JE YUDA ATAHUKUMIWA KWA KUTIMIZA UNABII?
SWALI Je! Yuda atahukumiwa na Mungu kwa dhambi yake ya usaliti?
Mimi ni MATHAYO DAUDI SUDAI ungana na mimi kwa habari ya kujifunza dhambi ya Yuda na
Je! Yuda atahukumiwa na Mungu kwa dhambi yake ya usaliti? Na wakati ulikua mpango wa Mungu Bwana Yesu afe kwaajili ya ukombozi?.
Endelea.......
JIBU: Ndio Yuda atahukumiwa kama mkosaji..Kwasababu Bwana Yesu huyo huyo alisema..
Marko 14:21 “… lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu; ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa”.
Hapo Bwana anasema ingekuwa heri kwake kama asingalizaliwa, maana yake mtu atakayemsaliti atakuwa na kosa kubwa sana. Haijalishi maandiko yametabiri au la!.
Sasa swali la msingi ni kwanini iwe ni kosa ilihali imeshatabiriwa na maandiko lazima yatimie?
Ili tuelewe vizuri hebu tusome tena unabii mwingine uliootolewa na Bwana ambao haujatimia bado lakini utakuja kutimia siku za mwisho.
Mathayo 7:21-23
21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Huo ni unabii Bwana alioutoa ambao bado haujatimia, lakini umeelenga baadhi ya watu, kwamba siku ile watamfuata Bwana na kumwambia maneno hayo, na Bwana atawakana sawasawa na alivyotabiri.
Sasa hebu tujiulize!.. Hao ambao watatimiza unabii wa kukanwa na Bwana siku ya mwisho, watakuwa hawana hatia au makosa, kwasababu tayari walikuwa wameshatabiriwa hayo?.
Kama jibu ni hapana!..basi hata Yuda anayo hatia ya kumsaliti Bwana hata kama unabii umetabiri hayo..
Kumbuka Bwana hakuwatajia jina la atakayemsaliti..alisema tu mmoja wenu atanisaliti akaishia hapo!!..hakuendelea zaidi kumtaja mtu jina, Ndio maana wanafunzi wake wote walikuwa na wasiwasi kuwa unabii unawazungumzia wao.
Marko 14:18-20
” 18 Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti.
19 Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi?
20 Akawaambia, Ni mmoja wa hao Thenashara, ambaye achovya pamoja nami katika kombe”.
Tofauti ya Yuda na mitume wengine 11 waliosalia ni Kwamba Yuda hakuwa anazingatia unabii wa kumsaliti Bwana hivyo baada ya kuusikia haukumshtua, aliendelea kuishi atakavyo.
Lakini wakina Petro na mitume wengine, waliingiwa na hofu na kauli hiyo ya Bwana, hivyo hata kama kulikuwa na roho ya usaliti ndani yao iliyoanza kuingia basi waliipambana nayo iondoke na hatimaye wakaishinda, lakini Yuda ilimshinda na ikamvaa..
Umeona?
Ni sawasawa tu na Bwana alivyosema..“watakuja wengi siku ile na nitawaambia siwajui”.Na watu leo wanalipuuzia neno hilo wala hawaogopi, bado wanaendelea na uzinzi, bado wanaendelea na ulevi, uasherati, uuaji, usengenyaji, wizi n.k unategemea vipi watu wa namna hii wasitimize huo unabii wa Bwana katika siku ya mwisho???
Hii ni tahadhari kwetu, kwamba tujitakase, ili tusiutimize unabii huo, kadhalika lengo la Bwana kutoa unabii wa yeye kusalitiwa ni tahadhari ya mitume wasije kumsaliti.
Je umeokoka????..au ni mkristo jina tu!
Maandiko yanasema..
Mathayo 7:21-23
“21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Maoni
Chapisha Maoni