HATARI YA MWANAMKE ASIPOFAA,
HATARI YA MWANAMKE ASIPOFAA,
Bwana Yesu asifiwe mabinti….
Moja ya viumbe ambavyo vina uwezo
wa kusababisha madhara makubwa isivyo kawaida ni mwanamke anapotumika tofauti…
๐Mwanamke ndiye aliyemfanya SAMSONI kushindwa na kuishia kunyolewa nywele hata kusudi lake kuishia pale…
๐Mwanamke Yezebeli ndiye aliyemshawishi mfalme ili Eliya afe na akafany wengi kumuabudu mungu baali
๐Mwanamke ndiye aliyesababisha Yohana mbatizaji kukatwa kichwa
Hiyo yote ni kwasababu mwanamke alisimama mahali asipofaa kusimama…
Kama binti ni lazima ujue kwamba madhara ambayo
anaweza kuyasababisha mwanamke huwa ni makubwa na yenye kuumiza sana kuliko
mwanaume.
Hata Adamu hakujua jinsi ambavyo mwanamke ameumbwa, lakini ni ukweli ni kwamba mwanamke amebeba siri kubwa sana ya Mungu na ndiyo maana hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kuwa na nguvu ya kuishi na mwanamke 100% na ndiyo maana hata Biblia ikasema…
Wanaume walichoshauriwa ni
kuwapenda wake zao na kuishi na mwanamke kwa akiri… kwasababu mwanamke ni
kiumbe kisichoweza kueleweka na mtu yeyeto kwa 100% kwasababu ya aina ya siri
ya kimungu aliyonayo mwanamke….
LAKINI PIA
Mwanamke akisimama katika nafasi
yake sahihi basi huwa chachu kubwa sana ya maendeleo na ndiyo maana hakuna
mwanaume mwenye kuweza kufanikiwa katika yote bila kuwa na mwanamke mwenye
hekima…
Pia mwanaume hata kama ana akiri
kiasi gani, hata kama ana pesa na nguvu kiasi gani lakini hana uwezo wa
kuijenga nyumba/familia bali anamuhitaji mwanamke mwenye hekima… na ndiyp maana
Biblia ikasema….
Mithali 14:1 Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Unaona hapo, mwanamke akiwa na
hekima hujenga, lakini ikitokea akawa mpumbavu yaani akasimama mahali pasipofaa
yeye kusimama au kufanya yasiyofaa basi hubomoa….
JE WEWE BINTI NI MWANAMKE GANI……
UNAJENGA AU UNABOMOA?
Mungu akubariki sana
Min. Mathayo Sudai
Maoni
Chapisha Maoni