Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2025

KAMA MUNGU ANAJIBU MAWAZO KWANINI TUNAOMBA??

Picha
KAMA MUNGU ANAJIBU MAWAZO KWANINI TUNAOMBA ?? Na: Minister Mathayo Sudai Bwana asifiwe karibu tujifunze tena hapa... Katika somo la nyuma tulijifunza kwamba Mungu ANAJIBU MAWAZO YAKO SIYO MANENO YAKO... Kama hujalipitia somo hili ni vizuri ukalipitia ili ukija Kuendelea uwe unaelewa vizuri... Bofya link hii hapa kwa somo hilo kabla hujaendelea na hili👇👇 https://elimuyabiblia.blogspot.com/2025/03/mungu-anajibu-mawazo-yako-siyo-maneno.html Kama umeshaelewa njoo tuendelee... Tuliishia kwenye kujiuliza 👉Kama ni hivyo kwamba Mungu anajibu mawazo Kuna haja gani ya kuomba??? 👉Je nikiwa nawaza tu pekeyake si inatosha mimi kupata majibu?? Lakini tukasema Jibu ni kwamba Japo kuwa Mungu ameyajibu mawazo yako lakini majibu yako hutayapata mkononi mwako mpaka utakapoomba(kutamka uliyokuwa unawaza) 🤔🤔 SASA Ili kuelewa hapa ni lazima tukubaliane na Biblia kwamba Mungu anapohitaji kumuhudumia mwanadamu huwa hafanyi yeye bali watumishi wake ndiyo huwa wanafanya kazi hiyo na watumish...

MUNGU ANAJIBU MAWAZO YAKO SIYO MANENO YAKO...

Picha
MUNGU ANAJIBU MAWAZO YAKO SIYO MANENO YAKO... Min Mathayo Sudai Bwana asifiwe wana wa Mungu... Njoo tujifunze kuhusu jinsi Mungu anavyoyatazama mawazo yako, na ukilijua hili hautadharau mawazo yako tena.... Kimsingi Mungu na Shetani wanapenda au hutenda kazi kupitia ulimwengu wa mawazo ya mtu yaani jinsi unavyowaza... (The realm of thoughts) Isaya 65:24 [ 24]Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia. Unaona kujibiwa kunaanza hata kabla ya mtu kutamka kile anachokihitaji... Kwasababu kile ambacho unakitamka ni matokeo ya vile unavyowaza, kabla hujaanza kuomba ni lazima utawaza kile kitu ambacho utakiomba... Kwa mfano.                                                                                             ...

KAMA BWANA ASINGALIKUWA MSAADA WANGU....

Picha
KAMA BWANA ASINGALIKUWA MSAADA WANGU.... Min. Mathayo Sudai Bwana asifiwe wana wa Mungu  Karibu tujifunze neno la BWANA Tuanze hivi👇 Zaburi 94:17 [ 17]Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya. Ulimwengu huu umejawa na mambo mengi sana ya ajabu ambayo yanalenga kuangamiza nafsi za watu, na kuwatoa watu nje ya makusudi ya Mungu... Kimsingi Mungu wetu ni mwaminifu kwasababu huilinda nafsi ya kila mtu mwenye dhambi na hata aliyeokoka na ndiyo maana watu wote hao wapo duniani.... Ni kweli kabisa kwamba kama Mungu asingekuwa anamlinda mtu basi wanadamu wangeshawekwa palipo na kimya (mautini)... Hapo Daudi anakiri kwamba kuishi kwake yeye ni Mungu tu na kama isingekuwa hivyo basi yeye asingekuwepo yaani angeshakufa muda mrefu.. Si Daudi tu, unaweza kujiangalia wewe mwenyewe hapo ukaelewa kwasababu 👉Kama si mkono wa Mungu uliokuvusha kwenye ile kesi basi muda huu huenda ungekuwa jera 👉Kama si Mungu kuwa upande wako pengine ungeuawa k...

KWANINI ULIMWENGU HAUKUMKUBALI YESU ANGALI YEYE NDIYE ALIYEUUMBA???

Picha
KWANINI ULIMWENGU HAUKUMKUBALI YESU ANGALI YEYE NDIYE ALIYEUUMBA??? Bwana asifiwe, karibu tujifunze... Biblia inasema hivi 👇 Yohana 1:10-11 [ 10]Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. [11]Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Tunaposoma biblia Kuna kitu cha msingi tunakiona hapo kwamba Yesu ndiye aliyehusika kuumba ulimwengu lakini inaonekana alipokuja ulimwenguni tena ulimwengu aliouumba mwenyewe na siku zote yupo humo lakini ulimwengu haukumtambua na hata wale ambao walikuwa wake walimkataa yaani hawakumpokea.. Je ni kwanini??? Ni jambo la ajabu sana kama umemzaa mtoto halafu baadae anakuwa hakujui tena na hata ukimfuata anakukataa yaani hakupokei bila shaka ni lazima Kuna kitu ambacho kimempata mtoto huyo maana si kawaida.... NI HIVI👇 Adamu alipoumbwa na Mungu (kristo Yesu ), ulimwengu ulikuwa chini yake na kila kitu kilikuwa sawa maana nuru ya Mungu ilikuwepo lakini baada ya shetani kumdanganya Adamu na kufan...

TAFUTA KUKUA, USIRIDHISHWE NA SHETANI

Picha
TAFUTA KUKUA, USIRIDHISHWE NA SHETANI Na:Minister Sudai Bwana Yesu asifiwe sana watu wa Mungu, karibu tujifunze kitu cha msingi kuhusu kukua kiroho... Soma hapa👇 Wakorintho 13:11 [11]Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Hapa Paulo anazungumza jinsi ambavyo unapaswa kuwa na utofauti kwa jinsi ulivyokuwa mtoto na ulivyo Leo... Jambo hili ni la kulitazama zaidi kwa mambo ya rohoni kwasababu kabla hujawa mtu Mzima kiroho ni lazima uwe mtoto na si ajabu biblia inalithibitisha hilo.....👇 Waebrania 5:13-14 [13]Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. [14]Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya. Unaona hapo...?? Mtu mzima si mtu aliyeokoka muda mrefu au Ana umri Mkubwa bali kunahusisha sana jinsi anavyoenenda kwa mambo ya ...