BINTI UHESHIMU MWILI WAKO



BINTI UHESHIMU MWILI WAKO
Na. Minister Sudai

Kuna wimbi kubwa la mabinti ambao katika namna moja ama nyingine wamekuwa wanashindwa kujua Siri iliyopo kwenye miili Yao hata wamekuwa wakiifanya kama sehemu ya kupata kipato au kupata kibali fulani...

👏Natamani utambue kwamba mwili wako ni wathamani Sana na kwaajili ya Mungu kujidhihirisha wala si kwaajili yako... na wewe yafaa Sana umtukuze Mungu ndani ya mwili wako na si kuuharibu..

1 Wakorintho 6:20
[20]maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu

👏Shetani amewafanya mabinti wengi kudhania kuwa miili Yao inaweza kuwa njia ya wao kupata pesa na ndiyo maana wengi huitoa tu miili Yao ili wapate kirahisi kile wanachokitaka....

👏Kuna mwingine unamkuta yupo kazini na anahitaji kupata kitu fulani au NAFASI fulani lakini unakuta anautoa mwili wake kama rushwa ya ngono ili apate nafas hiyo....

👏KUMBUKA Shetani haoni shida kukupa mamilioni ya pesa na kila unachokitaka ili tu upotee... na anajua njia rahisi ya wewe kupotea ni kupitia mwili wako, yaani anakutia kwenye kifungo ch dhambi.... kwahiyo unakuwa unapata kama ni pesa au NAFASI fulani lakini wewe mwenyewe unapotea... na ndiyo maana Yesu akasema .... 

Mathayo 16:26
[26]Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

👏Kuna mabinti wengine wanatumia miili yao kingono ili wapate mitaji ya biashara

👏Kuna mabinti wengine wanapokuwa wanadaiwa na mwanaume Basi huamua kujisogeza kwa mwaname huyo na kutumia miili Yao kingono kama njia ya kulipa Deni...

👏Binafsi ninaamini kuwa wengi hufikir kwamba jambo hilo wanalifanya muda mfupi tu Kisha wanakuwa hawana Deni Tena... na wengine hujipa kusema hakuna kitu kitatokea kwa wao kufanya hivyo....  

👏Lakini Leo natamani ujue kila ngono utakayoifanya na mwanaume imefanya au kuumba jambo kubwa Sana kwenye maisha yako bila hata wewe kujua....

mfano wa hayo mambo

1. wewe na mwanaume huyo mmeouwa mwili mmoja

2. kila Aina ya matatizo ya kinafsi na kiroho ya huyo Mwanaume lazima yatakuja kwako kwasababu umejenga daraja 

3. Hiyo ni ndoa tayari katika ulimwengu wa roho

na ndiyo maana mabinti wenye tabia hii huwa 

👉hawawezi kuingia kwenye ndoa maana Wana ndoa tayari

👉kama wapo kwenye ndoa basi ndoa huanza kusumbua

👉wengi hulia kwa kushindwa kujua Nini chanzo cha wa kutokusonga mbele...

Hayo yote yanaweza kusababishwa na wewe kushindwa kuheshimu mwili wako na badaa yake unautumia kwa ngono zisizo na msingi...

Mungu mwenyewe ANAUHESHIMU mwili wako na anataka uuweke katika utulivu na utakatifu kwaajili yake

Warumi 12:1
[1]Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

je nawewe Binti umeuwekaje mwili wako?, je unauheshimu?.. kama la! basi tubu dhambi Anza kutembea kwa kuuheshimu mwili wao....

Mungu akubariki Sana
#byministermathayosudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI