SADAKA YA AMANI ILIKUWAJE
SWALI: Sadaka ya Amani ilikuwaje? Mimi ni MATHAYO DAUDI SUDAI karibu katika kujua jinsi sadaka ya amani ilivyokuwa. Sadaka ya amani, ilikuwa ni sadaka inayotolewa kwa Mungu kutokana na amani mtu aliyoipata; Tofauti na ambavyo ingeweza kutafsirika kuwa ni sadaka ambayo mtu angeitoa kwa Mungu ili kupatana naye! (yaani kurejesha amani na Mungu), lakini sivyo, haikuwa na maana hiyo!. Wana wa Israeli walitoa aina hii ya sadaka, pale ambapo ndani yao walipata amani. Na amani hiyo ilitokana na Mungu kuwafanyia jambo Fulani zuri katika Maisha yao labda kuwafanikisha, au kuponywa magonjwa au kupatanishwa na maadui zao n.k. Hivyo kutokana na amani hiyo walimtolea Bwana sadaka ya kumshukuru, ndio iliyojulikana kama sadaka ya Amani. (Na sadaka Hii ilikuwa ni sadaka ya hiari na haikuwa ya amri, maana yake mtu hakulazimishwa kumtolea Mungu, ni kwajinsi atakavyojisikia yeye, kama ameona kuna sababu ya kumshukuru Mungu kwa amani basi alimtolea, kama aliona hakuna sababu basi aliacha!, hakulazimishwa