USIUPENDE USINGIZI


                       USIUPENDE USINGIZI

Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu

karibu siku hii ya leo tutazame ujumbe kuhusu Umaskini....


Mithali 20:13

[13]Usipende usingizi usije ukawa maskini; 

Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.


Tunajua Neno usingizi linaenda sambamba na Neno kulala...

mtu anaposinzia tunasema AMELALA..

lakini Biblia inatujulisha kwamba tusiwe watu wa kupenda usingizi...Maana yake tusipende kulala...

👉kupenda kitu maana Yake ni lazima utakifanya Sana au muda mwingi unapenda kukifanya....

👉lakini ukiwa Ni MTU wa kupenda usingizi Biblia inasema utakuwa maskini....

👉Hii ni kwasababu katika maisha ya hapa duniani tunahitaji muda maalumu kwaajili ya kufanya Mambo maalumu...

Tena tusipoutumia muda huo maalumu Basi ni lazima  utambue kuwa huo muda haurudi na lile ulilotakiwa kukifanya kwa muda huo hautalifanya Tena au la utahitaji muda mwingine ili kulifanya ambapo huo muda ulikuwa Ni kwaajili ya Jambo lingine...


kumbuka kila Jambo lafaa lifanyike kwa wakati wake...


Mhubiri 3:1

[1]Kwa kila jambo kuna majira yake, 

Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.


👉Kuna wakati unatakiwa kusoma itakubidi usome na si vinginevyo

👉Kuna wakati unatakiwa kuoa au kuolewa, Basi inakufaa ufanye hivyo bila kuchanganya nyakati...

na ufahamu usipofanya Jambo kwa wakati sahihi Basi jua Kuna Jambo umelipoteza....

👉Sasa moja ya Mambo ambayo hupoteza muda ni pale mtu anapopenda Sana kulala ...maana muda mwingi atakuwa yupo usingizini hata kushindwa kujihusisha na Mambo mengine ya kumuongezea kipato, hekima au hata maarifa ambayo yangefaa kwaajili ya Jambo fulani...hivyo anakuwa MASKINI

👉KUMBUKA maskini haina maana kukosa Pesa, Bali ni kukosa maarifa ya kuendesha na jinsi ya kutumia hata kile ulichonacho.....


Tena Kama Ni mkristo unayeelewa habari ya Mambo ya roho, Basi utaungana na Mimi nitakaposema kwamba Umaskini Ni roho....

lakini roho hii haihitaji maombi kukemewa ili itoke Bali inahitaji maarifa, Utendaji kazi, nidhamu pamoja na kutii Sheria zote za Mungu za kukifanya kuwa tajiri....


lakini Usingizi Ni silaha kubwa ya Shetani katika kumfanya mtu kuwa maskini kwasababu anajua ukipenda usingizi maana Yake hutahusisha akili na nguvu zako katika Utendaji wa majukumu....

👉unaweza kuwa maskini kimaisha

👉unaweza kuwa maskini wa maarifa

👉unaweza kuwa maskini wa hekima

👉unaweza kuwa maskini wa Mambo ya rohoni n.k


Lakini katika hayo yote huletwa na tabia ya watu kulalalala bila kupenda kujishughulisha...

👉unaweza kukuta MTU usiku amelala na mchana pia analala ...Sasa mtu wa namna hiyo ni hatari Sana maana ni lazima atakuwa maskini...

đź‘‹Ukiona mchana huna la kufanya pengine majukumu yameisha Basi lazima ujue huo so muda wa kulala Bali fanya Jambo lingine ili kuukomboa wakati.....kwa mchana Kama hivyo unaweza kuwa hata na kitabu chako kizuri na ukaanza kukisoma ili kupata kitu Cha baadae...au unaweza kuchukua muda kidogo kusikiliza mahubiri mazuri ya uzima..au unaweza kupita kwenye nyaraka tofauti za mafundisho ya kiMungu ili kujifunza....

 đź‘‹Ni lazima ufahamu muda umepangwa mahususi kabisa na kila Jambo lina wakati wake.....USITUMIE MUDA WOTE KULALA

đź‘‹Mtu anayeshindana na usingizi Ni mtu anayesshindana na Umaskini

👋hata matajiri ambao wamewahi kutokea na wale waliopo Basi tambua hawakupenda usingizi Bali walipambana na usingizi kiasi kwamba hata muda wa kulala haukuwepo kwao yaani walijibana kweñye kipengele cha muda na ndiyo maana wapo kama walivyo...

đź‘ŹHuwezi kuwa MTU wa unayemtazamia Kama sehemu kubwa ya muda wako unautumia kulala .....

đź‘ŹKama Ni huduma basis jua unatakiwa ujifunze sana na kwa muda mwingi kabla ya Mungu kukutumia...

đź‘Źkama Ni Biashara ni lazima utumie muda mwingi kusoma na kuifahamu Wala si kwa pupa...

👏usikubali kufañya kitu kwa pupa Bali fanya kwa bidii


Mithali 21:5

[5]Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; 

Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.


 đź‘ŹIli ufĂ nikiwĂ© na kuifikia ndoto yako Basi añza kupiga vita usingizi ...lala kwa wakati sahihi fanya kazi kwa wakati sahihi....


MUNGU akubariki Sana


Taifa Teule Ministry

Mwl/Ev. Mathayo Sudai

0744474230/0714732009

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI