JE DINI YAKO NI SAFI ?

               JE DINI YAKO NI SAFI ??

Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu...

Duniani kumekuwa na kundi kubwa la watu wanaojiita  wakidini, na huku wengine wakidhani ya kuwa dini Yao ndiyo bora kuliko ya wengine n.k

ni lazima ujue Neno Dini maana yake ni Njia ya mtu kuelekea kwa Mungu.... na ndiyo maana hata Yesu mwenyewe alisema kwamba yeye ndiye njia ya kweli na uzima... na akaongeza kwamba mtu yeyote hawezi kwenda au kumfikia Mungu bila kupitia njia hii au dini hii yani Yesu Kristo....

Yohana 14:6
[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Sasa ni lazima utambue kwamba wale ambao tunasema tunamfuata Yesu ndiyo tunaitwa WAKRISTO..

lakini katika dunia ya Sasa wengi waaitwa wakristo lakini hawamfuati Yesu Kristo Bali wanaenda tu kwasababu walikuta wazazi wao wapo kwenye Hilo... na wengine hawamfuati Yesu kwasababu wameamua kufuata mifumo ya kimadhehebu na kidini kutoka kwa wale waliowafundisha lakini ukijaribu kuilinganisha na Yesu unagundua kwamba haifanani na hapo ndipo tunapata dini mbovu isiyo na maana mbele za Mungu...

Soma hapa👇

Yakobo 1:27
[27]Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

unaona Biblia inatusaidia KUTAMBUA kwamba njia ya kumfuata Mungu iliyo safi ni Ile ambayo inasifa mbili...

1.KUWAJALI WATU HASA WAHITAJI
anaposema kwenda kuwatazama yatima na wajane maana Yake;...
👉kubeba mahitaji ya wengine
 đź‘‰kuwafanya wengine kuwa Bora na kuwapenda Tena hasa wanapokuwa katika taabu
👉kuwapa faraja wasio na faraja
👉kuwasaidia wenye shida...

na tunagundua kwamba hiyo dini yako

 đź‘‰isipokuwa na matendo ya huruma kwa wengine Basi ni njia mbovu
👉Isipokuwa na kuwajali wengine Bali kujiona kuwa ni Bora wala huna mpango na wengine hasa wanaohitaji msaada basi dini yako ni njia mbovu

Yesu yeye ndiye dini yetu na ndiyo maana yeye aliona hata kukaa katika enzi yake haina maana Sana kama wanyonge au wahutaji hawana msaada ....

Wafilipi 2:4-8
[4]Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
[5]Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
[6]ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
[7]bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
[8]tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

unaona kumbe UBINAFSI haukuwepo ndani ya Yesu na haufai kuwepo na kwetu.. na ndiyo maana akasema IWENI NA NIA KAMA ILIYOKUWA NDANI YA YESE... alihitaji kuwakoa wanyonge Hadi akamua kufa yeye.... unaweza kufikiri huo upendo na jinsi alivyowajari wahitaji.......đź‘‹đź‘‹đź‘‹đź‘‹đź‘‹

2.KUJILINDA NA DUNIA
Pia dini yako au njia yako kama ni Safi maana yakeni kwamba italenga wewe uwe na asili ya Mungu yaani utakatifu....

👉ukiona katika dini yako kuna mifumo ambayo inakuelekeza kufanya mambo fulani lakini haikupeleki katika utakatifu bas jua dini hiyo ni chafu mbele za Mungu na hivyo haiwezi kukufikisha kwa Mungu.... kwasababu anayemuona au kumfikia Mungu kwanza ni lazima awe na sura ya utakatifu ndipo aweze kumtazama yeye aliyemtakatifu...

Waebrania 12:14
[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

👉Kumbe kwenye dini yako kunaweza kĂşwa na amri, makatazo, na taratibu nyingi Sana, lakini kama hayo yote hayana nguvu ya kukufanya kuwa mtakatifu basi hayo yote hayana maana mbele za Mungu na wala siyo ya Mungu Bali wanadamu 

Wakolosai 2:20-23
[20]Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
[21]Msishike, msionje, msiguse;
[22](mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
[23]Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

👉kwenye mstari wa 23 Kuna Jambo la msingi Sana kuhusu hayo makatazo na amri ambazo watu wmejitungia na Wala haziwezi kuzuia uovu na tamaa za mwili.....

JE WEWE UNA DINI SAFI?????

Tafakari Hilo na chukua hatua,  achakupoteza muda kwa kuendelea kukaa kwenye madanganyo....

Mungu akubariki Sana

Taifa Teule Ministry 
Min. Mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI