anakuwa tayari ameshauchezea ujana wake kwa kile wanachokiita kula ujana.
Na wanaume wanaanza kumuona hana thamani maana wameshamchezea sana alipokuwa kwenye mihemko ya dunia hii na ndiyo maana anaweza kuwa ni mzuri tu, ana kazi nzuri tu, ana pesa nzuri tu, lakini ndoa hana,
🙂 ni kwasababu kila mwanaume ameshamjua na amechezea usichana wake.
👉Wanaume huwa wanaanza kusema HANA SOKO TENA
👉HANA JIPYA
Na ndiyo maana Biblia imesema👇
Mhubiri 12:1
[1]Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,
Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,
Wala haijakaribia miaka utakaposema,
Mimi sina furaha katika hiyo.
Siku mbaya kwa binti ni pale ambapo muda wa kuolewa umefika na anauhitaji wa kuolewa lakini inashindikana.
Ukifikia hali kama hiyo binti angali umesikia habari hii basi usije ukaanza kufikiri kuna mtu amekuroga ili usiolewe maana hapo unakuwa umejiroga mwenyewe.
Kwasababu👇
👉Umri unakuwa umeshaenda sana na huna tena nguvu kubwa ya kujipanga na kinachofuatia ni kusema kauli kama hizi👇
1. NIPO TAYARI KUOLEWA NA MTU YEYOTE
2. NAHITAJI NIWE NA MTOTO TU MASWALA YA NDOA SIYO LAZIMA
3. WANAUME WA SIKU HIZI HAWAELEWEKI
Binti, wanaume wapo wengi kulingana na wewe ulivyo.
Kabla ya kusema hawaeleweki, jiangalie kwanza wewe je unaeleweka.?
🙇♀️Kumbuka, jicho la kumuona mwenye hekima na busara analo mwenye hekima na busara.
NINI KIFANYIKE
Kwenye kipindi ambapo wengi wanashinda kwenye kioo, wewe binti wa Kristo shinda kwenye maombi
Muombe Mungu kuhusu maisha yako ya ndoa ambayo utaihitaji
Ukitumia muda mwingi kuomba basi jua Roho mtakatifu anaanza kukuandalia mume sahahi kabisa kwa ajili ya maisha yako.
Ninakuhakikishia kuwa ukiwa hivyo, basi ukifika muda wa kuolewa utashangaa umekutana na mtu sahihi hadi utashangaa, na hayo ndiyo majibu ya kushinda kwenye maombi mapema.
👏Acha kufanana na wanawake wasioelewa chochote, wajinga wasio na akili na hawataki kumtafuta Bwana, wao kazi yao ni kushinda saluni, na kwenye vioo tu kujiangalia uzuri wao lakini ghafla machozi yanaanza kuwatoka kwenye maisha yao yote.
Hebu jiulize, kwanini mwanamke anaweza kuwa na kila kitu lakini utashangaa hajaolewa wala kuchimbiwa au unakuta ana mtoto tu na hana mume, shida nini?
Ukiona unashinda kwenye kioo na unajiona kuwa wewe ni mzuri kuliko watu wote basi jua upo kwenye hali mbaya na wala haupo kama unavyojiona
Wewe si wa kwanza kuwepo, wala si mzuri kupita wote
Ila siri ya kuwa mzuri kuliko wote ni kuutumia ujana wako na Kristo, kesha kwenye maombi, na hapo wewe utakuwa ni mzuri kuliko wanawake wote wasiotaka kuwa na akili
na hapo ndipo penye akili, yaani kumtafuta Bwana.
Hebu soma hapa👇
Zaburi 53:2
[2]Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu,
Aone kama yuko mtu mwenye akili,
Amtafutaye Mungu.
Binti mwenye akili si yule anayetumia kile anachokiita uzuri ili kuwa na kila mwanaume, bali binti mwenye akili ni yule anayetumia Roho yote, akili yote na nguvu zote kwa ajili ya kumtafuta Bwana.
Achana na kushinda muda mwingi kujipamba kwa vitu vya muda bali jipambe kwa utu wa ndani.
Ni lazima ujue hata mume anayejitambua na anayemcha Bwana sawasawa, huwa hawezi kuwa na uwezo wa kumtaka mwanamke wa namna hiyo.
Kwahiyo kulingana na unavyojiweka ndivyo vivyohivyo unawapata wa namna kama yako.
👏Hapa nina maana ifuatayo👇
UKIONA UMEOKOKA HALAFU VIJANA WENGI WAKIUME WANAKUTONGOZA NA WENGINE KUKUSOGELEA KWA KUKOSA ADABU NA WENGINE KUKUZOEA BILA MISINGI SAHIHI, BASI NI LAZIMA UJUE WOKOVU WAKO HAUJAKAA SAWA, KWA NAMNA UNVYOISHI NA NDIYO MAANA KILA KIJANA HAOGOPI KUKUTONGOZA ILI KUTIMIZA HAJA YAKE.
HIVYO UNAPOONA VIJANA WENGI WAKIUME WANAKUZOEA KIPUMBAVU, USIJIONE KUWA NI MZURI SANA, BALI JUA TAA YA WOKOVU WAKO UMEIZIMA
👉Ogopa sana wanaume ambao wanapenda kujichekesha kwako, wakiwa na lengo la dhambi.
👉Ogopa sana kupoteza ushuhuda kwenye kipindi cha ujana wako maana wakati wa uzee hutoweza kuubadilisha
👉Ogopa sana kujifanya umeokoka halafu kumbe unatumia ujana wako kujishibisha haja za mwili
👉Ogopa sana kuwa na mahusiano na vijana ambao hata habari za Mungu hawazitaki angali wewe umeokoka kwasababu ni kazi kuyatimiza mapenzi ya Mungu, waache wamataifa wawazike wamataifa na wewe mwisraeli halisi jenga ushirika na Mungu wako vizuri ili akupatie mwisraeli na hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.
Na Mungu akubariki sana.
Taifa Teule Ministry
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 / 0628187291
Maoni
Chapisha Maoni