USIWE NA MKONO MLEGEVU


                    USIWE NA MKONO MLEGEVU

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.... karibu katika wakati mwingine tujifunze kuhusu ujumbe huu wa kutokuwa na mkono mlegevu...

Mithali 10:4 Biblia inasema
"Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha"

kufanya kwa mkono mlegevu maana yake ni kufanya mambo kivivu, bila kuweka juhudi katika mambo hayo,
✋Sasa Biblia inatuambia kwamba mtu anayefanya MAMBO kwa namna hiyo lazima atakuwa maskini...
na katika hili ni lazima uelewe kwamba Biblia ya kiswahili haijasema KAZI bali imesema MAMBO...

kumbe unaweza kuwa
👉umeajiriwa au kujiajiri
👉unaweza kuwa mwanafunzi unasoma
👉unaweza kuwa mtumishi kwenye huduma fulani
👉unaweza kuwa kiongozi sehemu fulani
👉unaweza kuwa mzazi katika familia yako..

ni lazima ujue kuwa katika sehemu hizi zote kuna majukumu ya kuyafanya na wahusika waliopo humo wote huwa na lengo moja yaani KUFANIKIWA ILI KUFIKA MALENGO....

neno UTAJIRI, maana yake ni mafanikio ambayo mtu anayalenga pale anapokuwa amejihusisha na shughuli fulani...
na ndiyo maana neno hilo ukilipeleka kati pesa tu au mali tu basi unakuwa umeweka mwanga mdogo sana, tofauti na uhalisia... na ndiyo maana .... MTU ANAWEZA KUWA
👉Tajiri wa pesa
👉mwingine tajiri wa ng'ombe
👉tajiri wa mashamba
👉mwingine ni tajiri wa maarifa na hekima
👉mwingine ni tajiri wa mali fulani

na ndiyo maana utakuta kuna jamii fulani ambayo mtu hana pesa lakini ana ng'ombe nyingi sana, sasa huyo anaitwa TAJIRI WA NG'MBE, lakini neno utajiri linabebwa na Neno mafanikio anayoyapata mtu kulingana na kazi fulani....

KUMBUKA si kila mafanikio ni utajiri bali ili mafanikio yako yaitwe utajiri basi ni lazima yaanze katika kiasi cha kukutosha wewe, kuwa na uwezo wa kuwahusisha wengine bila kuporomoka na pia uwe na akiba kubwa, hapo mafanikio yako yanaweza kuitwa utajiri...

TUTOKE HAPO
Tukirudi katika ujumbe wetu tunaona kwamba Mtu akifanya mambo yake kwa uvivu yaani bila kuwa na juhudi, basi hawezi kuyafaikia mafanikio ya kiasi hicho.... kama wakristo ni lazima tutambue kwamba kujikwamua kwenye hali mbaya ya kiuchumi, kielemu, kiutawala, kiroho n.k inatuhitaji tuwe na juhudi katika kila tunachokifanya...

jambo la msingi katika mafanikio ni kwamba Kila aina ya mafanikio uliyojipangia kuyafikia huwa yana kiasi cha juhudi ambacho kinahitajika ili kuyafikia.., ukiwa na malengo makubwa basi utatakiwa kuwa na juhudi sawa na malengo yako.... lakini wengi sana leo hii wanalalamika mbele za Mungu kwamba maombi yao au malengo yao hayajatimia lakini bila kujua kwamba katika nafasi zao wamekuwa na mikono milegevu, isiyo na nguvu, yaani wanafanya mambo yao bila juhudi..

✊wewe ni mwanafunzi na una malengo makubwa, .. basi soma sana katika wakati wa kusoma
✊wewe ni mfanya biashara,. basi fanya kwa juhudi, habari za kuamka saa mbili ndipo uende dukani au kwenye biashara yako, tambua huo ni mkono mlegevu
✊wewe ni mwajiriwa basi fanya kazi yako ipasavyo ili kufikia malengo yako
✊je wewe umejiajiri? basi hakikisha hufanyi mzaa na mtaji wako, au biashara yako ambayo unaifanya

✊hakikisha unafuata misingi inayotakiwa kwa hicho unachokifanya kwa wakati huo
✊fanya jambo husika kwa wakati husika...

MITHALI 10:5
"Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha"

unaona hapo, kumbe wakati wa kuvuna basi hakikisha unavuna kwa bidii ili wakati wa kula ule kwa raha, ukiwa na uwezo wa kukusanya wakati wa kukusanya basi wewe unafananishwa na mtu mwenye hekima sana kwasababu unafanya kwa juhudi kile unachotakiwa kukifanya ili kufika malengo na ni kwa wakati sahihi...

kuna watu wengi ambao walikuwa wanafunzi na wakachezea fulsa hiyo kwa uvivu, na wengine kupuuzia kile kitu, lakini sasa hivi wanajuta kwanini hawakusoma, HUO NI MKONO MLEGEVU...

Unaweza kujiuliza swali... je kwani kwa sasahivi hawawezi kusoma tena...
jibu ni kwamba WANAWEZA KUSOMA, ILA KWA WAO HUU SI WAKATI WA KUSOMA... na ndiyo maana tunatakiwa kufanya mambo kwa  bidii katika wakati ambao tumepewa maana kuna nyakati ambazo hutaweza kufanya hivyo tena na utabaki kujuta na kulaumu...
👉unapokuwa mvivu leo basi tambua unaandaa umaskini wa kesho
👉usipokuwa na juhudi leo katika masomo yako basi jua unaandaa na kuweka akiba ya ujinga wa kesho

👉Eneo lolote ulipo na unafanya kazi hapo, basi fanya kwa bidii maana kuna siku hutakuwa hapo tena na utakuwa pengine huku ukila matunda ya kile ulichokifanya hapo ulipo sasa

lazima ujue kuwa wakati wa kutafuta ni wakati
✋wenye maumivu makali
✋taabu nyingi
✋mapito mengi
✋milima mingi na mabonde mengi..
lakini hiki ndicho kipindi ambacho hutakiwi kuendekeza usingizi sana maana kikipita bila kufanya kitu basi aibu itakufuata....

hapo ulipo usiwaangalie wenzeka ambao hawajishughulishi bali Muda wote wapo tu wamepumzika, usifikirie kwamba wewe unajiumiza, bali tambua unachokifanya, kinatakiwa kifanywe kwa bidii ili kufikia malengo na wale wanaopumzika leo na kupenda usingizi basi mtakapofika kesho utaziona tofauti zenu....

lazima ujue kuwa kesho yako inaandaliwa leo na wewe mwenyewe... hivyo katika "LEO" hupaswi kuwa na mkono mlegevu....

MUNGU AKUBARIKI SANA

Taifa Teule Ministry
Min. Mathayo Sudai
0744474230/0714732009


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI