JE DINI YAKO NI SAFI ?
JE DINI YAKO NI SAFI ?? Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu... Duniani kumekuwa na kundi kubwa la watu wanaojiita wakidini, na huku wengine wakidhani ya kuwa dini Yao ndiyo bora kuliko ya wengine n.k ni lazima ujue Neno Dini maana yake ni Njia ya mtu kuelekea kwa Mungu.... na ndiyo maana hata Yesu mwenyewe alisema kwamba yeye ndiye njia ya kweli na uzima... na akaongeza kwamba mtu yeyote hawezi kwenda au kumfikia Mungu bila kupitia njia hii au dini hii yani Yesu Kristo.... Yohana 14:6 [6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Sasa ni lazima utambue kwamba wale ambao tunasema tunamfuata Yesu ndiyo tunaitwa WAKRISTO.. lakini katika dunia ya Sasa wengi waaitwa wakristo lakini hawamfuati Yesu Kristo Bali wanaenda tu kwasababu walikuta wazazi wao wapo kwenye Hilo... na wengine hawamfuati Yesu kwasababu wameamua kufuata mifumo ya kimadhehebu na kidini kutoka kwa wale waliowafundi...