USIISHI NA KIJANA NDANI KABLA YA NDOA
Bwana Yesu asifiwe mabinti wazuri wa Mungu
leo Ni siku nyingine natamani ujifunze na kutenda Jambo sahihi kwenye maisha yako....
leo tuangalie tabia ya ajabu iliyozuka kwa vijana na mabinti wengi...Ni kuhusu
KUISHI NA MTU NDANI KABLA YA NDOA...
1 Petro 4:2-3
[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
unaona hapo..kumbe Kuna utaratibu wa dunia hii ambao upo kinyume na utaratibu ambao Kristo anataka watu wake waenende...
👉Sasa katika swala la ndoa ni lazima ujue kuwa upo utaratibu mzuri tu ambao watu wa Mungu ni lazima waufuate...na utaratibu huo Ni mzuri na Ni mwepesi Sana kuufuata kwa Wana wa Mungu...
Mathayo 11:29-30
[30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
👉ukiona taratibu za Mungu zinaonekana Ni ngumu kwako wewe kuzifuata Basi usijidanganye kwamba umeokoka Bali ukiweza kaokoke upya kwasababu waliookoka hawaumii kuzifuata kanuni za Mungu.....👉Sasa Kuna tabia ya mabinti wengi kuishi na wanaume ndani kwa kigezo Cha kuwa wanajiandaa kuoana....hiyo Ni tabia mbaya Sana kufanywa na Binti wa kikristo...
👉Binafsi nimeshuhudia mabinti wengi ambao walikuwa watumishi wazuri lakini leo wamekuwa maadui wa Mungu kwa kuupenda utaratibu wa dunia hii...
👉Utaratibu wa dunia unawaruhusu watu kuanza kuishi pamoja wakishakubaliana tu lakini Mungu Hana utaratibu huo...
👉Ndoa Ni lazima ianze kabla ya tendo la ndoa
👉Wengi wanajidanganya kwa kudhani hao wanaume ndiyo watakaowaoa lakini hawajui kuwa thamani ya kitu kwa mkristo huonekana pale ambapo kristo amehusika kwenye Hilo Jambo..
Hivi karibuni Kuna kitu nimekutana nacho Hadi nikashangaa ...NI HIVI👇
KUNA BINTI ALIKUWA MTUMISHI MZURI TU HAPO MWANZO...SASA BAADA YA MUDA KIDOGO ALIANGUKIA KWENYE MAPENZI NA KIJANA MMOJA WA KAWAIDA TU...YULE KIJANA ALIKUJA KAMA MKRISTO MZURI LAKINI KUMBE KUNA JAMBO ALIKUWA ANALITAKA..MWISHO WA SIKU TUKAONA BINTI KAACHA KUJA KWENYE MAOMBI YETU KAMA KAWAIDA .....BAADAE TUKAPATA TAARIFA KUWA BINTI ANAISHI NA KIJANA HUYO KWENYE NYUMBA MOJA KAMA MKE NA MUME...BINAFSI NILIJARIBU KUMFUATILIA BINTI KWA UKARIBU KUONGEA NAE LAKINI BINTI HAKUTAKA KUSIKILIZA WALA KUACHANA NA NJIA HIYO MBOVU...
SI HIVYO TU LAKINI PIA YALE YOTE NILIYOKUWA NAONGEA NAE KWA LENGO LA KUMFUNGUA MACHO... YEYE BINTI ALIKUWA ANAMWAMBIA YULE KIJANA KILA KITU NA KWAMBA MIMI NAMSUMBUA NAKUMFANYA AISHI BILA AMANI....
MARA YA MWISHO KUONGEA NAE NI BAADA YA KUPATA TAARIFA KUWA KUNA WATU WANAMSEMA KWAMBA ALIJIFANYA AMEOKOKA SASA IKO WAPI NA WANAJIVUNIA KWAMBA AMETOKA KWENYE WOKOVU.......BAADA YA MIMI KUPATA TAARIFA NILIMTAFUTA TENA KUONGEA NAE....LAKINI SIKU HIYOHIYO AKAMWAMBIA HUYO KIJANA KWAMBA MIMI NIMEMWAMBIA KUWA AMEACHA WOKOVU NA AMEHAMA KANISA KUMFUATA HUYO KIJANA PASIPO KUJUA KWAMBA NILIKUWA NALINDA USHUHUDA WAKE...
KESHO YAKE ASUBUHI YULE KIJANA AKANIFUATA AKIWA NA HASIRA KWELI...ALIANZA KUNIAMBIA MANENO AMBAYO YA DHARAU NA KUSISITIZA KUWA NIMUACHE HUYO BINTI MAANA YEYE ANAMUANDAA KUWA MKE WAKE....BAADAE TULIMALIZA KWA AMANI HUKU NIKIKUMBUKA YOHANA ALIKATWA KICHWA ENZI ZA HERODE KWASABABU YA MWANAMKE AMBAYE ALIKUWA AKIFANYA UJINGA KAMA HUO.....
Sasa Hadi kufikia hapo niligundua kuwa Binti mwenyewe anapenda kufanya hivyo na ndiyo maana hataki tumfuatilie ....
👉mpaka Sasa hajali kuupoteza USHUHUDA na ANAISHI Kama kawaida na huyo kijana...
👉Watu wamekuwa wakisema mengi kiasi kwamba utumishi unatukanwa...
👉lakini ashukuliwe Mungu kwakuwa yeye humlipa kila mtu sawasawa na atendavyo...
BINTI
👉Kijana akikuheshimu hatakuvua nguo bila utaratibu👉hatakufanya uishi Kama kahaba
👉kijana akikuheshimu na kukupenda Basi atawafuata wazazi na atakuja madhabahuni kukuonyesha Heshima
👉 kijana akikuheshimu hawezi kuishi na wewe ndani angali wazazi wako na mchungaji wako hajui....
👉kuishi hivyo Ni DHARAU kubwa sana mbele za Mungu hasa kwa wewe Binti mkristo...
👉hata wewe Binti lazima ulinde Heshima yako na utambue kwamba wewe sio jalala la kubeba takataka bila utaratibu....
NIMESHUHUDIA MABINTI WENGI WAKILIA MPAKA LEO WAKIJUTA KWAKUTOKUBALI KUSIKILIZA KILE ANACHOKITAKA MUNGU...WANATAMANI SIKU ZIRUDI NYUMA LAKINI HAIWEZEKANI .......DHAMBI HIYO YA KUISHI NA MTU BILA NDOA IMEACHA MACHOZI KWA WENGI HADI SASA.....
Jilinde Binti yangu mzuri.....Mungu anakupenda..
Mungu akubariki Sana
Mwl/Ev. Mathayo Sudai
0744474230/0714732009
Maoni
Chapisha Maoni