USIUPENDE USINGIZI
USIUPENDE USINGIZI Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu karibu siku hii ya leo tutazame ujumbe kuhusu Umaskini.... Mithali 20:13 [13]Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Tunajua Neno usingizi linaenda sambamba na Neno kulala... mtu anaposinzia tunasema AMELALA.. lakini Biblia inatujulisha kwamba tusiwe watu wa kupenda usingizi...Maana yake tusipende kulala... 👉kupenda kitu maana Yake ni lazima utakifanya Sana au muda mwingi unapenda kukifanya.... 👉lakini ukiwa Ni MTU wa kupenda usingizi Biblia inasema utakuwa maskini.... 👉Hii ni kwasababu katika maisha ya hapa duniani tunahitaji muda maalumu kwaajili ya kufanya Mambo maalumu... Tena tusipoutumia muda huo maalumu Basi ni lazima utambue kuwa huo muda haurudi na lile ulilotakiwa kukifanya kwa muda huo hautalifanya Tena au la utahitaji muda mwingine ili kulifanya ambapo huo muda ulikuwa Ni kwaajili ya Jam...