NINI MAANA YA DERAYA

  SWALI:Deraya ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 59:17

Mimi ni MATHAYO SUDAI Karibu tuifunze ujumbe huu wa maana ya deraya.

JIBU: Tusome,


Isaya 59:17 “Akajivika haki kama DERAYA KIFUANI, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho”.


Deraya ni jina lingine la “ DIRII ”. Dirii ni vazi la chuma, askari walilokuwa wanalivaa kipindi wapo vitani, vazi hilo lilikuwa linafunika eneo la kifua na tumbo!, hivyo hata mkuki ukirushwa kwa bahati mbaya ukafika maeneo ya tumbo au kifua, basi usingeweza kupenya kwasababu ya vazi hilo gumu la chuma, lililopo kifuani. (Unaweza kusoma pia 2 Nyakati 26:14).


Lakini hii Deraya au Dirii, inafunua nini kiroho?, au inawakilisha nini katika roho?


Tusome tena hiyo Isaya 59:17.. “Akajivika haki kama DERAYA KIFUANI , na chapeo cha wokovu kichwani pake”


Umeona hapo?..kumbe Deraya au Dirii inafananishwa na HAKI, na chepeo yaani Helmet inafananishwa na Wokovu.. Sawa sawa na Waefeso 6:14..


Waefeso 6:12-14 

''12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na KUVAA DIRII YA HAKI KIFUANI”


Haki inayozungumziwa hapa, sio ile HAKI inayotokana na Matendo yako!, bali ni ile inayotokana na IMANI THABITI YA KUMWAMINI BWANA YESU.


Tunapopata Ufunuo wa Yesu ni nani?, na kujua kuwa kwa kupitia yeye tumepata ondoleo la dhambi, na yeye ndiye vazi letu mbele za Mungu, na kwamba tunahesabiwa haki bure! Kwa njia ya yeye, basi tunakuwa na Amani, na HAKI hiyo ni silaha tosha ya kumshinda shetani, ambayo kiroho ndio Dirii au Deraya.


Warumi 5:1 -2 

“1BASI TUKIISHA KUHESABIWA HAKI ITOKAYO KATIKA IMANI, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

2 ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu”.


Je! Umemwamini Yesu?, kama bado basi kiroho huna dirii kifuani mwako, na adui shetani, ana uwezo wa kukudhuru wakati wowote, na kukumaliza kabisa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI