NITAKUTAPIKA UTOKE....

     


NITAKUTAPIKA UTOKE....

BWANA Yesu asifiwe wana na binti za MUNGU.... KARIBU katika ujumbe huu wa leo na leo tutaangalia, kuhusu Mungu kumtapika mwanadamu.

Ufunuo wa Yohana 3:15-16
Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

Hapa Yesu alianza kusema NAYAJUA MATENDO, YAKO YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO. Kumbe ubaridi wa mtu unatazamwa na matendo yake, na umoto wa wa mt pia unatazamwa kwa matendo yake. matendo yako wewe ndiyo yanayokutafsirisha mbele za Mungu kwamba wewe ni Moto au Baridi, na ni lazima ujue kuwa kuwa moto maana yake ni kuwa upande wa Mungu na kuwa baridi maana yake ni kuwa upande wa shetani.... lakini hali hizo zote zinaonyeshwa na aina ya matendo yako..

kumbe kuna matendo yanayomwakilisha Mungu uliyenaye na kuna matendo ambayo yanamwakilisha shetani ndani yako... yaani matendo yako ndiyo yanaeleza kwamba uko chini ya Mungu au shetani✋✋

Sasa kuna wakati huwa unafika Mungu anapomtazama mtu anamkuta huyu mtu haeleweki, kwasababu kuna wakati anayafanya mapenzi ya Mungu na kuna wakati anayafanya mapenzi ya shetani, mtu huyu anashindwa kutambulika kwamba anamtumikia nani hasa, maana matendo yake yanaonyesha kuwa anawatumikia mabwana wawili, au anashiriki ibada katika mahekalu mawili tofauti; la shetani na la Mungu.

1 Wakorintho 10:20-22
........Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.  Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.  Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

Hapo ukisoma vizuri utagundua kumbe Mungu anampenda mtu aliye moto yaani upande wake... lakini si hivyo tu pia anapenda mtu ambaye amejiweka kwa shetani kwa matendo yake yaani mtu anayeeleweka kwamba yupo wapi✋✋

KIVIPI MUNGU ANAPENDA MTU ALIYE BARIDI...
Ni kwamba mtu anapokuwa baridi kabisa, Mungu huwa anamvumilia na kumtazamia akijua kabisa pengine kuna wakati huko mbele mtu huyo atakuja kumwamini Yesu na kuokoka..

2 Petro 3:9

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.

Lakini mtu anapokuwa vuguvugu maana yake haeleweki, wakati mwingine hata Mungu anashindwa kumpa jukumu la kufanya pale ambapo anafanya mapenzi ya Mungu kwasababu Mungu anaona hata hilo jukumu linaweza kufeli kwasababu ya aina ya mtu, mtu huyo ni lahisi kukuvamia na kukutumia , hivyo Mungu anasema atamtapika mtu huyo....


Mungu anaposema atamtapika yaani atamkataa, atamfukuza kwake, hana nafasi mbele za Mungu mtu huyo, kwasababu walio wa Mungu ni lazima wamwabudu Mungu na kufanya yale yanayompendeza Mungu tu.

👉Unapokuwa unasali na kutoa sadaka na huku unamchukia mtu basi tambua wewe ni vuguvugu..

👉unapomwabudu Mungu na huku unafanya uasherati/uzinzi basi jua wewe ni vuguvugu

👉unaposema umeokoka au unampenda Mungu na huku huna utakatifu unapokuwa mwenyewe basi jua kuwa wewe ni vuguvugu...

Kuna watu ambao wanajionyesha kuwa watakatifu wanapokuwa makanisani, wanapenda kujitangaza kwamba ni wakristo, wanapenda sana kujitangaza kwamba ni wafungaji wazuri, na wengine utakuta wana huduma fulani makanisani mwao lakini akiwa mwenyewe basi vitu anavyoviangalia kwenye simu yake ni AIBU TUPU... HUYU NAYE NI VUGUVUGU...


Lakini Mungu anasema watu wa namna hii ATAWATAPIKA WATOKE KWAKE.


Wewe Mtu wa Mungu unayesoma ujumbe huu, tambua kwamba kufanya dhambi hadharani au kwa siri na huku ukiwadanganya watu kuwa ni mkristo basi tambua kwamba Mungu bado amekupa neema ya kutubu na kutulia na yeye katika hali ya UMOTO ili ukaye naye daima.... acha kuishi maisha yasiyompendeza Mungu, acha kufutisha namna ya dunia hii, acha kuigiza kwa maficho ya kidini kwasababu Muda tulionao ni mchache sana yatupasa kuyatenda mapenzi ya Mungu....


1 Petro 4:2-5
Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu; mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.  Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.

MUNGU AKUBARIKI SANA

Taifa Teule Ministry
Min. Mathayo Sudai
0744474230/0714732009

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI